Bosi wa Reli, ATCL na TANESCO mnasubiri nini ofisini?

Shakari

Senior Member
Jul 6, 2022
157
440
Ripoti za CAG na TAKUKURU zilizowasilishwa mbele ya Rais Mapema leo Machi 29, 2023 zimeonyesha ufisadi mkubwa katika Mashirika Makubwa ya TRC, ATCL na TANESCO, Mhe Rais amesema waondoke swali je mnasubiri nini?

ATCL
“Kuna mradi hapa tumetengeneza Ndege ya mizigo ambayo tunakaribia kuipokea, last Installments ilikuwa tulipe dola milioni 37, invoice imekuja dola milioni 86….. unauliza mkataba ulisemaje? hii imetokana na wapi?, ooh vifaa vimepanda bei, vipi? mkataba wetu ulisemaje”

“Na bado aliyepokea anakuletea Serikalini hii ilipwe ndio invoice tumepokea….. stupid, ulipopokea umechukua hatua gani? umeuliza nini? umefanya nini? ukilitazama kwa undani hili ongezeko limeanzia huku ndani kuna Watu wameongea huko”

“Hatuwezi kwenda hivyo na nadhani hawa wanaopokea hizo invoice wakazileta kwa raha zao kabisa Serikalini watupishe, hawafai kuwa kwenye hizo nafasi, kama wanafaa angepokea huko akalihoji” Rais Samia.

TANESCO
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamduni amesema Takukuru ilidhibiti hasara ya Sh81.99 bilioni ambayo Serikali ingepata kutokana na Shirika la Umeme Tanesco kutozingatia masharti ya mkataba baina yao na Kampuni ya Pan-African Energy Tanzania (PAET).

TRC
TRC ILIMKATAA MZABUNI WA TSH BILIONI 616.4 NA KUMPA WA TSH. TRILIONI 1.119 BILA SABABU ZA MSINGI

Akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo mbele ya Rais Samia, Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema uamuzi huo ulisababisha ongezeko la matumizi ya Tsh. Bilioni 503.2 (82%) lisilokuwa na ulazima

Pia, katika ununuzi wa 'Locomotives' na Makochi ya Abiria, Shirika la Reli (TRC) lilitekeleza Mkataba bila dhamana ya Utendaji na kusababisha hasara ya Tsh. Bilioni 13.7 kutokana na Mkandarasi kushindwa kutimiza Masharti ya Mkataba

Aidha, CAG Kichere amesema Ukaguzi wake umebaini uwepo wa Manunuzi yenye Gharama Kubwa, Upotevu wa Fedha na Majadiliano ya Mikataba Yasiyolinda Maslahi ya Taifa na kusababisha kutofikiwa kwa Malengo yaliyokusudiwa
 
Screenshot_20230329-183252.png
 
Mama ameongea kwa uchungu sana jinsi pesa ya umma inavyoibiwa,

Tatizo yeye hatakiwi kulalamika!anatakiwa achukue hatua,aseme" juzi Kuna watu wameiba pesa,nimefukuza wote,na wapo ndani,mpaka walipe pesa yote,na mali zao nimezitaifisha."

Wazungu wanasema the "buck stops at her".

Hakuna mwingine wa kuwawajibisha wale wanaotakiwa kuwajibisha wengine,ni yeye tu,ndani ya nchi hii,hakuna mwenye madaraka zaidi ya Samia,hatakiwi kulia Lia,kusema nendeni mkatende.

Sasa bill ilikuwa bilion 37,inakuja 86!huyo aliyeileta,anayeipokea,anayelipa wote ni wizara ya fedha,sasa kwanini watu hawafukuzwi?

Analalamika madiwani wamefisadi pesa ya mikopo,madiwani ni WA ccm,waliingia kijambazi kwa wizi wa kura,sasa anategrmea Nini?

"The genie is out of the bottle",she should not be crying or asking who. Ginner put it back!!it's her job,she is failing miserably and has been all allong
 
Baada ya muda hizi habari zitakuwa zimepita na watu wataendelea kupiga hela.

Hata mimi nitawashangaa sana watakaokuwa kwenye nafasi za upigaji kisha wasipige. Iwapo watu wanafanya hivyo hivyo miaka yote, na hakuna hatua yoyote ya maana wanachukuliwa, huku wananchi wakiishia kupiga kelele mitandaoni, yaani uache upigaji ili iweje labda?
 
Back
Top Bottom