Bosi wa kampuni ya Nissan atoweka Japan baada ya kushtakiwa kwa kukiuka kanuni za fedha

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,216
7,907
Aliyekuwa bosi wa kampuni ya kutengeneza magari ya Nissan, Carlos Ghosn ametoweka kitatanishi nchini Japan, ambako ameshtakiwa kwa kukiuka kanuni za fedha na sasa yuko Lebanon huku polisi wa kimataifa, Interpol wakitoa taarifa ya kumsaka.

Kigogo huyo alitoweka Japan akiwa nje kwa dhamana, ambayo awali ilipingwa vikali na upande wa mashtaka.

Haijafahamika aliondokaje Japan, lakini serikali ya Ufaransa, ambayo ilisema haikujua mipango ya bosi huyo wa zamani wa Renault kutoroka nchini Japan, ilisema tajiri huyo alinufaika na ofisi ya ubalozi wake jijini Tokyo.

“Mamlaka za Ufaransa hazikutaarifiwa kuhusu kuondoka kwake Japan na haikuwa na taarifa kuhusu mazingira ya kuondoka huko,” ilisema wizara ya mambo ya nje, ikiongeza kuwa ilipata taarifa hizo katika vyombo vya habari.

Lakini taarifa hiyo inasema Ghosn alinufaika na usaidizi wa ofisa ubalozi wa Ufaransa jijini Tokyo, na kwamba kulikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara baina ya ofisi ya ubalozi, Ghosn na wanasheria wake.

“Hali yake, pamoja na maombi ya baadhi ya kanuni za kisheria zilifuatwa kwa umakini wakati wote na ubalozi wetu mjini Tokyo,” ilisema wizara hiyo.

Ghosn, ambaye ana uraia wa Ufaransa, Lebanon na Brazil, aliamriwa kusalimisha hati zake za kusafiria ikiwa ni sehemu ya masharti ya dhamana yake baada ya kukamatwa mwezi Novemba, 2018 jijini Tokyo.

Kigogo huyo wa Nissan mwenye umri wa miaka 65 anakabiliwa na mashtaka ya kutangaza mshahara wake wa mamilioni ya dola chini ya kiwango wakati akiwa mwenyekiti wa Nissan, ambayo ni mshirika wa kampuni ya kutengeneza magari ya Ufaransa, Renault.

Ghosn pia anatuhumiwa kuhamishia hasara zake binafsi katika kampuni ya Nissan.

Ukosefu wa taarifa kamili kuhusu kutoroka kwake kumeibua ubashiri kuhusu jinsi mtu huyo maarufu alivyofanikiwa kuondoka.

Alitakiwa kuweka dhamana ya dola 13.4 milioni za Kimarekani kabla ya kesi yake iliyopangwa kusikilizwa mwaka huu. Akihofiwa kuwa angeweza kutoroka, alitakiwa asalimishe hati zake tatu za kusafiria na kuwekwa chini ya uangalizi mkali na aliwekewa masharti mengi ya kutumia simu zake na kompyuta.

Asingeweza kutoka nyumbani kwake kwenda kununua maziwa bila ya kuonekana, lakini akatoweka.

Kuna hisia nchini Japan kuwa alisafirishwa kutoka Japan kwa kuwekwa kwenye boksi la vifaa vya muziki, baada ya kundi la muziki kutumbuiza nyumbani kwake.

Lakini wengine wanasema alitumia hati ya kughushi ya kusafiria, kwa mujibu wa jarida la Ufaransa la Les Echos.

Hata jijini Tokyo. Ghosn alikuwa na tabia ya kupotosha taswira yake. Wakati akitoka mahabusu baada ya kuachiwa kwa dhamana, alivalia kama fundi katika jitihada za kukwepa vyombo vya habari. Alivaa kofia ya bluu na kuziba uso na kinyago.

Wakati akifikishwa mahakamani, alitimuliwa kutoka Nissan na kampuni ya Mitsubishi Motors, kampuni ya tatu ambayo ilikuwa katika umoja aliounda, na baadaye kujiuzulu utendaji mkuu wa Renault.

Ghosn alithibitisha yuko Lebanon, Jumanne iliyopita na kulaumu mfumo wa haki wa Japan.

“Sasa niko Lebanon na sitawekwa ndani na mfumo usio wa haki wa Japan ambako hatia huamuliwa mapema (kabla ya mashtaka), ubaguzi ni mkubwa na haki za msingi za binadamu zinakiukwa,” alisema tajiri huyo.

“Sijakimbia haki, nimekimbia ukosefu wa haki na mashtaka ya kisiasa,” alisema Ghosn, akiongeza kuwa anaweza kuongea kwa uhuru na vyombo vya habari, kitu ambacho aliahidi kukifanya kuanzia wiki ijayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzetu mission zao ni za hali ya juu sisi hata kuku tu tunashindwa kukamata kistarabu
 
hata sisi tunao mkuu na huwa hazi fail unakumbuka tulimludisha rais wa burundi madarakani juzi kimafia
😂😂😂 Tena mkuu umenikumbusha mbali maana siku hiyo ilikuwa ni majira saa 12 jioni nikiwa zangu wilaya Bukombe mkoani geita mmmmh acha niishie hapa nilihisi move za akina John Rambo
 
😂😂😂 Tena mkuu umenikumbusha mbali maana siku hiyo ilikuwa ni majira saa 12 jioni nikiwa zangu wilaya Bukombe mkoani geita mmmmh acha niishie hapa nilihisi move za akina John Rambo
watu wanaichukulia poa sana nchi yetu hasa sisi watanzania tunajifanya wajuaaji ila kuna wanaume wako porini huko wanapambana ili sisi tunywe bia kwa raha huku mjini. Na saizi tumepata huyu rais ndio heshima imezidi manake wanamjua huwa hacheki na kima
 
Nilipoona alikua na mawasiliano ya karibu na ubalozi wa Ufaransa..... Pia alikua kigogo wa Renalt ambayo ni Icon company ya ufaransa nakajua tuu TAYARI watu wa system wamehusika kukamilisha mpango?!
 
watu wanaichukulia poa sana nchi yetu hasa sisi watanzania tunajifanya wajuaaji ila kuna wanaume wako porini huko wanapambana ili sisi tunywe bia kwa raha huku mjini. Na saizi tumepata huyu rais ndio heshima imezidi manake wanamjua huwa hacheki na kima
😂😂😂😂😂😂
 
watu wanaichukulia poa sana nchi yetu hasa sisi watanzania tunajifanya wajuaaji ila kuna wanaume wako porini huko wanapambana ili sisi tunywe bia kwa raha huku mjini. Na saizi tumepata huyu rais ndio heshima imezidi manake wanamjua huwa hacheki na kima
Lile onyesho la kumuokoa VIP leader siku ile ya Uhuru pale kirumba! Dah!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii movie kila mtu anasema yake wapo wanaodai waliona msafara wa kumrudisha nkurunzinza ikipitia ngara na kigoma pia hiyohiyo siku ulionekana msafara mwingine
Tena mkuu umenikumbusha mbali maana siku hiyo ilikuwa ni majira saa 12 jioni nikiwa zangu wilaya Bukombe mkoani geita mmmmh acha niishie hapa nilihisi move za akina John Rambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii movie kila mtu anasema yake wapo wanaodai waliona msafara wa kumrudisha nkurunzinza ikipitia ngara na kigoma pia hiyohiyo siku ulionekana msafara mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu asikudanganye mtu msafara ulipitia dar, moro, Dodoma, Singida, Tabora kwenye wilaya zake Igunga na Nzega Shinyanga sehemu ya Tinde na Kahama theni Geita kwa upande wa wilaya mbili Mbogwe na Bukombe then Biharamlo sehemu ya Nyakanazi to Nyakahura Mnzani Then Ngara to Boder ya kabanga anaebisha anyooshee mkono nimuulize maswali magumu yasiyo na majibu hata mimi mwenyewe siwezi jibu
 
Back
Top Bottom