Bosi mpya Uhamiaji chukua hatua wasaidizi wako watakuangusha

Rihana

JF-Expert Member
Apr 26, 2013
498
250
Nimekwenda Uhamiaji Kurasini kwa lengo la ku renew passport yangu. Taratibu zote zilifanyika bila kikwazo chochote wala mizengwe yoyote. Niliambiwa nirudi baada ya wiki ili kuchukua passport yangu. Nilivyorudi naambiwa hamna vitabu vya kuchapia passport, wakati huo huo baadhi ya watu tuliowakilisha nao maombi wamepata. Hivi kweli taasisi kama Uhamiaji inawezaje kuishiwa vitabu vya kuchapa passport?

Tafadhali Mheshimiwa Kamishna Jenerali chukua hatua.

Tunakuamini ni mchapa kazi na mtenda haki.
 
Hawa watu wapuuzi saana. Wanaliaibisha taifa mkuu...

Yaani Kurenew pass ichukue 4 weeks kweli. Wamenikera pia. Mara sababu mashine ni moja mara hamna vitabu.

Hata kama vitabu wanaagiza lakini wawe serious na maisha ya watu.
 
Ninakumbuka Enzi ninapata passport yangu ya kwanza pale uhamiajia, zilikuwa zinaandikwa kwa mkono, kitabu cha kijani kinaganda gumu na kidirisha. Kuna mtu alikuwa ana mwandiko mzuri sana, usiombe awe likizo hao wengine ni mcharazo. Sikuhizi ni mambo ya biometric.
 
Sawa kabisa Mkuu Daby mimi nimeshangaa sana
 
Sawa kabisa Mkuu Daby mimi nimeshangaa sana
Tanzania nchi kubwa watu wanasafiri kila siku wengine wagojwa , tunatafuta riziki, biashara, kusoma nk..sasa kumcheleweshea mtu pass kwa zaidi ya week ni kuchelewesha mipango ya mtu na ukishaharibu mipango unaharibu future ya mtu. pole lakini.

Aseeh huyo mama abadilishe wasaidizi wake.
 
Ninakumbuka Enzi ninapata passport yangu ya kwanza pale uhamiajia, zilikuwa zinaandikwa kwa mkono, kitabu cha kijani kinaganda gumu na kidirisha. Kuna mtu alikuwa ana mwandiko mzuri sana, usiombe awe likizo hao wengine ni mcharazo. Sikuhizi ni mambo ya biometric.
Picha inabandikwa eeh!
 
mimi passport yangu imeisha tokea tarehe 17 najiandaa kisaikolojia na majanga nitakayokutana nayo huko Mungu anisaidie tu maana hawa watu hawana maana kabisa!
 
Ninakumbuka Enzi ninapata passport yangu ya kwanza pale uhamiajia, zilikuwa zinaandikwa kwa mkono, kitabu cha kijani kinaganda gumu na kidirisha. Kuna mtu alikuwa ana mwandiko mzuri sana, usiombe awe likizo hao wengine ni mcharazo. Sikuhizi ni mambo ya biometric.
Hahahahaha nimecheka sanaaaaaa ,umenikumbusha mbali hyo micharazo ilkuwa kiboko.
 
Nimekwenda Uhamiaji Kurasini kwa lengo la ku renew passport yangu. Taratibu zote zilifanyika bila kikwazo chochote wala mizengwe yoyote. Niliambiwa nirudi baada ya wiki ili kuchukua passport yangu. Nilivyorudi naambiwa hamna vitabu vya kuchapia passport, wakati huo huo baadhi ya watu tuliowakilisha nao maombi wamepata. Hivi kweli taasisi kama uhamiaji inawezaje kuishiwa vitabu vya kuchapa passport? Tafadhali Mheshimiwa Kamishna Jenerali chukua hatua. Tunakuamini ni mchapa kazi na mtenda haki!!
Sio hao tu. Wiki mbili zilizopita nilienda TRA kijitonyama kurenew driving licence nikafanikiwa kufanya process zote siku iyo iyo. Wakaniambia baada ya wiki 2 niende. Nimeenda jana wananiambia eti hakuna material so nisubiri wiki 2 nyingine ndo niende kufuatialia tena. Hii ni kero kubwa sana yani taasisi kama TRA kuishiwa material tena material yenyewe makadi tu kuchapia leseni
Shame.
 
Nimekwenda Uhamiaji Kurasini kwa lengo la ku renew passport yangu. Taratibu zote zilifanyika bila kikwazo chochote wala mizengwe yoyote. Niliambiwa nirudi baada ya wiki ili kuchukua passport yangu. Nilivyorudi naambiwa hamna vitabu vya kuchapia passport, wakati huo huo baadhi ya watu tuliowakilisha nao maombi wamepata. Hivi kweli taasisi kama uhamiaji inawezaje kuishiwa vitabu vya kuchapa passport? Tafadhali Mheshimiwa Kamishna Jenerali chukua hatua. Tunakuamini ni mchapa kazi na mtenda haki!!
Unaandaliwa mazingira ya rushwa ila unajidai huelewi!
 
Kumbe hili tatizo ni sehem nyingi...kuna benki nilienda kuomba cheque book mwezi mzima eti vendor ameishiwa material
 
Poleni wote mliokutwa na hilo janga.

Tusisahau pia dereva hasikii kelele zetu.
 
Sasa hivi CORRUPTION IMERUDI UPYA UHAMIAJI na hii inasababishwa na kuwa na staff wengi mno mfano hapa Arusha. Ile transparency iliyokuwepo miaka 5 iliyopita ambapo mtu alikuwa anapata passport fasta haipo tena bali umerudi ule ubabaishaji wa maiaka 1990s
 
Kuna idara nyingine za serikali ni nanga za kuzuia maendeleo. Mojawapo ni hii fikiria wanayotimua mipango ya watu kusafiri
 
Back
Top Bottom