Bosi mnoko kakukuta nawe ni bosi mahali pengine...........!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,806
15,373
Hebu chukulia kwamba mtu aliyekunyanyasa mpaka ukaamua kuacha kazi wakati akiwa Bosi mahali fulani, umekutana naye hivi sasa akiwa anatafuta kazi mahali ambapo wewe ni Bosi na ukiwa na maamuzi ya mwisho. Hebu niambie kama ni wewe ungefanya nini?
 
Kama utendaje wake ulikuwa ni mzuri, nitamchukua, uzoefu unaonyesha Boss anayeonekana kuwa mnoko kwa watu walio chini yake mara nyingi anakuwa muhimu kwa Kampuni au shirika. Kwa difinition yangu mnoko ni mtu ambaye hataki taratibu zilizowekwa zikiukwe. Sasa ni boss gani mzuri apendaye taratibu zikiukwe?
 
Mtu anayependa taratibu za kazi zifuatwe hanyanyasi watu..............................
 
Mtu anayependa taratibu za kazi zifuatwe hanyanyasi watu..............................
Mtu anayejua kazi yake na taratibu zoote anafuata hanyanyasiki utamuanzia wapi? Hebu jiulize upo ofisini unafanya kazi zako vizuri na unafuata taratibu zoote mbona ni kazi sana boss wako kukunyanyasa? na kama atafanya hivyo it means hayupo sawa kiakili, na hajui nini anatakiwa kukifanya. Na mtu wa namna hiyo hakuna haja hata ya sisi kumjadiri hapa, kwasababu jibu ni kwamba hafai inatakiwa ufanye maamuzi ya kutokumuajiri basi, au unataka uende mbali zaidi na kumpaka?
 
unamwajiri halafu unakuwa unamsikilizia jinsi atakavyokuwa anajiongeza we burdani tu..
 
Mkuu mbona hauleweki,ebu weka wazi mara ulifukuzwa chuoni mara mkuu aliosababishwa ufukuzwe kazi,vipi tena funguka la moyoni::
 
mara nyingi wafanyakazi wengi wanajinyanyasa wenyewe kabla ya boss na ukiona boss kakufuatilia kidogo tu utalalamika unaonewa lkn wewe kama wewe ndo chanzo ... kuhusu ajira nitamwajili kama kawaida na nitaangalia utendaji kazi wake maana nitakuwa namfahamu vizuri ila kama utendaji wake haukuwa sahihi basi atakuwa na udhaifu wa kuficha makosa yake na kuandama wengine hapo sitakuwa na sababu ya kumwajiliu
 
Mkuu mbona hauleweki,ebu weka wazi mara ulifukuzwa chuoni mara mkuu aliosababishwa ufukuzwe kazi,vipi tena funguka la moyoni::

Kwani aliyefukuzwa chuoni hawezi kujiendelea na masomo na kuja kuwa Boss? ndio maana kuna msemo unaosema, "Mlango mmoja ukifungwa, kuna mwingine umefunguliwa pembeni yako......................"
Mimi sikuwa mjinga, niliangalia fursa nyingine na maisha yakaendelea.....................

Anyway, huo ulikuwa ni mfano tu, lakini haunihusu kwa namna yoyote............................ Umeelewa eh!
 
kama sifa zinazotakiwa anazo sinabudi kumwajiri na wala siwezi kumtendea vibaya kama yeye alivyokuwa akinitendea, na hii kumtaka tu ajifunze kutoka kwangu kwamba ni namna gani Boss anavyotakiwa kuwa siku zote..
 
Kazi nyingine zinahitaji wanoko ili ziende, ukiwa liberal hamtamfika popote, mi ntamuajiri

Halafu anakutilia unoko, wewe unafukuzwa na yeye anachukua nafasi yako...................................
 
CHANGANYA NA ZAKO!
Mpaka hapa kwenye hii post tayari unajua kuwa aidha wewe ulikuwa mzembe fulani kazini, au bosi alikuwa hakutaki uwepo kazini!
Mwajiri tu, lakini fuata sheria zote za ofisi yako, kama utamwogopa au kumpendelea au kumnyanyasa bila sababu, then ujue tayari ushaanguka majaribuni...hutakuwa na tofauti na yeye!
 
Namwajiri,na pia natumia fursa hiyo kumuonyesha ni jinsi gani nilivyo si kwa ubaya isipokuwa kwa wema tu.

kwani kufanya hivyo,inaweza ikawa nafasi ya yeye kugundua mapungufu yake na ikawa 7bu ya yeye kubadirika na kujutia kile alichokufanyia hapo awali. Siku zote tunatakiwa tufahamu kuwa jambo baya hulipiziwa kwa jema.
 
sio rahisi kufanya nae kazi kwa mtu kama huyo na yeye pia hatakuwa free hapo ofisini kiutendaji kutokana na kukumbuka yaliopita.kwangu mm sitaku wa huru kumwajiri kama nlikuwa nafanya kazi kwa haki lkn akanifukuza kwa majungu,
 
Mkuu mbona hauleweki,ebu weka wazi mara ulifukuzwa chuoni mara mkuu aliosababishwa ufukuzwe kazi,vipi tena funguka la moyoni::

Mkuu mimi naamini mtu anapoleta mada si lazima iwe imemtomkea mwenyewe wakati mwingine amekiona hicho kitu au kuna mtu amemshirikisha so anaamua kuileta ili apate mawazo kutoka kwa watu mbalimbali.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom