Bosi Kampuni Binafsi abainika Kuangalia wanawake nyeti zao wakiwa Chooni

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,095
2,429
Mnisamehe tu maana najua kuna watu wakiona tu bandiko langu mioyo yao inakunjamana."jamaa kabandika tena aargh..." msini mind mimi mengi yananipata na mengine nasimuliwa maana najichanganya sana na watu hivyo sikosi ubuyu kwa wadada na kashata wa wakaka.ukicheki begi langu la begani lina vitu hivyo kila wakati maana mimi kambi popote. sichelewi kuahirisha safari kumkimbizia demu au kukaa kusikiliza habari za mjini. labda na kazi yangu inaniruhusu pia si unajua sisi wengine tunafanya kazi za kutumwa tumwa.

jana nmekaa na watu flan meza moja tunapata msosi wa mchana kijimgahawa flan hivi kitovuni mwa jiji. mara wakaja wadada watatu wanaongea mmoja sura yake ikiwa imeiva kweli kweli kwa hasira na midomo ikimtetemeka.kilichonifanya nimtizame sana ni kuwa alikuwa kabisa anaonekana ana hasira utadhani alimeza moto sasa anataka kutapika halafu koo linagoma kufunguka..

walipokaa ndo mmoja akaanza kusema kwa sauti ya kawaida ila yenye hasira "tuleni kwanza ili tupate nguvu halafu tumwendee yule hayawani akatueleze toka ameanza kuangalia nyuchi zetu ame pee mara ngap na ole wake iwe mmoja wetu kapata mimba kwa ujinga wake huo" nikashtuka kidogo... mmoja akasema "hebu chiku twambie ilikuaje " nami nikaona hapo siwezi kosa lakuja kushare nanyi waungwana humu kwenye masuala la mahusiano,mapenzi na urafiki.ukiwa na jambo zuri unashare na wenzio.uongo?

chiku akajitawanya pale kitini sehemu yake ya kiuoni kushuka chini...alhamdullilah mtoto alikuwa amekaa kweli kweli...kile kiti chote kakifunika na kumwagika.usiniulize ya mchina au mwafrika.mi sijui. ndo akaanza kuzungumza. "unamjua yule kaka anayenitaka muda mrefu huwa anapenda kunitania?" wenzake watatingisha kichwa kuonesha wanamjua. dada akaendelea. "yule kaka kanifata leo analalamika mpaka analia, nikamwuliza hayo malalamiko yako ya nini? maaana alianza tu kusema "we mwanamke muuaji wewe, huna huruma kabisa..unanitaka nini lakini ?nakupa nusu ya mshahara wangu mimi na mke wangu na watoto watatu tunahangaika.nakupa hizo pesa leo mwezi wa 5 nilichoambulia kwako ni kiss tu na maneno matamu matamu kuwa nisubiri mambo mazuri hayataki haraka.mwaka huu sasa unanipa moyo tu ila boss unampa issue yako kirahisi tu"

mwenzenu nikashtuka.boss gani tena. ndo kumuuliza akanambia "boss alikuita ofisini muda flan umekaa kama saa moja umetoka. umerudi nikawa nimeenda kuna jambo nijadiliane naye. nmefika tu akawa anasema " huyu mwanamke anapenda sana kuvaa chupi nyeusi utadhani ana msiba huko chini" nikajiuliza anajuaje kuwa umevaa chupi nyeusi. nikamwambia boss labda tu leo imetokea.akanambia... "hamna zaidi ya mara 7 mwezi huu kavaa chupi nyeusi" moyo ulishtuka kama mtu aliyefumaniwa na wakwe. nikajikongoja tu ndani kwa ndani nikauamsha moyo wangu maana maskini nlihisi kama umedondoka kwa ule mshtuka na kuangua kwenye maini au figo. nikajiuliza huyu boss umempa kwa mwezi mara 7 mimi mwaka sasa na nusu ya mshahara wangu nakupa,bado lunch nakutoa mimi kila siku kwa bill, hapo hujanambia pesa za voucher na saluni. unataka nikupe nini we mwanamke uridhike?"
ndo nikashangaa kiukweli leo nimevaa chupi nyeusi.lakini sikukaa vibaya kusema kuwa boss ameniona maana nimevaa na skin tight.

nilimkatalia jamaa na kuapa kwa dini zangu zooote.jamaa akawa bado haamini nikamwambia basi aende akaangalie kwa wale watu wa cctv maana ofisi zetu zote zina cctv. kweli akaamua kwenda.akarudi akasema kule hajaona kitu chochote ila akawa anajiuliza kuwa labda boss ni mchawi? basi tukawa tunabishana mara nikakumbuka kuwa kuna yule dada Siwema alikuwa anafanya kazi hapa kipindi kile tumeanza akaacha. nikampigia simu kuwa boss anaongea maneno haya ni nini. si ndo yule dada akafunguka? kuwa yule boss ana tabia ya kuchungulia wanawake wakiwa chooni na yeye aliacha kazi pale sababu hiyo baada ya boss kumwambia siku hiyo kuwa "Siwema una mashavu yamenona sana utadhani yamebandikwa" siwema alijibu tu aah boss si unajua chips tunazokula hizi tunanenepa kama nini" ndo boss akajikuta ametamka " aah mi sizungumzii hayo ya juu, nazungumzia mashavu mnato..mashavu ya chini.akaendelea... na chupi zako unavaa zinayabana..." yule dada anasema alipotupa macho yake kwenye kioo pembeni ya mlango wa boss akaona reflection ya kile kilichopo kwenye screen ya computer ya boss. kunaonekana chooni na mwenzao mmoja amechuchumaa anapunguza uzito. kumbe boss alijisahau na zipu yake ipo wazi. akakumbuka kuwa alipotoka tu chooni ndo boss alimwita.na hakuna la maana lolote mpaka muda ule alilomwambia....zaidi tu ya kumkodolea macho na kuanza kuropoka hayo maneno.

anasema boss alishtuka na kumsihi sana asiongee neno kwa watu akamwambia ampe mil 5 na amtafutie kazi kampuni nyingine ya clearing and forwarding pale aombe tu ku resign. siwema akajionea kuwa fahari ya macho haifilisi duka...so akachukua na kuomba aombewe kazi kwingine.

chiku akaendelea kusimulia "mwenzenu toka nimesikia habari hizo yaani hapa nawaza mara kadhaa nikienda chooni navyojiachia mwenyewe tena natoa nguo zote,kumbe yule mshenzi,mwanahizaya,mwanaharamu,baradhuli anakaa kule kutuangalia halafu anapiga punyeto...na ndo maana kuna kipindi anaweza kukuita ofisini kwake uende ukienda hana la maana unakuta tu mijicho yake imelegea kama amebwia unga. tunashikana naye mikono kumbe anatupakaza mananii yake tu" alimalizia chiku. huyu mwingine naye akapandisha mori...maana yeye hakujua kisa sasa nadhan aliposikia hivyo akawaza naye ameshaonwa sana na boss...wakawa wanazungumza kupanga mikakati. ...

nikaona hapa kuna fursa.si unajua wajasiliamali wanasema ukiona fursa changamkia....? nikainuka pale kwangu nikajisogeza kwenda kukaa meza yao utadhan ndo naingia muda huo. nikawasalimu tu kwa ukarimu" akina dada habari zenu"wawili wakajibu mmoja hakujibu alikuwa ameivuta kweli midomo yake. nikamwambia "dada samahani kama kukaa hapa ntakuwa nimekukwaza maana hata salamu yangu hujaitikia utadhani mimi ndo nimeuzia maandamano ya ukuta...." akacheka baada ya kujitahidi kujizuia na kusema :aargh kaka we acha tu kuna mitu hapa duniani mi******* kweli. yaani nawaza hapa sijui hilo limtu nikaling'ate ******** nanii yake na kuitafuna. nikaona salaaaalehh...ashakum si matusi huyu dada..... ndo nikamwambia " binadamu anayewaudhi warembo kama ninyi hastahili kuishi hata kidogo inapaswa apelekwe jehanam ya hapa hapa duniani. ndo wale wadada kunisimulia kisa na mkasa.
tukabadilishana namba za simu maana nikawa kama kaka yao na rafiki nikiwaambia nataka hiyo kesi yao wanikabidhi mimi.wakaniahidi kuwa watakachoenda kufanya huko watakuja kunisimulia.

nikaanza kuwaza . kukweli ukimwona huyo chiku? mashallah....mtoto ameumbika jamani asikwambie mtu...yaani nikaanza kuwaza nami ntaweza kukabidhi salary yangu kwake? anyway mambo mengine inabidi tu upige moyo konde. nikaukunyata moyo wangu maskini mie unaweza toa salary yako halafu usione ndani....ila naweza jaribu maana si ajabu inzi kufia kwenye kidonda. ni kama unapoenda kuvua.si ndiyo? kwani unajua kuwa ntamkuta samaki ananisubiri sehemu flan?si unaenda tu unatupa ndoano yenye chambo na kusubiri kuvua?kuna kipindi ukinyanyua unakuta chambo kaliwa ila samaki katokomea..unalaani unaweka chambo mwingine....

hebu nisubiri hii issue yao itakuaje nami nimejipa madaraka makubwa kweli eti ntawasaidia na sheri yote inawalinda....unajua ili nionekane kidume nlilipa bill yao pia jana? zilinitoka kama 45,000 hivi...hivi mabint wa siku hizi kwa nini mnagharama hivi? nliposema tu ntawalipia wakaanza na kuagiza take away....aaargh nilikuwa natabasamu usoni lakini moyoni najenga chuki kwao. maana miaka ile ya nyuma mabint walikuwa na aibu....siku hizi?????thubutuuuu.

anyway wanasema "mkono mtupu haulambwi" wadada hebu nendeni mkaangalie huko vyooni kwenu. hamna camera kweli? unaweza kuta kuna hidden camera libosi lako linakuchora tu halafu ukitoka nje una maringo wakati ukienda chooni......
 
  • Thanks
Reactions: THT
dah wadau miaka hii mmekuwa wavivu kichwani. mi nimeisoma hiyo hadith mara moja na nimeielewa kirahisi sana. mbona ipo rahisi kitu gan hamkielew? au ni hizo alama za kunukuu n.k? jamaa anadhan uelewa wake wa insha ni kama wetu.si wengine hatukusoma sana hata hatuzielew hizo alama lakini kiukweli story inaleweka sana sema tu hii si level ya wasomaji wengi. wengi wamezoea maandishi mepesi mepesi...
 
Tatizo unaongea sana mpaka hata kama ni kisa cha kweli kinabadilika kuwa hekaya za sindbad baharia
 
aisee.... nmeshindwa niseme nini. ngoja niwachie wawe na maoni yao huru kabisa. kusoma is one thing kuelewa is another. namfaham jamaa mmoja yeye anajua kusoma na kuandika lakini ukimwambia nieleze ulichosoma anakwambia sijaelewa hata moja labda wewe unielezee.... hosp wanasema ubongo wake una tatizo la ku connect ideas so ukiandika kitu complicated tu anachanganyikiwa kabisa. he cant take many at a go. so kuna watu ni kuwaelewa.
 
aisee.... nmeshindwa niseme nini. ngoja niwachie wawe na maoni yao huru kabisa. kusoma is one thing kuelewa is another. namfaham jamaa mmoja yeye anajua kusoma na kuandika lakini ukimwambia nieleze ulichosoma anakwambia sijaelewa hata moja labda wewe unielezee.... hosp wanasema ubongo wake una tatizo la ku connect ideas so ukiandika kitu complicated tu anachanganyikiwa kabisa. he cant take many at a go. so kuna watu ni kuwaelewa.
Usijali huko vizuri, Shigongo hakunyimi kazi, labda wewe mwenyewe usiridhike na mshahara wa majaribio.
 
kumbe ndo maana boss wangu anajuaga nipo period kumbe ni hizi kamera bna
asante mdau maana nilitukanwa sana huku mara ooh nanuka nikiwa period atakuwa anasikia harufu yaani miaka 30 na kitu niliyonayo nishindwe kujiswafi kipindi nipo period jamani
kumbe ananicheki kwenye camera ni rahisi kujua maana saa ingine nachukua pedi kwenye pochi naenda kuchange nikinyanyuka lazima nijiangalie nk
 
KESHA KAMATA UKUTA HUYU NDIO UMEANDIKAJE ? SKUIYO WAJAMAA WATAKUWA WANAMAADHIMISHO ALAF WAMESEMA WATAFNYA USAFI SIKU NZIMA
 
Mkuu hadithi nzuri sanaaaa tu.Wasio kuelewa wasome maoni Labda wataelewa.
 
Back
Top Bottom