Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Bosi mmoja aliyemfukuza mfanyakazi wake kazi alilazimika siku moja kulala macho yaan kukesha baada ya kuona kila siku akiamka asubuhi anakuta kinyesi mlangoni mwake, sasa siku moja akaona akae macho usiku wote huku akiwa amejificha ili aone nani anayemfanyia upuuzi huo mungu naye si Athuman bwana bosi baada ya kukaa macho na kujificha majira ya saa saba usiku akaona mtu anakuja kama kawaida anavua kaptura ili afanye yake yule bosi akamvizia hatimaye akamkamata kuja kumwangalia vizuri kumbe ni kijana aliyemfukuza kazi akamwuliza mbona unanifanyia hivyo kulikoni? Yule kijana akasema nilikuwa nakuonesha kuwa Ridhiki hutoi wewe hata kama umenifukuza kazi bado naendelea kupata chakula kama kawaida bosi alichoka na kumwacha kijana aende zake na kumwomba amsamehe asiendelee kuja kufanya mambo ya kuacha kinyesi tena pale.