Boris Johnson ajiunga na Biden, watwanga usingizi mkutanoni Glasgow

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,839
17,437
Boris Johnson ajiunga na Biden, watwanga usingizi katikati ya mkutano wa tabianchi, Glasgow

Nov 03, 2021 10:48 UTC

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiunga na Rais wa Marekani Joe Biden na kutwanga usingizi mfupi wakati wa vikao vya Mkutano wa Hali ya Hewa unaofanyika Glasgow huko Scotland.

Picha ilizosambaa mitandaoni ya mojawapo ya vikao vya jana, Jumanne huko Grasgow, inamuonyesha Johnson akiwa amezama kwenye uingizi bila ya kuwa na barakoa akiwa karibu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na mwanaharakati wa hali ya hewa wa Uingereza Sir David Attenborough, ambaye ana umri wa miaka 95.

Katika kikao cha Jumatatu iliyopita Rais Joe Biden wa Marekani pia alionekana kwenye picha za video na kamera zilizonasa matukio ya shughuli za vikao vya mkutano huo, akiwa amechapa usingizi, jambo ambalo limemfanya adhihakiwe katika mitandao na vyombo vya habari kote duniani.

[https://media]Joe Biden katika mkutano wa Glasgow

Nchini Uingereza waandishi wa habari na wanasiasa wamemkosoa Boris Johnson kutokana na jinsi anavyoonekana akiwa amelala kwenye kikao hicho wakisema kuwa picha hiyo haiendani na tukio la hali ya hewa duniani.

Mbunge David Lammy wa Uingereza ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba: "Ni wakati wa Boris Johnson kuamka, dunia inaungua. Sir David Attenborough anazingatia mgogoro wa hali ya hewa, hivyo ni wakati wa serikali yako pia kufanya hivyo."

Viongozi kutoka nchi zaidi ya 100 duniani wanahudhuria mkutano huo wa 26 wa kujadili mabadiliko ya tabianchi, ulioanza tarehe 31 Oktoba na kuendelea hadi tarehe 12 ya mwezi huu wa Novemba mjini Glasgow, Uskochi.
 
..
4by750c49f4c391ytkc_800C450.jpg
 
Hapo nadhani ilikuwa ni wakati mama yetu anatema madini,halafu mbona Buhari yeye hawamuoneshi
Maanake wanaona kabisa maushungi hana hoja na hapo ndipo wengine wanatoka kabisa nje kwenda kuvuta sigara.
Nyie kama ni wanaume basi nina uhakika wa 100% kuwa hamna malinda, wallahi tena!

Ukiwa makini ni rahisi tu kuwajua wasio na malinda.......wanakuwa na vitabia fulani vyepesi vya kijinga kijinga na utastaajabu wenyewe wanavyofurahia!!!
 
Mimi Sioni tatizo hao NI BINADAMU.
Kulala NI kitendo cha lazma sio hiari.
Yaani utake utalala usitake utalala.
Hapo ndipo mungu anajipa sifa katika Quran.
Sura ya 2:255.
(Asiyeshikwa na usingizi Wala kusinzia)
 
Mbona Jaffo alieahi kuchapa usingizi mbele ya Hayati JPM
Umesahau Tyson Akiwa Bungeni Aliutandika Mpaka
Magazeti Yalipohoji Walisema Hakulala, Anatafakari
Alipofunga Vifungo Vya Koti Hovyo Magazeti Yalipoandika Ukweli Tena Wakakataa

Mwenye Pictures Atatuwekea Kwa Rejea Za Watu
 
Nyie kama ni wanaume basi nina uhakika wa 100% kuwa hamna malinda, wallahi tena!

Ukiwa makini ni rahisi tu kuwajua wasio na malinda.......wanakuwa na vitabia fulani vyepesi vya kijinga kijinga na utastaajabu wenyewe wanavyofurahia!!!
Hivi vitabia hujavigundua kwa babu & baba yako
 
hapo waliposinzia ndiyo muda pekee mama enu mdogo anaweza kujisogeza na kupiga picha Biden yani japo hata selfie.
 
Mnamchukia Samia sababu ya dini yake tu kumbe, wakristo kwanin mna chuki Sana na kiongozi akiwa wa dini nyingine haswa muislam???

Eti maushungi!
Sio kweli, hakuna rais ambaye hakuwahi kupachikwa jina. Ni mambo ya kawaida hata Trump alipachikwa Mr. Trumpet 🎺.
 
Mimi Sioni tatizo hao NI BINADAMU.
Kulala NI kitendo cha lazma sio hiari.
Yaani utake utalala usitake utalala.
Hapo ndipo mungu anajipa sifa katika Quran.
Sura ya 2:255.
(Asiyeshikwa na usingizi Wala kusinzia)
Kupiga miayo na kusinzia Wakati wa mkutano au darasa huonesha ama darasa/mkutano una bore au msikilizaji hana interest na kinachozungumzwa. infact anapotezewa muda.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom