Bora Uongozi na Uongozi Bora: Kesi ya Tanzania na Cyprus | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bora Uongozi na Uongozi Bora: Kesi ya Tanzania na Cyprus

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by zimmerman, Jul 12, 2011.

 1. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Katika kile kinachodhihirisha utofauti wa fikra kati ya viongozi bora na bora viongozi, hapa tunapata mfano husika unaoonyesha hilo. Juzi ilikuwa siku ya kusikitisha kwa taifa la Cyprus ambalo ni kisiwa kilichopo katika bahari ya Kati (Mediterranean Sea) ambako milipuko ya mabomu ilitokea kwenye kituo cha jeshi la nchi hiyo, milipuko iliyoua takribani watu 12 wakiwemo raia na askari.

  Japo mazingira ya matukio haya ya milipuko ya mabomu pale Cyprus yanafanana kabisa na yale yaliyotokea hapa Tanzania pale Dar es Salaam; mfano:
  - chanzo sahihi cha milipuko hakijajulikana kisayansi
  - milipuko ilisababisha vifo vya raia na askari

  Hata hivyo kuna utofauti wa kimsingi unaoonyesha jinsi hili suala lilivyopokelewa na kushughulikiwa kiuongozi na viongozi wanaohusika; kimsingi:
  - ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Cyprus tukio hili la kusikitisha linatokea wakati kwa Tanzania yametokea matukio kama haya mawili, kwa nyakati mbili tofauti zinazopishana kwa miaka miwili, la kwanza mwaka 2009 (Mbagala), la pili mwaka 2011 (Gongo la Mboto)

  - Viongozi wa juu wa kijeshi kadhaa wa Cyprus wakiwemo Mkuu wa Majeshi na Waziri wa Ulinzi wamewajibika kwa kujiuzulu kw hiari mara moja; hapa Tanzania hakuna kiongozi yeyote yule wa ulinzi, awe wa chini, kati, au juu aliyejiuzulu. Tukio la karibu na kujiuzulu liliwahi kuzungumziwa na waziri wa Ulinzi, Dr. Hussein Mwinyi, pale alipoonyesha kusikitishwa na vifo vya raia katika tukio la kwanza pale Mbagala alipogusia kwamba tukio kama hilo halitatokea tena chini yake – na kama lingetokea tena atajiuzulu mara moja. Ukweli ni kwamba tukio kama lile lilitokea tena miaka miwili baadae na, pamoja na kukumbushiwa usemi wake na watu tofauti waliokuwa na kumbukumbu, aligoma katakata kujiuzulu.

  Maoni yangu: Nadhani hapa tunaona mfano husika wa dhana ya uongozi wa uwajibikaji ukijionyesha katika matukio ya aina ile ile lakini kwa namna tofauti kabisa ya utekelezaji miongoni mwa viongozi wa Cyprus na viongozi sambamba wa Tanzania. Swali la kujadili: Je Tanzania tuna viongozi wa serikali wanaowajibika kwa wananchi wake?
   
 2. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Jibu la swali ni kwamba hatuna viongozi wanoamini kwamba wanawajibika kwa wananchi hawa tulionao wanawajbika kwa JK full stop.
   
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kaka unafananisha chungwa na jiwe unatuuliza ni kipi kitamu?
  hatuna viongozi haspa tz.
  tuna wafuasi wa ...........
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa sijaona mada hii, nimeandika nyingine kama hii nadhani mod ataunganisha.
  Serikali ya Tanzania inajiaibisha kutokana na kauli ya Waziri Mkuu Pinda bungeni kwamba serikali iko makini sana. Kwa nji zenye kufuata uongozi bora na siasa safi kosa la kurudia kosa ni kusafisha safu yote ya uongozi. Lakini kikwete alipotokea Gongolamboto huku akiwa anatabasamu na kuchekacheka ni ushahidi wa udhaifu na ulegelege wa serikali tulilyo nayo.
   
Loading...