Bora tuiite "Vita ya Bara la Ulaya" na sio vita ya Dunia

mfungwa

JF-Expert Member
May 23, 2015
1,291
341
Huu ni ulimbukeni wa hali ya juu. Kusambaza slogan ambayo hakika sio kweli. Mara nyingi najiuliza kwanini vita ile tuiite vita ya Dunia wakati direct ilikuwa inawausu wazungu. Na wao katika kuja kuingilia na kunyonya bara mfano la Africa na kikubwa kugombania sehemu mbali mbali hasa Africa.

Kutokuelewana kwao katika kugawana kukasababisha vita ya kwanza na ya pili. Halafu jina walilotafuta ni vita vya dunia. Huu ni ujinga wa hali ya juu. Wao wasikwepe kwamba walikuwa sababu hiyo na ilianzia kwao. Baadae ndio ikasambaa. Siingii suala la nchi nyingine (za kisocialist). Lakini sababu kubwa na wao wasikatae jina lao waite tu wazi "vita vya ulaya".
 
Kuiita vita ya ulaya sawa na kuiita vita ya dunia sababu hao watu wa ulaya walikuwa wamegawana sehemu kubwa ya ulimwengu na kuzifanya kama nchi zao!ingekiwa wamepigana tu wao halafu sisi huku tumelala sawa,ila kama tulienda kupigana kuwasaidia wao basi vita ilituhusu ila tulikuwa hatuna maslahi nayo
 
Iliitwa vita ya dunis kwasababu nyingi
1. Idadi ya watu waliohusika, askar na wasio askari ilikua ni kubwa kuliko vita yoyote kabla
2. Teknolojia ilotumika ilikuwa bora zaid kuliko kabla
3. Maeneo, ilipiganwa maeneo mengi zaid, karibu kila bara (hata Tanganyika pia)
4. Madhara yalikua makubwa haikupata kutokea kabla
 
Iliitwa vita ya dunis kwasababu nyingi
1. Idadi ya watu waliohusika, askar na wasio askari ilikua ni kubwa kuliko vita yoyote kabla
2. Teknolojia ilotumika ilikuwa bora zaid kuliko kabla
3. Maeneo, ilipiganwa maeneo mengi zaid, karibu kila bara (hata Tanganyika pia)
4. Madhara yalikua makubwa haikupata kutokea kabla
Kwakuongezea tu, ilipiganwa dunia yote. Asia, Afrika, Ulaya, Amerika zote na visiwani. Mfano, ile ya kwanza hitimisho lake lilikuwa Tanganyika, ya pili Japan. Ni tukio lililolikumbwa dunia yote.
 
Back
Top Bottom