Bora TANESCO Muache kutangaza makato ya umeme, maana ni kila siku

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Lazma mjielewe TANESCO Mtangaze msitangaze lazma mkate umeme, kitu kinachopaswa kutangazwa ni kile kinachotokea kwa nadra sana, Sasa nyie kila siku mnakata umeme, acheni kututangazia fanyeni kazi zenu ukiwepo sawa hata usipokuwepo sawa.

Mnatumia mamilioni kila siku kutangaza makatizo ya umeme kwa ajili ya Nini Sasa. Wakati mnajua kila siku ni tabia yenu kukata umeme.

Shirika gani kila siku hitilaf, juzi imetokea hitilaf Kenya Hadi huku nikasikia matangazo, Sasa nyie ni kila siku. Au fungueni kituo Cha tanesco Cha kutangaza makatizo ya umeme.

Shirika limejaa mgao, hitilaf, mitambo mibovu, huduma mbovu, Rushwa, nyie kwenu zuri ni lipi, achaneni na sisi hatutaki hayo matangazo yenu nyie kateni Mana ndo tabia yenu.

Hawa samaki naenda kuwamwaga hapo ofisi ya emergency halaf mtu aniguse
 
Mimi mtaani ninao kaa leo umeme upo ila mdogo sana, sasa kama upo mzigoni halafu friji lipo ON,ukirudi lazima ulie yaani bora mngekata kabisa tujue moja.
 
TANESCO inaongozwa na watu wenye kiwango kidogo cha kufikiri au wanafanya makusudi ili wapige pesa
 
Back
Top Bottom