Bora nichukiwe na Wana Simba SC ila ukweli huu Mchungu uliochangia Kipigo Kitakatifu cha Mzulu na Mkaburu Kaizer Chiefs FC niuseme

Ndo maana daily mnaitwa takataka. Mbna hayo hukuyasema wakati simba anashinda? Alafu kufungwa sio jambo geni na ukizingatia bado tuna mechi ya nyumbani. Hata Simba ikitolewa hakutaifanya yanga ibebe ubingwa zaidi mtaendelea na majungu mnyama anasonga.
You're very Foolish.
 
Kwa mtizamo wangu naona benchi la ufundi la Kaizer lililizidi mbinu kwa mbali sana benchi la ufundi la Simba kama ifuatavyo:-

1. Simba waliidharau sana Kaizer baada ya kuaminishwa na takwimu za waandishi hapa bongo kuwa Kaizer ipo nafasi za chini sana kwenye ligi yao, Kaizer wamefunga magoli machache na kufungwa mengi kwenye CL hivyo basi wanafungika kirahisi na hawafungi sana, wamepita tu kwa bahati kwenye kundi lao licha ya kulingana na Horoya na pia wachezaji wao tegemeo Biliati na kipa tegemeo Itumilenge ni majeruhi. Matokeo yake viongozi wa Simba na benchi la ufundi wakiongozwa na Gomez wakaingiza hizo propaganda kichwani mwao wakaanza kucheza vipasi vyao vifupi wakafunguka jamaa wakastukiza wakawapiga kimoja lakini Simba hawakushtuka wakaendelea kuona tu wanawamudu Kaizer na watasawazisha akili kuja kuwakaa sawa sawa tayari half time ubao unasoma 2 - 0
2. Kaizer ni wazuri lakini hawakutii ubora wa Al Haly. Vipi Al Haly kafunga moja lakini Kaizer kafunga nne? Je tatizo nini? Tatizo lilianzia kwenye benchi la ufundi kujiamini badala ya kucheza kama walivyocheza Misri na Kongo kwao wakafikiri wanacheza na Dodoma Jiji. Laiti kama Simba wangejilinda na kushambulia kwa kushtukiza na kumuacha Mugalu mbele peke yake na wote kurudi nyuma kama walivyofanya Kongo na Misri nina uhakika mechi ingeisha kwa kupoteza kwa goli moja na si zaidi. Hivi benchi la ufundi lilifikiria nini kuanza na viungo Bwalya na Mkude kwenye mechi ya kugongana kiasi kile wakati kwenye benchi una Muzamiru na Nyoni? Siku zote Bwalya na Mkude ni wapiga pasi wazuri sana lakini ikifika kwenye kugongana kama anavyofanya Lwanga hutawaona kabisa. Kwa hiyo inaonyesha kabisa Simba walijiandaa zaidi kwenda mbele kutafuta magoli badala ya kujiandaa kujilinda kwanza.
3. Urefu na maumbo ya wachezaji wa Kaizer ilikuwa tatizo kwa wachezaji wengi wa Simba. Hili ni funzo kwa benchi la ufundi la Simba siku zijazo kuwa wakati wa usajili pamoja na uwezo binafsi wa wachezaji lakini wakati mwingine unatakiwa uwe na wachezaji wawili watatu wababe warefu wenye miili kama Lwanga kwa ajili ya mechi kama ya jana na hapa kwenye ligi yetu wanapokutana na timu kama Prison. Kuna mchezaji beki wa pembeni kushoto mrefu alikuwa Namungo na sasa yupo Ruvu kama sikosei anaitwa Charles Manyama wakimsajili naamini Simba haitajuta. Kwani kwa mijitu kama ya Kaizer au Prison atawafaa sana. Na tatizo lingine ligi yetu inazibana sana timu zetu kuwa na wachezaji 10 tu wa kigeni hivyo basi Simba inatakiwa ifanye kazi kweli kweli kupata wachezaji bora wa ndani na hao wachache 10 wa kigeni ambao ni bora kabisa. Ni wakati sasa kwa benchi la ufundi laSimba lianze kuwafundisha wachezaji mpira kucheza mpira wa nguvu pale inapobidi bna sio kutegemea aina moja tu ya mpira laini laini. Na ili ucheze mpira wa nguvu ni lazima uwe na mijitu hasa iliyokamilika kama wachezaji wa Kaizer.
4. Kwenye mechi ya jana nalipongeza sana benchi la Kaizer kwa sababu waliwapa Simba kitanzi wakajinyonga wenyewe. Kaizer sio kama hawajui kucheza pasi fupi fupi wanajua sana na ndio mchezo wao. Wao waliwaacha Simba wacheze vipasi vyao vifupi (eti biriani) wao Kaizer wakawa wanawasubiri halafu wanapiga mipira mirefu (counter attack). Kiufupi Kaizer waliamua kucheza "direct football". Kwa mtu ambaye hazifahamu Simba na Kaizer angefikiri kuwa Kaizer ndio ipo ugenini na Simba ndio mwenyeji. Lakini ni lini benchi la ufundi litastuka na kumtumia mtu kama Ndemla (anaozea benchi) kwenye mechi kama hizi ambazo Simba inaishia katikati na kushindwa kuvusha mpira mbele? Ukiacha Chuji ambaye ameshastaafu nadhani kwa Tanzania amebaki Ndemla tu peke yake anayeweza kupiga pasi mita zaidi ya 30 kwa usahihi. Kama yupo mwingine naomba kujulishwa.
5. Mabeki wote wa pembeni na wakati walikosa utulivu. Hili siwezi kulisemea sana kwa sababu sijajua lilisababishwa na nini. Kapombe, Husein, Wawa na Onyango walifanya makosa sana walikosa kabisa utulivu ambao walikuwa nao katika mechi zilizopita za CL. Walikumbwa na kitu gani wote kwa pamoja tena katika mechi moja wao ndio wanajua kwani sio kawaida.
6. Viungo wakati na pembeni walikuwa wanachelewesha sana kupeleka mipira mbele kwa haraka. Badala yake walikuwa wanapiga pasi nyingi sana zisizo na malengo wala faida kwa timu. Pale ambapo wanapoamua kupeleka mpira mbele unakuta tayari Kaizer wameshajipanga watu zaidi ya saba kwenye eneo lao la kujilinda wanawasubiri Simba. Na hili ni tatizo sana kwa Simba hata kwenye ligi ya hapa nyumbani. Simba wapo taratibu sana kutoka katikati ya uwanja kwenda eneo la adui na hii huwa inampa adui muda mwingi sana wa kujipanga jinsi ya kuwazuia Simba sema tu kwenye ligi yetu hapa timu zinazoweza kutumuia hayo mapungufu ni chache sana.
7. Benchi la ufundi liwakumbushe mafowadi na viungo washambuliaji wa Simba kuwa sio mara zote lazima wapige pasi mpaka wamkute kipa. Shuti la maana nililoliana ni la Miquisone lililopaa na la Boko ambalo kipa alidaka. Katika akili ya kawaida kabisa Simba wamefika kwenye kumi na nane jamaa wamejaaa wakawa wanajaribu kupiga "one two" mara ya kwanza, pili, tatu, nne jamaa wanaokoa hivi bado tu benchi la ufundi lipo tu wamekaa badala ya kuwakumbusha wajaribu kupiga walau unaweza kukuta kipa yupo "off timing" au hata ikatokea mpira ukamgonga beki ukaenda wavuni.

Mwisho nawapongeza Simba kwa kufika hatua hii. Kwa kweli wanahitaji pongezi sana. Tusiwabeze kwa kilichotokea bali tuwape moyo na ushauri mzuri utakaowasaidia mbeleni. Kwani walianza kupigwa tano tano Misri na Kongo lakini mwaka huu tumeona As Vita kapigwa nje ndani na Al Haly kafa hapa taifa. Nina imani mwakani wakijipanga wakajiimarisha zaidi na kufanya usajili mzuri watafika zaidi ya robo fainali. Mungu ibariki Simba Mungu ibariki Tanzania

Mpira biriani,Manara anasema wanacheza kama Barcelona,thubutu? Labda Barcelona ya ushetu
 
Teh, baada ya kipigo sasa ndo mmekubali kuwa mnabebwa na mnadekezwa na tff
 
Back
Top Bottom