Bora nichukiwe na Wana Simba SC ila ukweli huu Mchungu uliochangia Kipigo Kitakatifu cha Mzulu na Mkaburu Kaizer Chiefs FC niuseme

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Kama Mwamamichezo Halisi ( japo sijifichi ni mwana Simba SC ) nianze kwa Kuwapongeza Kaizer Chiefs FC kwa Ushindi wa Goli Nne na niwape pia Pole Simba SC kwa Kufungwa Mchezo huu wa Kwanza leo.

Zifuatazo ni sababu zangu Binafsi za Kiuchambuzi Mimi Krav Maga kwanini Simba SC tumefungwa na Kaizer Chiefs FC ambazo hata hivyo sikulazimishi uziamini japo unatakiwa uziheshimu kama ambavyo nami naheshimu ( nitaheshimu ) zako.

1. KUBWETEKA KWA WACHEZAJI

Huitaji Akili Kubwa ama kuona au kugundua kuwa Mafanikio ya hivi karibuni ya Simba SC yamewapa Kiburi cha Kipuuzi Wachezaji wa Simba SC kiasi cha kuanza Kubweteka wakijiona ni akina FC Barcelona.

2. MIPIRA YA KROSI NI TATIZO SUGU KWA MABEKI WA SIMBA SC

Nilidhani baada ya mwaka Juzi Kufungwa Goli Tano Tano na AS Vita na Al Ahly kwa Mipira ya Krosi Simba SC ingejifunza na Kulifanyia Kazi Ila leo Makosa haya haya ya Kutokujua Kukaba Krosi yamesababisha Beki Shomari Kapombe asababishe Kufungwa Goli 3 huku Beki Mohammed Hussein Zimbwe nae akisababisha Goli 1 ( tena la Nne ) kwa Kumzawadia Pasi ya Upendo Adui na akafumua bonge la Shuti ( Muwa )

3. UZEE KWA MABEKI WA KATI WA SIMBA SC NA KUCHOKA KWAO UPESI

Ifike mahala sasa Simba SC ijifunze ama kutokupenda Kusajili au Kung'ang'ania Wachezaji Wakongwe ( Wazee ) huku wale Vijana na wenye Uwezo kama Beki Kijana ninayemkubali sana Ame Ibrahim na David Kameta Duchu tukiacha Kuwatumia. Leo akina Wawa na Onyango wamefanya Makosa makubwa mno na laiti yangetumiwa vyema na Washambuliaji wa Kaizer Chiefs FC huenda leo tungefungwa hata Magoli 7 au 8 pale Bondeni kwa Madiba.

4. KOCHA WA SIMBA SC KUKARIRI KIKOSI NA KUKOSA PLAN B YA HARAKA

Nikiri tu kuwa Kocha Mkuu wa Simba SC Didier Gomez kweli ni Tactician ila nae sasa ajifunze Kucheza Mechi zake Kimkakati na Kimazingira zaidi kuliko Kujiamini sana na kuingia Kichwa Kichwa tu.

5. VYOMBO VYA HABARI KUPENDA KUIPA SIFA SIMBA SC ZISIZOSTAHILI

Nilitegemea kuona Vyombo vingi vya Habari nchini Tanzania ( hasa vya Michezo ) vingekuwa vinaiambia Ukweli Simba SC kuhusu Klabu ya Kaizer Chiefs Matokeo yake Kutwa tu Magazeti na Watangazaji wa Vipindi vya Michezo Kazi yao ni Kuisifia tu Kinafiki Simba SC kwa kutokujua kuwa Wanawaharibu Wachezaji kupelekea kutokuwa na Ufanisi.

6. UBOVU WA LIGI YA TANZANIA. KUDEKEZWA SANA NA TFF HUKU MWILI KUTOKUWA TAYARI KIMCHEZO

Binafsi niliwashangaa mno Wapenzi na Mashabiki wa Simba SC walipokuwa wakiibeza Klabu ya Kaizer Chiefs kwakuwa iko nafasi ya Kenda ( Tisa ) katika Ligi Kuu yao.

Watu wa Simba SC walisahau kuwa Kaizer Chiefs FC wapo katika Moja ya Ligi Kuu bora barani Afrika ambayo ni Professional League wakati yetu hapa ya VPL ni Semi - Amateur kwa sasa.

Pia sasa imefika wakati TFF kuambiwa ukweli juu ya kupenda Kuidekeza Simba SC na Kuisikiliza kwa kila walitakalo wakati kumbe hapo wanakuwa hawaijengi Klabu bali wanazidi tu Kuibomoa.

Sikuona sababu ya Simba SC kukaa karibia Siku 9 au 11 kutokucheza Mechi yoyote ile ya Kimashindano ( hasa Ligi Kuu ) kwa Kisingizio kuwa wana Mechi za Champions League na hawataki Wachezaji wao ( wetu ) Kuumizwa.

Cha Kushangaza Kaizer Chiefs FC ndani ya Siku hizo hizo ambazo Simba SC ilidekezwa na TFF kwa Kusikilizwa na kutokucheza Mechi yoyote ile ya Ligi Kuu ya VPL wao Kaizer Chiefs wameweza Kucheza Mechi zao Mbili za Ligi Kuu yao Kubwa ya PSL.

Kwangu Mimi Krav Maga naamini mojawapo ya sababu Kubwa ya Simba SC yangu kupokea Kipigo Kitakatifu ni Wachezaji kutokuwa na Match Fitness tofauti na Wenzao ( Kaizer Chiefs FC ) ambao kuendelea Kwao kucheza Mechi zao za Ligi Kuu zimewasaidia Kuwaimarisha Kimwili, Kiufundi na Kimchezo.

Simba SC wangeacha Kudekadeka na TFF nayo kukubali Kuidekeza ingecheza Michezo yake Miwili ya Ligi Kuu VPL dhidi ya Watani zao Yanga SC na Coastal Union FC ingekuwa Faida Kwao ya kukijua Kikosi na kukifanyia marekebisho ili isifungwe Kifedheha na Kaizer Chiefs FC kama ilivyotokea leo ( jana ) pale Soccer City ( FNB Stadium )

7. SIMBA SC HAINA KIKOSI CHA MICHUANO YA NUSU FAINALI YA CL BALI INA CHA KUCHEZA VPL, ASFC NA CHA KUISHIA TU ROBO FAINALI YA CL

Ili ujue ( mjue ) kuwa Simba SC ina Wachezaji tu wa Kuifikisha hapo Robo Fainali CL na siyo Nusu Fainali CL angalieni jinsi Wachezaji mahiri wa Simba SC ambao Kutwa huwa tunawaimba walivyokuwa outshined kwa kila Kitu na Wachezaji wa Kaizer Chiefs FC ambao wanaonyesha kuwa wameandaliwa vyema na katika Misingi hasa ya Soka.

Sasa ni wakati wa Simba SC kupitia Mwekezaji wake Mo Dewji kufikiria Kusajili Wachezaji wa Viwango vikubwa vya Kucheza hatua ya Nusu Fainali ya CL na siyo hawa tulionao ambao uwezo wao ni wa kutufikisha tu kila mara katika hatua za Robo Fainali CL.

Kuna Wachezaji wa Kigeni mahiri mno Walisajiliwa kwa Mbwembwe zote na Simba SC kuja Kuongeza Nguvu kama akina Junior Lukosa na Peter Maduhwa ila sijajua wamepotelea wapi, wameitia Hasara Kiasi gani Simba SC yetu na kwanini Kutoweka Kwao wana Simba SC hatukuambiwa pia.

Hata hivyo nihitimishe tu kwa kusema kuwa japokuwa Simba SC leo ( jana ) imefungwa Goli Nne kwa Bila ila ikijipanga vyema na kuwa na Mikakati ya Ushindi ya ndani na nje ya Uwanja Krav Maga nina uhakika Jumamosi ijayo Kaizer Chiefs FC anafungwa hata Goli Sita kwa Sifuri Uwanja wa Machinjio wa Benjamin Mkapa Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Kutokana na Hali ya Hewa ya Baridi Kali la Afrika Kusini nawashauri Simba SC hii Mechi yao ya marudiano ichezwe Saa 9 Alasiri ili iwe Changamoto Kwao Kimchezo na Faida Kwetu.

Kikubwa tu tuvumilieni Kuchekwa na Watani zetu wakubwa Yanga SC kwani ndiyo mpira na Utani huo ila nasi sasa tujitahidi kuyafanyia Kazi mapungufu yetu yote ya Kimchezo kusudi Mchezo wa marejeano Simba SC tupindue Matokeo kwa Ushindi kisha nasi tuendelee Kuwaacha Kimafanikio huku wakiendelea tu kupoteza Alama ( points ) kama kwa Namungo FC leo ( jana ) na watukabidhi mapema Ubingwa wetu wa Nne mfululizo wa VPL.

Tumefungwa, lakini tusikate tamaa pia.
 
Mimi maoni yangu ni haya

simba uzoefu unawaponza.. enyimba, mazembe, mamelodi na wengine waliowai kutwaa ubingwa wa caf wanaijua formula... mashindano ya caf ni mpira zengwe.. sio mapasi pasi na matobo na kanzu ili mashabiki washangilie jukwaani... kaizer chiefs kacheza direct football kama simba alivyocheza away game ya kwanza na as vita.. simba kinachowasumbua ni ego .. wanajiona wanajua mpira kiasi cha kwenda ugenini kupiga piga mapasi ovyo... tazama game ya simba na vita pale congo mwaka huu . Utajua simba alikosea wapi... mwishoni locha alichezesha wote bocco, mugalu, kagere wote washambuliaji ila hawajapiga shut on target hata moja... enyimba walitwaa ubingwa wa africa kwa sababu walijijua wao ni wapya.. lazima tuheshimu wapinzani.. passi za kipuuuuzi hatutaki.

Simba lazima wakubali ukweli zimbwe, kapombe , sio wachezaji wa kuanza katika timu yenye malengo ya ubingwa.. tazama game zote za robo fainali.. uone miili na umakini wa mabeki
 
Mimi maoni yangu ni haya

simba uzoefu unawaponza.. enyimba, mazembe, mamelodi na wengine waliowai kutwaa ubingwa wa caf wanaijua formula... mashindano ya caf ni mpira zengwe.. sio mapasi pasi na matobo na kanzu ili mashabiki washangilie jukwaani... kaizer chiefs kacheza direct football kama simba alivyocheza away game ya kwanza na as vita...
Nakubaliana nawe 100% Ndugu yangu.
 
Hii mechi itachezwa kuanzia saa 11 jioni hii ni CAF siyo tff rafiki ujue wakisema hakuna taa wataambiwa saa 10jioni ni si saa 8 kumbuka hata Al ahaly walitaka hivyo CAF wakakataa

Simba hata ajipange vipi kaizer chiefs inawafunga ndani nje.

Hata Kwa mkapa watapokea kichapo Tu simba
Tatizo Simba ulozi saa , nadhani unakumbuka kaduguda alivyologa as vital Kwa maelezo yake kabisa kutoka usiku wa manane kwenda uwanja wa as vital kuloga akafanikiwa


Kwa mpira wa Simba hauwezi kirekebishwa siku moja au ndani ya miezi 6 hasha .

Simba Hana wachezaji wanaofiti kwenye zaidi ya mfumo mmoja . Simba wanasoft ball na siyo tough ball .


Simba timu yeyote ikicheza tough ball lzm Simba walale tu

Ushauri wagu

Acheni uchawi .
Sajirini wachezaji wanaofiti mifumo hata 3
Acheni figisu na timu zingine za vpl.
Acheni kuitumia tff ili mbebwe
 
Uchawi unajidanganya ...hiyo ndio Raha ya soka ya afrika ...ni kama alkasusu tu kwanza ni uwezo
 
Mipira ya cross ilikuwa shida sana jana unadhani hawa jamaa kila wakipiga cross unaona kama wanafunga ni kweli wanatakiwa kitu cha kwanza kuzuia zile cross lakini pia beki zetu za katikati hawakuweza kabisa kuwazuia jamaa mipira ya vichwa. Mimi naona tatizo kubwa la team zote wakipata mafanikio kidogo umakini unapotea wanaanza kujiona na mpaka media zetu.

Nakumbuka mashindano yanaanza target yetu tufike robo final baada ya kumaliza juu ya Alhly tu zikaanza tambwe sasa tunataka kombe ok sio mbaya lakini unatakiwa ku manage expectations hii inatoa pressure kwa wachezaji tukaanza kufurahia kupangwa na Kaizer kama tunaenda kucheza na JKT tumeshajipitisha nusu final hata hatujawahi kucheza nao badala ya kuwapa heshima zao na ku focus na game tukabweteka.

Wakati mwingine tunatakiwa kujifunza kwa wenzetu angalia mfano City kila mtu alikuwa anajuwa ni muda tu watachukuwa ubingwa lakini huwezi kusikia kocha au mchezaji anasema tayari unasikia ni kweli tuko nafasi nzuri lakini ni lazima tu focus na kushinda game yetu ya kesho tunacheza na team nzuri lazima tupigane.

kwetu huku Simba alipkuwa nafasi ya pili ndio ana mechi mkononi lakini unasikia tunakuja wenyewe sisi ni mabingwa watarajiwa ni bahati tu league yetu sio kihivyo lakini profesional huwezi kuongea namna hiyo waache washabiki story hizo sio team officials. Turudi kwa Kaizer tukaanza kauli zetu za league yetu hawana kitu badala ya kuwapa heshima matokeo tumeyaona.
 
Back
Top Bottom