Bora mkae kimya, Kelele zenu mtasababisha ndege zote wapewe JWTZ

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Nahisi mnakumbuka kilichotokea Baada ya Watu kupigia kelele MV Dar es salaam. Sasa hivi hakuna anayeiongelea tena. Baada ya JWTZ kupewa, Sasa hakuna hata anayejua wala kuweza kuhoji kama meli hiyo inaweza kuwaka.

Sasa hizi choko choko zenu mlizoanzisha Na mange kimambi. Mtasababisha jamaa awape hizi ndege JWTZ na mnajua kabisa Kiongelea mali za hawa jamaa kwa Tanzania ni uchochezi. Ni kosa la jinai kuzungumzia kifaru cha jeshi.

Ni ombi langu, mkae tu kimya. Ingawa ni mabovu kweli na wengine tunaogopa kuzipanda. Ila yamesaidia fast jet kupunguza bei maana walibakiza kidogo kuwa monopoly.

Kumbukeni kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Nasikia ugonjwa uliompata Baba mwenye Nyumba Mzee Kipara umesababishwa na majengo(magofu) ya ofisi za Serikali yaliyopo Dar kukosa wateja hata wa kuyaulizia bei. Alitegemea hiyo fedha ajengee Dodoma
Anaugonjwa tena!!!!
 
Awakabidhi tu jeshi ili tusijadili tena
Kazidi upigaji akijidai anabana matumizi
 
Kweli mtanzania ni shida, sijui afanyiwe nini alidhike kila kiongozi kwao ni mmbaya, ukimweka mgongoni atasema tuu, dawa yao Mjomba.
 
Mleta Mada Ni Wa Kupuuzwa Tu Kwani Huko Jeshini Unadhani Hayazungumziki ? Ama Wewe Mgeni Hapa Tanzania

Hujawahi Kusikia Habari Ya Meremeta Hata Hiyo Iliyonunuliwa Billion 8 Japo Ni Kuukuu Yaani Used Ya 1979 Mwaka Wa Matengenezo

Bahkresa Kaleta Vyombo Vipya Kwa Billions 4
Sasa Ukweli Unasema Popote Siyo Majungu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom