Bora mfumo wa chama kimoja, haya ni mateso kwa Afrika

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Nikiangalia kinachotokea uganda.Nakiri demokrasia ni silaha ya wazungu waliyoileta ili waafrica tuangamizane wenyewe kwa wenyewe.

Uganda matokeo yanatangazwa bila kuainisha yanatoka mkoa upi na jimbo lipi.
Mwenyekiti hujiamulia tu na kuongeza idadi kwa jinsi anavyojisikia,lakini cha kushangaza waangalizi wanauita uchaguzi wa Haki na Amani.

Ni bora Africa tungebaki kubanana na mfumo wa chama kimoja kuliko adha waipatayo waafrica chini ya kivuli cha demokrasia ya mateso.
 
Mpaka sasa wamesemaje........?......maana sitaki presha......naomba nieleze taratibu......
Kiza kashikiliwa na jeshi,Mbabazi naye kakamatwa.Mwenyekiti anaendelea kutangaza bila kuainisha matokeo anapoyapata."mfano"Jimbo A kadhaa B kadhaa yeye anaropoka tu na namba zake kichwani,Wapinzania wanashikiliwa huku waangalizi wanasema uchaguzi umeenda vizuri.Ni aibu kwa waafrica,Sijuwi nani katuroga
 
Africa ni bara jeusi kila kitu cheusi tuvumilie tu hakuna kitu kinacho kuwa Africa Allah atujaalie Africa asitutie motoni kwani kila kitu cha Africa ni moto ujanja wa Africa ni kuwa na jeshi tu
 
Kiza kashikiliwa na jeshi,Mbabazi naye kakamatwa.Mwenyekiti anaendelea kutangaza bila kuainisha matokeo anapoyapata."mfano"Jimbo A kadhaa B kadhaa yeye anaropoka tu na namba zake kichwani,Wapinzania wanashikiliwa huku waangalizi wanasema uchaguzi umeenda vizuri.Ni aibu kwa waafrica,Sijuwi nani katuroga

Oooh.......kwa hiyo M7 ni rais tena......?......
Hebu nipe namba ya Trampu........kuna matusi kayasahau......
 
Yani ni kituko, Kiiza yuko mikononi mwa polisi Mbabazi nyumba imezungukwa na usalama...yani haifai hata kusimlia.
Na huyo Museveni eti awe mtu wa kati katika mazungumzo ya warundi...upuuzi kabisa!

Wayiii......sasa ndio nini.......
 
Mseveni hakuna cha kumtenganisha na urais labda kifo wangalizi hawa wakimataifa nao ni wale vyama vyao vya siasa ni vya kukandamiza demokrasia kilichobaki ni yeye kutaka kujitoa icc tu akae kwa amani duniani ndio maana mkurunzinza alisema atapambana nao wakipeleka majeshi
 
Nilisema Mwinyi ni Jecha mwingine huko uganda

Mazee mapuuzipuuzi yasiyojiheshim huwa nayachukia sana. Hayana faida kabisa kwa jamii.
 
Kama ni wizi ama uhuni basi M7 amevunja rekodi maana hata wizi, unatoa kura mfano jimbo A badala ya kura 2000 unazichezea through cloudy system na kuzifanya kuwa 20,000. Lakini M7 analeta kura kwa Mwenyekiti wa Tume kutoka vijiji ambavyo hata havipo Uganda na havijawahi kuwepo labda vikafutwa. Afrika tunapoteza fedha nyingi sana katika hizi elections bure.
 
Hapa kwetu hivyo hivyo lile zee lenye upara lilikuwa linapewa namba nakutangaza kwa maslahi ya ccm.

Liliumbuka sana Pale Tunduma waliposhangazwa na idadi ndogo iliyotangazwa tofauti na ukweli

Asubuhi likarekebesha eti makosa yalitendeka Tunduma pekeee....kumbe wapi wizi....wizi....wizi....kote mpa wine akashinda.

Haya mazee yakiafrika haya weledi...hekima wala aibu yapo kimaslahi na utapeli zaidi sio haki
 
Back
Top Bottom