Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
NI BORA MAPUNGUFU YA J-KIKWETE, YALILIFANYA TAIFA KUBADILI MTAZAMO.
Leo Wapinzani ukiwauliza watakuambia ni afadhali ya Kikwete, lakini wao sababu yao kuu ni mikutano kubaniwa. Wananchi ukiwauliza wao watakuambia bora tumelingana lakini wafanya biashara ukiwauliza wao watakwambia Nchi imekuwa maskini zaidi mambo ya megonga mwamba. Watumishi wa Umma kwa kuwa wako kwenye Payroll ukiwa uliza watakwambia mfumo unarekebishwa. Yote kwa yote amani itawale.
Mstaafu Kikwete ni kweli alifanya mengi Mazuri sana tena sana, hii ni kwasababu ya celebrity yake, na kwakuonekana hivyo alipendwa sana na wengi, lakini waliita serikali yake ni Dhaifu kwakuwa alikuwa easy taker, lakini watu walifanya kazi na maisha yalienda bila bughuza.
Awamu ya nne aliachia nafasi ya wengine kung'aa maana yeye hakuogopa kumezwa, Bali alikuwa MTU kwa baadhi ya mambo bila kujali wivu.
JK hakuwa mchoyo kwenye Ridhiki kwa watu wote. Tatizo lake ilikuwa ni ufatiliaji tu wa mambo na utendaji wa watendaji wake. Lakini kama angeshituka dakika ya mwisho angeweza kurekebisha, lakini hilo lilisababishwa na baadhi ya Mawaziri danganyifu ambao hawakutaka astaafu kwa kuwatumbua.
JK, mzee wangu si kwamba alikuwa mpole bali Mwanasiasa Mkarimu. Ukarimu wake ndio uliomfanya wamkosoe sana lakini aliwafanya wakosoaji wake kuwa marafiki na maisha yakaendelea na serikali yake ikaendelea kumetameta.
Alipenda sana kusafiri nje ya Nchi ili kujifunza mambo mengi ya kuisaidia nchi yetu. Napenda sana kukutana naye nibadilishane naye mawazo ili nipate wazo la kuandika kitabu "RAIS KIKWETE NA DEMOKRASIA TANZANIA". Sina chuki na Kikwete hata kama katika utawala wake baadhi ya watendaji wake walinifanyia unyama ambao sitausahau, lakini nachelea kusema kuwa Jakaya kitukuu cha Kikwete alikuwa bora sana japo alikuwa mzigo kwa fumbo la kufumbiwa asijue kinachotakiwa.
Deogratius kitukuu cha Kisandu ni Mtanzania aliyekuta vyama vya Siasa vimeungana na kuwa CCM mwaka 1980 kipindi amezaliwa. Nasema hivyo JK alitenda haki hata pasipo hitaji haki. Niliwahi kumkosoa kuwa aachie Urais lakini kwa nia njema, kiongozi mzuri anapokosolewe hadhalilishi mkosoaji bali anamuokoa ili apate pa kurekebishia makosa yake.
Ndio maana tumeamua kuanzisha Chama cha Siasa cha Arena for Correcting Africa-Tanzania (ACA) kwa lengo la kufanya Masahihisho ya Viongozi barani Afrika na Tanzania kwa ujumla. Na tunaomba Mungu tupate usajili tutakapofika kwa msajili wa vyama vya Siasa.
Deogratius Nalimi Kisandu.
Mwenyekiti wa Taifa mteule wa chama cha ACA.
26 Jan 2017