Bora Mafisadi wa Kenya Kuliko Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bora Mafisadi wa Kenya Kuliko Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RealMan, Jan 27, 2011.

 1. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Wapendwa wanaJF,

  Nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya majirani zetu Kenya, Uganda na Rwanda kwa muda sasa.
  Wenzetu wana matatizo mengi ikiwa pamoja na amani isiyo thabiti lakini kiuchumi wanakimbia sana.

  Pale Rwanda yule mkuu wa nchi hana mchezo na rushwa ingawa anaandamwa kuvunja haki za binadamu.

  Uganda mzee M7 alianza vizuri kwa kudhibiti maambukizi ya ukimwi yaliyokuwa yanaua nguvu kazi na akaongeza uwajibikaji lakini pia uchumi mkuu wa waganda umeshikwa na wazawa.

  Kwa watani wetu wa jadi Kenya RUSHWA iko juu sana kuliko Tanzania lakini uchumi wao unakua sana na bajeti ya serikali haitegemei bakuli la wafadhili.
  Tofauti ya matajiri au mafisadi wa Kenya ni kwamba mabilioni wanayoiba wanawekeza nchini mwao katika miradi ambayo inafaidisha serikali kwa kodi na ajira kwa wakenya.

  Hapa Bongo - Tanzania ambapo mabillioni yanaibwa serikalini kila mwaka lakini hakuna investment za maana wanazofanya zaidi sana tunaambiwa watu wana vijisenti kwenye off shore accounts.

  Ufisadi ni dhambi lakini nadhani kuna ufisadi wenye faida. Kwa mfano mama aliyeolewa na mwanaume mlevi lakini akawa anamwibia (husband wake) ili watoto wasome, wapate chakula bora, kujenga nyumba n.k huwezi kumlaum.

  Je matycoon wa Tanzania wameifainyia nini nchi hii????
  Je mtazamo wangu ni sawa au ndio nami naanza kuwa fisadi??
   
 2. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kuna Wizara (Ministry of Nairobi Metropolitan Development) inayoshulika na uundwaji wa Nairobi mpya chini ya "Nairobi Metro 2030 Strategy".
  Pamoja na fujo zote the ball is rolling.
  Cant our corrupt system borrow a leaf from our good brothers??
   
 3. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  hakuna mafisadi wazuri, wote wabaya na wanaharibu nchi zetu. tunahitaji revolution kama Tunisia vile. ukiangalia kroll report uone vile akina Moi, kotut, Biwott walivyofilisi hii nchi utashangaa.. its dishartening that you think Kenyan politicians are better because most of us hate them with a passion. God help Africa
   
 4. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Smatta;
  Nakubaliana nawe mafisadi wote ni wabaya na kwamba tuanhitaji revolution kama Tunisia lakini je si kweli kwamba mafisadi wa tanzania ni wabaya zaidi??
  Moi anamiliki hectare kibao za mashamba ya chai na ng'ombe anagalau kuna mkenya ataajiriwa pale.
   
 5. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bora fisadi anayeiba na kuwekeza nchini mwake, au bora hata hao wenye human rights records chafu lakini nchi inakimbia, sisi hatutembei, hatukimbii tumelala na mafisadi wanendelea kutupora kama tukilinganisha nadhani sisi tupo kwenye hali mbaya zaidi....
   
 6. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  na sasa wanafanya out of court sttlement meaning unarudisha ulichoiba unaachiwa huru. Embu fikiria Liyumba na mabillion yote yale amefungwa for just 2yrs na akitoka raha kama kawa bse mahela yake hayajaguswa.
   
 7. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Tunahitaji viongozi wakali na wenye uchungu na nchi hata kama kufanya hivyo wataonekana madikteta.

  Kama watz tunaipenda sana CCM basi ushauri kwa waporaji wa uchumi ni kuziwekeza hapa nchini.

  CCM imeendelea kubaki haven ya mafisadi Tanzania
   
 8. k

  kishanda JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2015
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MIMI BINAFSI NAONA HIVI , HAWA WANAOCHUKUA PESA NYINGI ZA SERIKALI MAALUFU KAMA FISADI WANGEKUWA WANAWEKEZA HAPA NCHINI KWENTU KWA KUJENGA VIWANDA , KUWEKEZA KWENYE MASHAMBA ,ELIMU N.K . YAANI KUWEKA MIRADI MIKUBWA AMBAYO INAWEZA KUAJILI WATANZANI WENGI HASIRA ZA WATANZANIA KIDOGO ZISINGEKUWA KUBWA SANA MAANA WATU WANGELIKUWA NA AJILA.YAANI UCHUMI UNGEBAKI KUKUA PESA HAITOKI NJE .
  SASA HAWA WANAOCHUKUA PESA HIZO NYINGI KAMA INAVYOELEZWA KWENYE VYOMBO VYA SERIKALI WANAPELEKA NJE YA NCHI AIDHA WANACHIMBIA ARDHINI AU WANABADILISHA KWENYE DOLA HATIMAYE UCHUMI UNAYUMBA WATANZANIA WANAHANGAIKA.

  MIMI NAWASHAURI HAO MAFISADI WAKICHUKUA HIZO PESA WAENDE WAJENGE VIWANDA VIDOGOVIDOGO KWENYE MAENEO YA WAHITAJI, WAFUNGUE VIWANDA WATU WAPATE AJILA, YAANI KWA UJUMLA WAWEKEZE TANZANIA WATAKUWA WAMETENDA JAMBO ZURI , MAANA MTOTO ANAYEIBA ANALETA NYUMBANI NI NAFUU SANA KULIKO ANAYEKWAPUA NAKUAPELEKA KWA JIRANI BAYA ZAIDI ANAKWAPUA NYUMBANI KWAO HAPOHAPO. HIVYO NAWASHAURI HAO AMBAO WAPO KWENYENAFASI ZA KUFANYA HIVYO WABADILISHE MWELEKEO WACHUKUE LAKINI PESA IBAKI NYUMBANI KUNA NAFUU SANA HASIRA YA WANANCHI HAIWEZI KUWA KUBWA MAANA WATAONA HIYO PESA IMEFANYA NINI.

  MUNGU AWATIE MOYO WA HURUMA WAKUMBUKE KUWA JAMII IMEWAAMINI NA WANATEGEWA. AMINA.:A S-fire1:
   
 9. s

  sandy candy JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2015
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 490
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mmhh no comment!
   
 10. sr bachelor

  sr bachelor JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2015
  Joined: Aug 4, 2014
  Messages: 1,198
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hawa hawawezi kuwekeza hawana...akili hiyo..sana sana wanaenda kujengea nyumba vimada kule kijichi tu..
   
 11. Apologise lady

  Apologise lady JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2015
  Joined: Sep 16, 2013
  Messages: 6,007
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  HAPO ndio wanapokera, wao wanaiba pesa nyingi alafu maabara tunaambiwa tuchangie sisi kama sio uonevu nini?
  Viongozi wamejawa na ubinafsi na kupenda kuabudiwa, ndio maana wanakazana kuweka gap kati ya wao na wasakatonge sie ili tuwaabudu.
   
 12. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2015
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Asee wa huku kwetu wanakumbuka! Embua mcheki mramba alivyoiacha rombo? Rombo hawakumchagua tu kwa sbb ni mwanaccm lkn hata agombea kesho asubuhi na tadea anashinda. Unajua kilimanjaro tumeamua kwa dhati kabisa kuizika ccm! Kwenye strong hold zao hapa kilimanjaro tumeingia kwa kasi ya kimbunga! Mnamo mwezi oktoba asubuh na mapema kabisa siku yauchaguzi tutakuwa tunawasha mishumaa kwenye kaburi la ccm
   
 13. y

  yaliyomoyamo JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2015
  Joined: Oct 17, 2014
  Messages: 489
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Awekeze nyumbani?! likimbumburuka mumnyang'anye mali zote? si bora akafiche ng'ambo, kikinuka fedha zake ziko salama nje
   
 14. M

  MBATATA JF-Expert Member

  #14
  Jan 8, 2015
  Joined: Jul 23, 2013
  Messages: 544
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Ufisadi wa wenzetu: Mtu anaipigia mahesabu nafasi ya kupata mapesa mengi, na tayari ameshafikiria na kutambua atafanya nini nazo.Anasubiri fursa kwa utulivu.

  Ufisadi wa WaTz: mtu kajikiuta tu kwa baghati mbaya fursa ya kupata mapesa hii hapa, kisa ati aliimba sana sifa za Chama wakati wa Kampeni akapewa wadhifa wa kisiasa. Au mtu amesota na u-ofisa ndani ya serikali kwa kipindi huku akiangalia wenzie wenye fursa anachoona ni kwamba wanakula bata na kuzunguka zunguka huko nje full stop! Matokeo yake, upeo wake wa uelewa unaishia kuwaza kula bata na trip za nje. Ghafla anakutana na fursa ya kupata mapesa mengi...unategemea nini kama sio kuongeza idadi ya vimada na matanuzi ya kutaka sifa? Mifano si ya hao hao kina Liyumba?
   
 15. d

  dinosour JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2015
  Joined: Dec 2, 2014
  Messages: 623
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Watanzania tuko hapa kwasababu kuna viongozi wametufanya tuwe hivi!!! tulikuwa na kampeni ya kuwakamata wahujumu uchumi chini ya MORINGE SOKOINE!! serikali ikawafirisi hata maskini,wanyonge waliokuwa wamepata mali kwa njia halali wakawaacha vigogo!! hii yote ni chini ya CCM!! viongozi wetu wanaitaji waitwe miungu!! hawaitaji hata maskini apate kitu!! wakulima wamejitahidi kulima eti hakuna masoko!!! yaaani JK anazunguka dunia nzima kwa safari nyingi lakini hatutafitiii masoko? kila kitu kwao ni porojo? MAFISADI WANATUMIA FEDHA ZETU!! kuhonga vi kahaba!! mara hooo!!!!raisi,w/mkuu na makamu wa raisi wako ulaya kwenye fusa!! mbona hatuzioni wakija?? kwa hali hii mafisadi wetu hawaitajiki kabisa!!! ilani ya chama na falsafa za KUJITEGEMEA hazijatekelezwa tangia uhuru!!! je nchi yetu hii itafika lini? tukiendelea kuwaacha waovu na tunaowapa dhamana ya kusimamia maendeleo wanagawana fedha za miradi!!! hawastahiri hata kidogo...
   
Loading...