Bora Kupambana na Waasi Wa Msituni Kuliko Kupambana na Waasi wa Fikra | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bora Kupambana na Waasi Wa Msituni Kuliko Kupambana na Waasi wa Fikra

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanangwa, Dec 23, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Nawapa heko WaTZ.

  Kwa kupevuka kifikra. Kwa kukataa mafisadi wa CCM kufikiria kwa niaba ya WaTZ. Hii ni hatua kubwa katika kuelekea ukombozi wa taifa letu ambalo tunaambiwa lina utajiri wa dhahabu, uranium, tanzanite, ruby, makaa ya mawe n.k. lakini mamilioni ya WaTZ hawajui umbo wala rangi ya madini haya.

  Tukomae nao. Siku 100 za utawala wa mchakachuaji. Bado ninaona waTz wana msimamo uleule...CCM ni dudumtu. wezi. wabinafsi. waroho wa madaraka. mafisadi wasiokuwa na huruma na watanzania masikini.

  Tuhamasishe ndugu na jamaa zetu kuhusu huu uasi mtakatifu. uasi wa fikra. tuwaambie. tuwaelezee. uovu wa hiki kitu kinachoitwa chama tawala. inawezekana.

  2015 hata ccm waweke malaika. watapambana na upinzani mkali kuliko huu wa 2010.

  ni mimi mwanachama wa waasi wa fikra Tanzania.

  Ng'anangwa aka mtoto wa mkulima mlalahoi aliyefulia kuleeeee kijijini.
   
 2. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Habri ndio hiyo waTZ hatudanganyiki tena hata kidogo, tutapambana mpaka kieleweke.
   
 3. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,339
  Trophy Points: 280
  Ng'wanangwa,

  Hapo umesema kweli, hawa ni wezi.

  Chakula cha mchana kinaiva kumbe jamaa wameweka magunzi watoto tunaendelea kucheza, bajeti ya mchana imeuzwa kwa wengine.

  Lazima tukomae, bado hawa ni wezi wale wale.

  Wengine ndiyo wamekuwa watalii, wanaoga kuiba kama walivyozoea sasa wanajihahalishia kwa kutengeneza safari.

  Huu ni upuuuuzi, lazima wote tusimame imara. Tumechoka
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Inawezekana.

  Mbona CUF wamewakomalia Zanzibar mpaka CCM wamenawa? Wameamua kuungana nao.
   
 5. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wewe Ng'wanangwa, unataka kuhatarisha amani na utulivu wetu?
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  omutima wange unahatarishaje amani na usalama?

  au amani yetu ujinga wetu?

  tumeng'amua.
   
 7. semango

  semango JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kweli 2015 itakua kivumbi na jasho
   
 8. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Basi natuwapatanishe Slaa na Zito halafu tumuombe JK Muungano!
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuna usemi mzuri sana "Kutodanganywa pia ni Kudanganyika" JF member

  CCM huku bara wanaweza kutawala fikra za watu haraka sana!

  Assume ushindani ni kati ya wafuatao

  Magufuli (CCM) vs. Slaa (CDM) or

  Sitta (CCM) vs. Slaa (CDM) or

  Maghembe (ccm) vs. Arfi (cdm)

  Kelele zote zitaisha wanachukua kilaini ..just think critically!
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  kwa sasa Tz haina amani ina utulivu tu! Kama unajua maana ya amani ndo uongee! Unakuja wakati ambapo Tanzania usiku utakuwa mchana,uwezo tunao na nia tunayo na haki tunayo. Tutapambana kama si kwa nguvu basi kwa fikra. Sitakufa bila kuchangia Tz iwe nchi huru,ee Mungu nisaidie!
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Ndugu tunasema tena asubuhi na mapema akina Magufuli, Mwakyembe, Sita, Mama Tibaijuka, Shy-Rose Migiro na MALAIKA WENGINE kama bado wamo ndani ya CCM kwamba SWALA LAO LINAFIKIRIKA TU kwetu sisi vijana pindi wakituomba kuwachagua WAKIWA NJE KABISA YA CHAMA CHA MAFISADI cha Rostam Aziz na Lowasa.

  Vinginevyo wasahau kabisa mbali na kuwapenda kule!!!
   
 12. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao wote hakuna kitu!
  Wamo kwenye kapu lililojaa samaki waliooza kitambo sana!
  Hawatufai kabisa kwa kuchoma wala kubanika,
  Hawatufai kwa kusafisha wala kuanika,

  Bora wangewahi mapeema kutoka humo ndani ya kapu la JK.

  LINANUKA!
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Thububutu kujitokeza na chochote wazo hata kama ni la kisomi na umeufanyia utafiti au kwa uzoefu tu, alimradi utofautiane na MAFISADI wanavyotaka bali ujue wewe ni MAREHEMU MTARAJIWA. Lakini sasa NASEMA BASIIIIIII, liwalo na liwee!!!!

  Sasa ndio hivyo walimu hao hao na wasomi wengi tu wakija na mawazo mazuri ya kufanyiwa utafiti lakini ikitokea tu kwamba yamepingana na yale ya watawala wanavyotaka ndio kesho yake unasikia Mwalimu huyo huyo mara kapigwa risasi na watu wasiojulikana getini kwake.

  Acha taifa letu liendelee kudumaa na mawazo mgando. Maendeleo kamwe hayawezi kupatikana kama Wa-Tanzania wote tunamawazo wanayofanana.

  Ukweli huu hata Mzee wetu na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Warioba aliwahi kunukuliwa akisema kwamba ukiona katika kijiji fulani Vijana wanazo mawazo yanayofanana na yale ya wazee wao kwa kila njia na kwamba muda wote hushinda pamoja tu wakipiga gumzo basi wala usijisumbue kuuliza kiwango gani kijiji hicho kitakua kimejiweka kimaendeleo. Tanzania kama taifa hatuko mbali sana na ukweli huu.

  Lakini kubwa zaidi, kuna mwana-JF mmoja humu ndani anaitwa Ndg Ng'wanangwa ameliweka vizuri zaidi hali tulio nayo sasa hivi nchini mwetu akisema kwamba 'NI AHERI KWA SERIKALI KUPAMBANA NA WAASI WANAOPIGANA HUKO MAPORINI KULIKO KUPAMBANA NA WAASI WA KI-FIKRA' jinsihali ilvyo sasa. Hii ni kauli nzitu sana, sana, sana!!!

  Ni taathmini wa hali ya juu. Na maana yake ni kwamba wasomi kwa kuwa wamefika mahala mawazo yao hayasikilizwi, hayathaminiwi wala kuzingatiwa huku taifa likiendelea kuporomoka kana kwamba hakuna hata msomi mmoja tu basi ndio chanzo cha haya yote.

  Na wasomi vijana, hii ndio maana hasa kwetu kung'angania kutaka KUFA NA MAFISADI NA NDUGU ZAO ambao wengi wao ni mbumbumbu tu.Huu ni wakati mzuri sana ndugu, jamaa na marafiki wa MAFISADI kuwambia watu hawa kujitokeza waziwazi na kutuomba msamaha kama taifa laa sivyo na wao gharili itawakumba.

  Mwisho, ni rahisi sana kuua mwili wa watu kibao tu lakini KAMWA HAKUNA ALIEWAHI KUSHINDA VITA DHIDI YA'WAZO'. Kwa mfano tu, hata Prof Haroub Othman aliondoka lakina swala la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio hii hapa imekodoa macho.

  Prof Mwaikusa katuacha kaondoka zake lakini swala la Mgombea Binafsi ndio hiyo Wa-Tanzania pamoja na EU tumelivalia njuga mwili mzima!!!!
   
 14. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Pamoja tuna safari kubwa sana kuondoka katika mawazo mgando
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  ukweli lazima usemwe.

  wauwaji na anayeuwawa wote watakufa. kufa si suala la kujadili au kumchulia mtu.

  uasi huu lazima tuuendeleze vizazi na vizazi.

  nchi hii itafika mahala itakombolewa kutoka mikononi mwa walanguzi.
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Jan 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MHE KIKWETE: MCHAKATO MZIMA WA KUANDIKWA KATIBA SHARTI UWE KWA NJIA SHIRIKISHI

  Mhe Kikwete asikubali KATIBA MPYA kwa misingi ya UJANJA UJANJA jambo ambalo litachokoza zaidi maelewano kupotea.

  Mchakato mzima uanzie bungeni kuliko na wawakilishi wa wananchi. Hakuna tena busara za mtu mmoja ikulu kuamua kwa peke yake mambo ya taifa zima kwa kuwa imani kwake ni kiduchu. Baada ya Bunge kuundwa Tume ya taifa ya Kuratibu Mchakato wote wa kuandikwa KATIBA MPYA tume hii itakua ikiwajibika kwa bunge na wala si mtu mmoja.

  Kwa maana nyingine uandikwaji wa Katiba MPYA nchini mwetu ni SHARTI iwe SHIRIKISHI KWA WADAI WOTE tangu hatua za mwanzo kabisa hadi mwisho; (1) tangu kuandaa Adidu za Rejea, (2) kuandaliwa kwa RATIBA ya mchakato mzima wa KATIBA (3) uteuzi wa wakusanya maoni.

  Hii ndio njia sahihi na tunayoipenda.
   
Loading...