Bora Elimu: Kwa njaa ya masaa 20, mtoto atafundishika darasani?

Hoja yako Ni mzuri na ukweli unafahamika kwamba mwanafunzi hawezi kusoma huku akiwa na njaa.

Ila wazazi wanahamini sera ya elimu bure,,, Ngoja waje wajibu .
 
Hata kwa waalimu ni shida pia. Unafundishaje darasa lililo choka na wewe ukiwa umechoka?. Au unawaza mipango yako mingine uliyokuwa unafanya inasimama.
 
Inasemekana nchi inajitosheleza kwa chakula na aziada.
Hii kama ni kweli basi kuna viongozi wana roho MBAYA. Wanashindwaje kuratibu hata hiyo ziada watoto wakala shuleni?

Sijawahi kuamini kua hii nchi imewahi kujitosheleza kwa chakula.

Wakati nipo S/msingi kuna miezi walimu walikua wanaendesha zoezi la kujua wanafunzi wangapi wamekula mchana kwao. Shule nzima ni watoto wa waalimu tu ndio walinyoosha mkono kua wamekuka.
 
Tatizo lako hufuatilii vyombo vya habari.
Hujasikia nchi yetu imeingia kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa Kati?
Nunua TV na Redio mkuu
 
Siku zote vitu vya bure vina shida, wapenda vya bure wataendelea kusifia huo utaratibu!
 
Shule za binafsi zitaendelea kufanya vizuri wakati wote.
 
Kweli Tz ni nchi ya walalamikaji tu, wewe ada hulipi bado unashindwa kujiongeza angalau kwa kumpikia mwanao kiazi Cha Kula shuleni. Unataka kila kitu serikali ihusike. Mambo hayawezi kwenda kwa staili hiyo. Isitoshe kila shule inakaa vikao vya wazazi. Kama mnaona inafaa basi wazazi mnaweza kuamua nakuadhimia kuchangia gharama za chakula cha mchana kwa wanafunzi. Serikali haijakataza hilo.
 
Hivi unashindwaje kumhudumia mwanao kula shule hadi uje kulalamika humu, au ndiyo kampeni za michango zenu zilizopigwa biti na serikali?
 
Umemakaa kwa shemeji yako unaandika upupu tu,zunguka vijijini uone watoto wanavyoteseka
 
Back
Top Bottom