Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,994
- 144,329
Cha ajabu, watu hawa ambao kwao ni mwiko kum-challenge Rais alie madarakani katika kugombea uraisi kupitia chama chao,ni watu hawa hawa wako busy kumshambulia Mbowe na CHADEMA kwa ujumla kisa tu Mbowe kaamua kugombea tena.
Hawa watu ni wanafiki sana na lengo lao kubwa sio kutetea demokrasia, bali ni kutaka kuweka pandikizi lao ili lije kuyumbisha chama kwa masilahi yao ya kisiasa.
Msisahau kuna mtu ameapa kuangamiza upinzani na hawa wanafiki wanaojidai kutetea demokrasia ndani ya upinzani, hawajawi kumpinga mwenyekiti wao anaetaka kuua demokrasia ya vyama vingi.Wanafiki wakubwa!!
Lingine la ajabu, ni watu hawa kufurahia wagombea wao kupita bila kupingwa kama tulivyoona kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tena kwa kutumia mbinu zenye utata alafu watu hao hao wanataka Mbowe asigombee bali aachie wengine wakidai ndio demokrasia.Wanafiki sana!!
CHADEMA kamwe msiwasikilize CCM kwani hawatahili kuwashauri chochote na kama wana cha kushauri,basi waanze kushauri ndani ya chama chao ambako hata demokrasia ya kuchaguana kwa sasa ni mtihani.
Mchakato wa kupata wagombea kupitia kura za maoniu ndani ya CCM ni mfano mzuri wa nini kinaendele leo hii ndani ya chama chao kuhusu demokrasia na haki ya mtu kuchagua ama kuchaguliwa.
Mwisho,CHADEMA chagueni mtu makini na mfia chama (awe Mbowe au mtu mwingine yoyote yule) mradi tu awe ni mtu ambae kamwe hatoweza kutumika kutimiza adhima ya Bwana yule ya kutaka kuua vyama vya upinzani nchini.
Sambamba na sifa nyingine,sifa ya muhimu na ya kuingalia kwa jicho la tatu katika kuchagua mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa, ni awe mtu ambae hatoweza kutikikiswa wala kushawishiwa kwa namna yoyote ili mpaka afikie hatua ya kusalimu amri na kukibomoa chama, vinginevyo tutakuja juta huko mbeleni.
Bwana yule uchaguzi huu kwake ni muhimu kuliko hata wa ndani ya chama chake.