
- Joined
- Mar 18, 2014
- Messages
- 1,942
- Likes
- 1,319
- Points
- 280

NANDERA
JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2014



wiki hii nimesoma kitabu maarufu sana kwa sasa, kiitwacho NDOA YANGU, NINGEJUA. Nimekipenda sana kwa sababu kinaeleza kwa kinagaubaga kwa nini ndoa nyingi hazina amani. Kwa kweli kimenigusa kwa sababu kuna sehemu mtunzi ameeleza historia ya ndoa yangu utadhani ananijua, na hasa zaidi maswali aliyouliza: 1. KAMA UNGEJUA MKEO AMA MUMEO ATAKUWA NA TABIA ALIYO NAYO SASA, JE UNGEKUBALI KUOANA? swali hili ni zuri kwa sababu kwangu mimi nisingekubali, na hata mke wangu alipojibu swali hili, nae akasema asingekubali. Ukweli kitabu hiki ni kiboko, na ingawa nimekiazima, kwa kweli sitamrudishia mwenyewe, nataka nikisome zaidi na zaidi nitambue makosa yangu na huenda kikanisaidia pia katika kuwashauri wenzangu.
Kitabu cha pili nilichosoma kinaitwa MY DEAR BOTTLE, ukianza kukisoma andaa mbavu zako, maana kinaonyesha jinsi ambavyo pombe kumfanya mtu akapoteza utu wake na thamani kwa wengine
Kitabu cha pili nilichosoma kinaitwa MY DEAR BOTTLE, ukianza kukisoma andaa mbavu zako, maana kinaonyesha jinsi ambavyo pombe kumfanya mtu akapoteza utu wake na thamani kwa wengine
Kama wewe kimekusaidia na unatamani kukisoma tena na tena ili uweze kuwashauri na wengine kwa nini upange kutokukirudisha badala ya kupanga kukirudisha na kununua cha kwako? Huoni kama ni dhuluma na kukosa shukrani? Aliyekupa unadhani hataki kukisoma tena na tena kama wewe au unadhani hana ndugu na marafiki anaotamani wapone kama wewe? Tunapowaazima vitabu si kwamba tunakuwa hatuvihitaji tena ila tunakuwa tumeamua kutanguliza mahitaji yenu mbele na kuweka ya kwetu nyuma. Samahani bwana. Ni kwamba comment yako imeamsha kumbukumbu ya vitabu vyangu nilivyodhulumiwa. Mrudishie mhusika kitabu chake na umuombe radhi kwa kukichelewesha. Vinginevyo unamkatisha tamaa asiweze kuhudumia wengine kama alivyokuhudumia wewe. Dhuluma ni dhuluma hata kama si fedha.