Boniface Jacob mgombea ajaye jimbo la Ubungo CHADEMA

Chagas democratic movement

Sent from my Infinix X624 using Tapatalk
 
Hata kama kubenea akibaki illa ajiandae kisaikolojia!! Mr Jacob jimbo lipo wazi wewe tu.
 
Wakazi wa Ubungo ndio watakao chagua mbunge wao,hiki siyo sampuli ya viti maalumu.
Ubungo wanataka mbunge wa kutatua ISSUES zinasohusu Ubungo kwanza na si vinginevyo.
Ni muda mrefu ubunge wa Ubungo umegeuka jamvi la wakuja.
Ubungo inategemea sana wazawa na wakazi wao wawili mmoja ni yule kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya mikoa ya kaskazini,aliewahi kuwa publicity secretary wa Yanga Mhe.Jerry Muro,na mwingine ni meya na mtoto wa kijiweni Mayor Boniface
Hawa watu wawili wakichuana itakuwa sawa na vita kuu ya tatu.
Jerry Muro alishafeli kabla hata hajatangaza nia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili halina mjadala. Bwana Mdogo Boniface amewapigania Wana Ubungo wote hata zaidi ya mpaka yake ya udiwani.

Ni wazi pia Kubenea ataondoka Chadema. Kwa tunaofuatilia series of events za Chadema tangu zivuje Voice notes za Kumdhuru Boniface Jacob kwa lengo la kumdhoifisha Mbowe asigombee Uenyekiti Chadema (Walioshiriki kwenye zile Sauti wanajulikana) na (walio Kuja kugombea na Mbowe wanajulikana) na (kilichotokea baada ya Mbowe Kushinda kinajulikana).

Kubenea haaminiki tena ndani ya Chadema. Inaelezwa kuwa 'amevumiliwa' sana na sasa Chadema wapo radhi aende zake kama alivyofanya swahiba wake, Anthony Komu. Kikubwa katika siasa, hakuna uadui wa kudumu kwaiyo wanaweza baadae wakaunda timu moja kwa Milango utakaokuwa wazi nyakati hizo ila kwa sasa aliyeandaliwa na anayeandaliwa kuwa Mbunge wa Ubungo ni Mdogo wangu Boniface Jacob.

Boniface Jacob ameshawaaga wakazi na wapiga kura wake kuwa hatagombea tena Udiwani na hivyo hata kuwa Meya tena wa Ubungo baada ya kuweka historian ya kuwa Meya wa Kwanza wa Manispaa ya Ubungo ikiwa chini ya Chadema.

Mimi Binafsi namuunga Mkono Boniface na kumtakia kila lenye heri. Kazi alivyofanya kwa wanaubungo haijifichi ni kubwa na kila mtu timamu anayeishi Ubungo ambaye hajafaa joho la uwendawazimu anaelewa.

Inasadikiwa kuwa Kiongozi mmoja wa ngazi ya JUU katika mkoa fulani analitolea macho na udenda Jimbo hilo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha MBOGA MBOGA ilhali Mwana JF Mkongwe pia anatamani pia kugombea Jimbo hilo kwa tiketi ya Mboga Mboga pia.

Muda utaamua.

Alamsiki,
Mzito Kabwela
Ya kweli hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom