PastorPetro
Senior Member
- Feb 25, 2008
- 189
- 36
Naona huyo jamaa Kibira yuko tayari kumwaga filamu nyingine:Nimepata hii kwenye barua pepe.
Moja kwa moja kutoka mjini Dar-Es-Salaam, tunafurahi kutangaza siku ya uzinduzi maalumu wa sinema ya Bongoland II. Tarehe ya uzinduzi ni mwezi April 5, 2008 hapa mjini Minnepolis, Minnesota katika ukumbi wa sinema wa Oakstreet Cinema.
Sinema hii ilitengenezwa mwaka jana July pale mjini Dar. Vitongoji maarufu vya mji huo kama Manzese na Magomeni vilitumika katika utengenezaji wa sinema hii. Kusema kweli, hii itakuwa ni hadhi kubwa ya wasanii wa ki-Tanzania maana sinema hii itaonyeshwa katika tamasha mbali mbali za sinema za kimataifa.
Sinema hii ni inamhusu Juma Pondamali ambaye baada ya maisha na malengo yake kutofanikiwa nchini Marekani, aliamua kurudi nyumbani. Lakini visakato alivyovikuta nyumbani vilimshangaza sana na hakuna kitu chochote hapa ulimwenguni ambacho kingemtayarisha kupambana na visakato hivyo. TRELA MPYA
Jitayarishe kuwaona wacheza sinema wakongwe wa Tanzania kama Mzee Kipara, Bi Chuma Selemani Mzee na Bi Thecla Mjatta. Vile vile pia kuwaona wachezaji chipukizi kutoka mjini Dar-es-salaam.
Msanii mhusika mkuu ni Peter Omari ambaye anacheza kama Juma. Peter, ambaye kwa sasa anishi Mwanza, aliwahi kucheza katika sinema yetu iliyopita iliyoitwa TUSAMEHE.