Bongoflavor na ujumbe mzito! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongoflavor na ujumbe mzito!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rwabugiri, Jan 3, 2008.

 1. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nilitokea kuvutiwa na mdundo wa wimbo wa ‘’Marlaw’’ wa rita sikiliza hapa
  http://www.jamboforums.com/bongoflava.php

  Nikiendelea kusikiliza nikaguswa na kisa kinacho simuliwa ndani ya wimbo huu, na mwishoni muimbaji akahitimisha kwa kusema hii ni true story!!

  Lakini pia nilisha sikia kisa kinacho endana na hicho juu ya watoto fulani yatima, mmoja wao yule aliimba wimbo wa kipindi cha watoto show cha ‘’redio one’’(kama nakosea nisahihishe) Uyatima wao unahusiana moja kwa moja na kisa cha wazazi walio tengwa kwa mmoja wao alikuwa na asili ya kiasia!

  Ghafla nimejikuta nikiguswa na wimbo huu, na ukanikumbusha mjadala mkali tulio ufanya hapa juu ya miss Tz 2007. Basi nikaingiwa na mawazo/maoni yafuatayo:

  -Huyu Rita ndugu zake wenye asili ya kiasia ‘walimkolimba’ moja kwa moja kwa vile tu aliolewa na mmatumbi, ama walimsababishia kifo kwa kumtia kashi kashi kubwa!
  -Hata tujipendekeze vipi kuwaita hawa waasia wenzetu, bado wanatuona sisi si binadamu mbele yao, ndo maana walifikia hatua ya kumfanyia walichomfanyia Rita

  Wito:
  Huyu mwimbaji yupo, na anaweza saidia wana harakati kuanzisha uchunguzi wa kilicho tokea, ili isaidie kuondoa huu ubaguzi na chuki iliyo wazi kwa hawa wenzetu wenye asili ya asia,(hebu fikiria hatima ya huyo mtoto aliye ondokewa na mama yake?) kwani vinginevyo hii kitu inazidi kukua ndani kwa ndani kesho na keshokutwa itamtokea mwingine (mfano, hata mzee wa kijiji tumeona katika matamanio yake ya mwaka huu ni kuona posa yake inakubaliwa, sasa isije kuwa chemistry ya moyo wake ilimpeleka kwa dada yetu Richa na yakampata yaliyo mpata huyo aliye kuwa amemuoa Rita lol!)

  Wana JF karibu kwa maoni juu ya ujumbe mzito ndani ya wimbo huu.
   
Loading...