Bongo tyube. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo tyube.

Discussion in 'Celebrities Forum' started by ngoshwe, May 15, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kuna hii site BONGO TYUBE.

  Inaonekana ilianzishwa kwa malengo mazuri sana ya kusaidia kutanganza miziki ya kibongo nk. Hata hivyo inaoekana kama wamilki wake wamekwenda likizo.

  Aidha,ukipitia mashrti ya kuhusu Hakimiliki ya site hii inaonekana kana kwamba pengine inaweza kuwa ngumu kwa wasanii wa Kitanzania kuweza kufuatilia haki zao iwapo itatokea ukiukwaji wa hakimiliki utakaofanywa kwa kuhusisha site hii kwani inataja sheria zitakazotumika ni za Marekani. Sina hakika kama wahusika "JIMICHU LLC" ni wamarekani au lah kwani hakuna anwani zao kamili kwenye site, japo anatajwa Bw.M.Michuzi kuwa ndie mwakilishi atakae pokea malalamiko yote yahusuyo ukiukwaji wa Hakimiliki.

  Kama yupo anayefahamu kwa kina hii site tafadhali msaada wa kujua kwa nini haipo "updated" na kwa nini ikatumia sheria za Marekani ikiwemo kushughulikia migogoro ya hakimilki za kazi za Wasanii wa Kibongo??.
   
Loading...