Dubai bi moja sehemu inayoendelea kwa kasi kubwa,cha kupendezesha jamaa wameamua kutumia mali ya asili waliyonayo mafuta kuendeleza nchi yao mainvesta kutoka sehemu zote za dunia wanawekeza pale,Tanzania nasi tunaweza kufanya kama Dubai kama tunataka kwani tuna kila kitu,ila inatubidi tuanze sasa kabla ya vitu vilivyobaki kuuzwa kwa wajanja.naona kwa kuanzia Gorv ijenge barabara zote zinazounganisha wilaya kwa wilaya kwa kiwango cha lami,kwa kufanya ivyo tutakuwa tumepiga atua kubwa sana kisha kuacha kutumia jembe la mkono na kutumia matrekta katika kilimo,kuvuna na tuwe na wakulima wachache sana,pia kuanzisha viwanda vipya,ambavyo tutazalisha maitaji ya soko la ndani na nje ya bongo,pia elimu iongezewe nguvu zaidi na kila mtoto apate elimu kwa kufanya hivyo basi tutakuwa tunakwenda na mageuzi kama ya Dubai,India na China.