popiexo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 742
- 183
Nimejaribu kulinganisha kati ya vipindi hivi viwili, nikagundua kwa TPF wako vizuri sana katika kuandaa shindano lao kuanzia mwanzo kwenye upatikanaji wa washiriki na hadi kwenye shindano lenyewe. TPF ni acedemy ikiwa imeandaa walimu wazuri kwa ajili ya kuwafundisha washiriki wakati wote wa mashindano tofauti na BSS, majaji wa TPF pia wako vizuri sana wakiwakosoa washiriki na kuwaeleza wapi hasa wanamapungufu tofauti na BSS ambapo majaji wanabore, wanawakosoa washiriki bila kusaidia kuwajenga, utakuta jaji anasema ooh mimi nilikuwa nimelala kwa jinsi ulivyo imba vibaya. Matokeo yake BSS haichangii kabisa katika kuinua vipaji, ukizingatia washindi wote wa BSS hakuna hata mmoja aliyesimama kwenye fani wote wamechemsha, na nafikiri huwa wanapatikana kwa kubebwa. Mwaka huu sijui watambeba nani?