Bongo Star Search (BSS) na mshindi mzungu!!

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Shindano la kumsaka superstar wa bongo wa muziki linafikia tamati leo huku kukiwa na uwezekano wa mzungu joseph pyne ambaye zaidi amekua akitamba na wimbo wa "malumbano/ msongamano" kuibuka mshindi baada ya kuonekana akiongoza katika kura zilizooneshwa wiki mbili zilizopita.

Naomba endapo mzungu ataibuka mshindi yasijitokeze yale yaliyomkuta richer adhia miss tanzania aliyeshambuliwa na makundi ya watu pamoja na vyombo vya habari kwamba wamechagua mshindi ambaye ni "muhindi" Inavyoelekea hakuna utaratibu unaowataka washiriki wa shindano hilo wawe raia wa tanzania ndio maana majaji walimpitisha kwenye mchujo!!!
 
Huyo ni mzungu kachumbari au pure? Bongo maanake Tanzania hivyo mzungu hawezi ku-qualify kuingia kwenye mashindano ya Bongo flava. Kama Bongo star search ni international competition basi sawa lakini mbona warundi hawamo?
 
Mtanzania ni rangi au uraia? Panueni wigo wa fikra mko hatarini kuachwa pabaya with xenophobic mentalities. We increasingly becoming a global village where our talents are in competition globally!
 
Nadhani ni vizuri wale wote wenye kutamani sana asishinde huyu mzungu wanapiga kura nyingi sana kumchagua mswahili mmojawapo wanayehisi anaweza.
Kama sivyo, hao nao ni wanafiki tu, wale wapenda maneno matupu bila matendo, wenye kumpenda mzunguu wanapiga kura, je nyie wenye kumpenda mwingine mbona hampigi?
Mwacheni mtoto wa watu atese na wapenzi wake, wenye kuona utamu wa kipaji chake.
 
mhuu huyu mzungu anastahili kwani anaweza kuimba tuache mambo ya uzungu ama ubongo tu judge kitu kwa kuangalia uwezo wa mtu
 
Aaah huyu mzugu wamchakachue tu hata akishinda tuwape wabongo. UTAIFA MBELE. Watanzania tuache umbumbumbu Rangi na uasili Vinamata sana kwa utaifa kote duniani. Kama tunabaguliwa tukiwa nje huu ukondoo wa kulamba viatu rangi nyeupe unatoka wapi? COME ON?.
 
Mbona mt base wanachukua hadi wabongo? Tusker je? Ukweli uliowazi mzungu anajua kuimba na anafuraisha sisi watazamaji kuliko hao wabongo wenu kazi kubana pua tu wakati wa kuimba. Lengo moja wapo la mziki ni kuburudisha hadhira ya watazamaji na katika wote hao yule mzungu ndo anaburudisha kweli na ndio anayefanya watu waangalie bss.
Akishinda ni haki yake na si hao wabongoo wenu full mapozi baada ya kuimba nyooo
 
attachment.php
attachment.php
attachment.php


Usiku wa leo Ijumaa ya mwezi huu itakuwa ndiyo siku ya kutegua kile kitendawili ambacho kilikuwa kikisubiriwa kwa muda mrefu cha yule "The Next Bongo Super Star" ambapo wale washiriki watano bora kwa mwaka huu watakapopanda jukwaani kuonyesha ujuzi wao.

Washiriki waliobakia mpaka sasa baada ya mchujo wa wiki iliyopita ni washiriki watano ambao ni Mariam Mohamed, James Martin, Joseph Payne, Bella Kombo, Waziri Salum ambao kwa pamoja wametokana na kura zenu.

BSS mwaka huu ilikuwa na jumla ya washiriki elfu 6 (6000) toka usaili wa mikoani mpaka kufikia Top 20 na mwisho kabisa Top 5 ambao siku ya Ijumaa ndipo atapatikana mshindi mmoja ambaye atatawazwa kama mshindi wa BSS 2010.

Mshindi wa mwaka huu atajinyakulia kitita cha shilingi Milioni 30 (TSH 30,000,000/=), pamoja na zawadi nyingine nyingi.

Utabiri wangu ni kuwa mzungu aka "CIA attache" kushinda leo!!
 

Attachments

  • wote leo.JPG
    wote leo.JPG
    41.3 KB · Views: 229
  • mutta.JPG
    mutta.JPG
    41.4 KB · Views: 228
  • mzungu na mariam.JPG
    mzungu na mariam.JPG
    30.7 KB · Views: 214
mzungu anajua kuimba - pamoja na wengine lakini yuko juu - ingawaje hajui kucheza hizo nyimbo anazoimba - ila inaoneka WATZ anawapata sana kwenye nyimbo anazochagua. All in all hivi atakayeshinda akipata 30m na wengine wanapata nini jamani???

sometimes BSS is entertaining ..........................
 
binafsi napenda sana mzungu anavyoimba,pia ningependa sana ashinde kwakweli kama wanaangalia ubunifu na kipaji hasa jamaa anacho,sema sijui kama kigezo cha ushindi lazima uwe mtz au la,wat I ad ni kuwa mshindi wa kwanza M 30,wa pili M10,wa tatu M5,But my vote goes tu mzungu mzalamo
 
anajitahidi kuimba lakini hastahili kuwa mshindi. uwingi wa kura anazozipata ni kwa ajili ya huo uzungu wake watu wanapenda awepo kwa sababu wanamwona kama kiburudisho jambo ambalo wanakosea badala ya kuangalia mwimbaji bora wenyewe wanataka viburudisho. maana naona ni wimbo mmoja tu wa nendanenda ndo umemkaa kichwani basi, sidhani kama atakuwa competent kwenye nyimbo nyingine.
 
Mimi nawaasa msipige kelele kama hammkubali mzungu pigeni kura nyingi kwa mbongo mnayewaza atashida...Tatizo la wabongo kulalamika tu halafu hawapigi kura... yale yale ya dokta slaa...watu wanaacha kupiga kura wakiamini kuwa hatashinda japo wanampenda! Come on!!!!!!!!!11
 
Mimi nawaasa msipige kelele kama hammkubali mzungu pigeni kura nyingi kwa mbongo mnayewaza atashida...Tatizo la wabongo kulalamika tu halafu hawapigi kura... yale yale ya dokta slaa...watu wanaacha kupiga kura wakiamini kuwa hatashinda japo wanampenda! Come on!!!!!!!!!11
ya Dr Slaa yameingiaje huku na wewe!
 
Back
Top Bottom