Bongo Star Search (BSS) ina uozo mkubwa sana

Niliacha kufuatilia tangu wampige chini msechu

Na baada ya mshiriki wangu kuwaprove wrong akafanya vizuri kuliko mshindi wao nikajiaminisha najua muziki kuliko wao

Kupiga kelele haisaidii ukiona kitu ni cha kiboya unapiga chini watashtuka baadae
 
Katika program za hovyo hii inaongoza,Kwanza wasanii bora watano tu hapa bongo,hakuna aliyepita kwenye mikono ya BSS,wote asilimia kubwa ya walioshinda kwenye hii program,vipaji vyao vilipotea baada ya kushika mpunga,Kama kwa miaka kumi program haijawahi kuzalisha msanii mwenye hadhi Kama zuchu,au Sam wa ukweli,au Nandy,Marioo,whozu,hii program ni mfu
 
Bruce atarudishwa.
Kumbuka hadi kufikia hapo ukawaona nao ni ufanisi mkubwa.
Sio lazima washinde.

Je uliwahi kimsikiliza Fanabo aliyetolewa na Kayumba?
 
Katika maisha kuna kujua na bahati!

-Unaeza ukawa mjuzi ila huna bahati ukaishia kufa na kipaji chako.

-Unaweza kuwa na bahati ukawa kila unalogusa ni dhahabu mafanikio yakaja chap.

Ndio maana walimwengu wanasema lilia bahati katika maisha.
 
Nianze kwa kuwatakia kila la heri katika mwaka huu mpya watanzania wenzangu na wana JF kwa upekee na mkawe na mwaka mzuri utakaotimiza angalau asilimia themanin kama sio mia ya malengo ambayo mmejiwekea.

Mimi nimpenda burudan na napenda sana mziki hivyo napenda sana maingizo ya vijana wapya kwenye tasnia ya muziki na hili lilinifanya niwe nafuatilia moja ya vyanzo vya maingizo ya wasanii kwenye tasnia hii ambayo ni bongo starseach.

Bongo star search toka inaanza haijawai toa super star ambae inaeza kaa ikajisifia mbele za watu ila imetoa waimbaji maarufu ambao nao wapo kwa uchache kama vile kala Jeremiah, Peter msechu na kayumba, madam Rita na Master J wapo karibia misimu 11 lakin hakimu yule na producer wa muziki wa studio kubwa kabisa toka ianzishwe (MJ records) hawajawai tuletea full package kwenye kiwanda cha muziki na msanii mkubwa Tanzania

Nimekuja kugundua pamoja na uzoefu wa karibia misimu 11 na zaid ya miaka 20 kwenye muziki wale watu ni wapigaji wa hela kupitia vipaji vya vijana wenzetu. Wa kitanzania, mbali na kutotolea maelezo malalamiko ya baadhi ya washindi kutopewa hela zao hawa jamaa hawatakuja kuleta msanii mzuri kwenye tasnia hii.mfano mwaka juzi mshindi alikua Sarafina Michael huyu dada alikua full package yaan toka bongo star search ianze mpaka mda huu sijaona wa kufikia talent yake lakini kwa watu wenye kufuatilia tasnia ya muziki na wenye jicho la tatu tuliona kabisa sarafina hataweza kuendelea na muziki hata baada ya ushindi na kweli ndo alichokifanya Dada yule mwaka wa pili now hana hata nyimbo ya kwake ya kujivunia


Ndugu zangu naandika haya yote baada ya kuona madam Rita na team yake kuviondoa vipaji vya vijana wawili ambao wana vipaji vya ajabu na kama wangepewa nafasi wangekua bidhaa adimu kwenye hichi kiwanda ambacho kina radha zilezile miaka nenda rudi...Vijana hao ni Bruce na Gideon kan nitawazungumzia kwa ufupi


GIDEON KAN...huyu jamaa ametoka round ya 32 bora kwenye huu msimu wa 11.,ndugu zangu hata kama kuna mtu hajui muziki lakini huyu jamaa ana kipaji cha ajabu na kwa aina yake ya uimbaji hakuna wa kufanana nae toka BSS ianze na hata kwa wasanii waliopo sokoni kwa wakati huu.,huyu jamaa angeweza kutoa burudani na kufanya Hip Hop iwe na radha zaidi ya bongo fleva,anapiga guitar na anachana juu ya guitar, ana swags achililia mbali muonekano,ana perform live kuliko wasanii wote waliopo kwenye game wakati huu,anainjoi anachofanya na ilionesha wazi alienda BSS ili aingie rasmi kwenye tasnia ya muziki so sadly Rita na wenzake wake wamempiga chini kabla haja deliver tulichokiona kwake

Bruce... At least huyu ameishia 16 bora..Bruce ndugu zangu hakuna haja ya kufahamu muziki ili kuona kipaji chake.,kwa aina ya jinsi ana perfome,uimbaji wake ,mpangilio wa muziki,sauti yake ,upigaji wake wa guitar swagz sake ,muonekano wake ,flow yake alistahili kabisa kuchukua ushindi msimu huuu,alikua ingizo sahihi kabisa kwenye tasnia ya muziki so sadly majaji wanaojiita wana experience hawalioni hil...hakika Ritha endelea kuchezea muda na vipaji vya vijana wenzetu ili kila mtanzania aone uozo na upigaji mlionao kwenye mgongo wa kutafuta nyota wa bongo
Hao Bruce na Gideon kutolewa BSS siyo mwisho wa muziki, kama wanavipaji wataendelea
 
Washindi wa American Got Talent huwa wanatoboaga? (Naomba jibu kwa wafuatiliaji)
Liona lewis nais ni mfano. Alaf AGT uwezi ilinganisha na BSS kumbuka ile inachukua watu wa fani tofauti tofauti
 
Back
Top Bottom