Bongo Movie rekebisheni yafuatayo niangalie movies zenu

kibuyu180

JF-Expert Member
Oct 22, 2016
1,710
1,814
1. Wekeni mtaji wa kutosha ili kutengeneza movies zenye ubora na uhalisia. Kwa gahrama za kuandaa movie ya 3M mtawauzia ndugu, jamaa na rafiki zenu tu.

2. Utunzi wa hadithi ujae ubunifu. Video unapoitazama upate hamasa na udadisi, sio picha inaanza ndan ya Dk 15 huna haja ya kuangalia part 11 kwani umeshajua inaishia vp.

3. Punguzen hadithi za mapenzi tu. Jamii inahitaji na mambo mengine ya kujifunza. Sio mapenzi na uchawi tu.

4. Ombeni msaada wa kiserikal ktk kutumia baadhi ya maeneo, vitu n.k ili kuleta uhalisia chanya.

5. Punguzen bei ya CD zenu. Nendeni na hali halisi ya maisha kwa sasa. Niwaeleze tu wateja wenu wakubwa ni wananchi wa chini. Sasa ukimuuzia CD @ 5000. Hili akamilishe atahitaji 10000.

6. Badilikeni kimuonekano, si lazima kuvaa hereni mtoto wa kiume. Au kuweka wave kichwani na mapoda ya kutosha mtoto wa kiume. Na nyie wadada ubora wa video si kuvaa nguo fupi, ama kukaa kwa kuacha mapaja yote wazi. Ama kuwatumia wenye mata...makubwa.

Nawasilisha kwa leo.
 
Kingine si lazima watuoneshe mapaja yao na kufanya mambo ya kizungu, kingine ubunifu na usiriaz, haiwezekan mzimu unavuka barabara ukaangalia magari kushoto na kulia au jambaz s lazima avae koti ndefu na ajifunge maski au eti jambaz anavua viatu wakat anapotaka kuingia ndani.. badiliken bwana watu mnaigiza na mtu anajua kabisa mnaigiza?
 
Movie za kitanzania Baba amevaa maheleni analalamikia tabia za watoto wake kuwa mbovu.
Tanzania mitaani sijawahi kumuona baba wa hivyo labda jamaica
Bongo movie wanapaswa kubadilika, binafsi mahala pekee ambapo naangalia bongo movie ni kwenye mabus safarini
 
Watanzania ni wazuri sana kwa sura na maumbo mazuri pia, wanaume na wanawake, sasa mbona watu wenu wako hivyo? Alafu kwani lazima watu wakiongea wana onyesha kugombana tu! Alafu too predictable! Wanavuuuta sana!
 
Kingine si lazima watuoneshe mapaja yao na kufanya mambo ya kizungu, kingine ubunifu na usiriaz, haiwezekan mzimu unavuka barabara ukaangalia magari kushoto na kulia au jambaz s lazima avae koti ndefu na ajifunge maski au eti jambaz anavua viatu wakat anapotaka kuingia ndani.. badiliken bwana watu mnaigiza na mtu anajua kabisa mnaigiza?
 
1. Wekeni mtaji wa kutosha ili kutengeneza movies zenye ubora na uhalisia. Kwa gahrama za kuandaa movie ya 3M mtawauzia ndugu, jamaa na rafiki zenu tu.
2. Utunzi wa hadithi ujae ubunifu. Video unapoitazama upate hamasa na udadisi, sio picha inaanza ndan ya Dk 15 huna haja ya kuangalia part 11 kwani umeshajua inaishia vp.
3. Punguzen hadithi za mapenzi tu. Jamii inahitaji na mambo mengine ya kujifunza. Sio mapenzi na uchawi tu.
4. Ombeni msaada wa kiserikal ktk kutumia baadhi ya maeneo, vitu n.k ili kuleta uhalisia chanya.
5. Punguzen bei ya CD zenu. Nendeni na hali halisi ya maisha kwa sasa. Niwaeleze tu wateja wenu wakubwa ni wananchi wa chini. Sasa ukimuuzia CD @ 5000. Hili akamilishe atahitaji 10000.
6. Badilikeni kimuonekano, si lazima kuvaa hereni mtoto wa kiume. Au kuweka wave kichwani na mapoda ya kutosha mtoto wa kiume. Na nyie wadada ubora wa video si kuvaa nguo fupi, ama kukaa kwa kuacha mapaja yote wazi. Ama kuwatumia wenye mata...makubwa.

Nawasilisha kwa leo.
Haya uliyoorodhesha ni ya kweli. Na yanaonyesha tu jinsi tasnia hii ilivyo nyuma hapa Tanzania. Halafu tatizo lao kubwa ni kukimbilia kuigiza vitu na mazingira wasiyo na uwezo nayo. Kwanini wasichague vitu simple vinavyoendana na maisha yetu kila siku! Kingine... wanafikiri kuigiza ni kuchagua waigizaji wa aina moja tu... wanoongea sauti ya aina moja na kuvaa nguo za aina moja... Kwa kifupi waigize kitaalamu!
 
Sijashawishika na hawa wapaka hina wa bongo movies. Sizipendi filam za kibongo,hawana hata nusu ya kiwango cha wenzetu. Ubunifu mbovu, kuigana kwingi, location hizo hizo kila kukicha. Kuangalia bonhomie movies kwangu ni ushamba coz hazina ubunifu.
 
MSEMAKWELI NI MPENZI WA MUNGU.....

KINACHOIUA BONGO MOVIE HIKI HAPA

1. TEKNOLOJIA DUNI.....Movie nyingi sana za kibongo zimeigizwa huku zikiwa zinatumia teknorojia duni sana......uwezo wa kuchanganya picha na kuhusianisha na matukio bado ni mdogo sana ukilinganisha na uwezo wa nchi zingine zilizoebdelea katika sekta hii ya movie........matokeo yake movie nyingi zinakosa mvuto.

2. WASANII WENGI KUKOSA UBUNIFU.....Ni jambo lisilo la kificho kuwa waigizaji wengi sana wa hizi movie sio wabunifu na hapa tatizo liko kwa pande zote zinazohusu uandaaji wa hizo movie......UNASHANGAA MTU ANAAMKA ASUBUHI NA JANA YAKE JIONI ALIENDA OGA AKALALA LAKINI AKIAMKA ANA WANJA NA KAJIPODOA!!!! ....hii ni aibu.

3. SHERIA ZA NCHI YETU......Moja ya kikwazo kikubwa cha bongo Movie ni sheria za nchi......Nchini Tanzania ni marufuku kuvaa baadhi ya mavazi kama ya kijeshi.....pia kuna baadhi ya Bunduki haziruhusiwi kutumiwa na raia....jambo hili ni kikwazo kikubwa sana kwa bongo movie.....KINAWWFANYA BONGO MOVIE WAIGIZE KITU KWA MTINDO ULE ULE HIVO KUWACHOSHA WATAZAMAJI.

4. KUKUA KWA TEKNOLOJIA....hii ni sababu mojawapo ya kufa kwa bongo movie......hv sasa kanda moja original inaweza zalisha copy fake zaidi ya laki moja na zikauzwa kwa bei nafuu zaidi ya ile original....wezi wa kazi za wasanii ni pigo kubwa sana kwa wasanii wa bongo movie.

Sababu ni nyingi sana ila hizi ni kubwa sana zinazosabqbisha kazi ya sanaa ya filamu hapa nchini kuonekana sio nzuri na soko linaanguka siku hadi siku.

Nyingine ni waigizaji kujiingiza kwenye siasa hiyo imewagawa mashabiki.. Mfano ni Mm siwapendi au sipendi kuangalia muvi zote ambazo wasanii wote ambao ni mashabiki wa ccm
992232d4a85b97fc0af0c42746d89462.jpg
 
Halafu kuna baadhi ya wasanii wao siku zote wanataka waigize nafasi za ubosi au utajiri tu!Muigizaji wa kweli nafasi yoyote anaweza kuifanyia kazi.
 
Kuna filamu moja ya Kinaijeria inaitwa state of emergency humo ni fully uhalisia hadi inasisimua!Yaani huwezi amini kama ndiyo wale wanaogiza filamu za mapenzi.Hapa kwetu aliyezoea kuigiza nafasi za utajiri ukimwambia aigize nafasi ya umasikini,anaweza kurusha ngumi.
 
Kingine si lazima watuoneshe mapaja yao na kufanya mambo ya kizungu, kingine ubunifu na usiriaz, haiwezekan mzimu unavuka barabara ukaangalia magari kushoto na kulia au jambaz s lazima avae koti ndefu na ajifunge maski au eti jambaz anavua viatu wakat anapotaka kuingia ndani.. badiliken bwana watu mnaigiza na mtu anajua kabisa mnaigiza?
Yaah hawana ubunifu. Story waiba za ulaya
 
Back
Top Bottom