Bongo Hip Hop, MC mkali wa kizazi hiki ni dizasta vina

Guevara Jr

JF-Expert Member
Mar 29, 2017
300
811
Wasalaam, mimi ni mfuasi wa Hip hop(Underground) na leo natumia haki yangu kikatiba kumtaja Msanii bora wa mziki huu kwa sasa hapa Tanzania.

Dizasta.....Kutoka kundi la Panorama,kwa sasa anafaa kuvishwa crown na kuitwa Underground King. Alikuwa member wa Tamaduni music na anauenzi utamaduni wa Hip hop to the fullest.

Msomi asiyejigamba na elimu yake. Hana shobo za kibwege ila jamaa ni bonge moja la mwandishi.

Nimemfatilia kwa muda mrefu na nimesikiliza karibu ngoma zake zote. A man is superb. Ana tungo za hatari na nadhani alifaulu vema somo la Fasihi.

Raia hawamzingatii bado ila Kijana ni halfman half-rap machine . I'm sorry Unju bin upupu, crown namvisha Dizasta.

Naandika hii thread nikiisikiliza Nobody is safe 3 iliyotoka jana, unyama mwingi humu ndani. Marapa wenu wamechanwa vibaya mno

Mnisamehe wakongwe, Dizasta ni Kilanja Mkuu wa hiki kizazi. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Asante
 
Single sentence inayo analyse full chapter.

Hii ni no body is safe number1

Akaja akasema "kuna jambo dogo ambalo hata watoto hawajajua kuna joto ila dizasta ni wa moto kushinda juà"
 
Dizasta Vina ni zaidi ya msanii ase, huyu mwamba ni mzima kichwani sijawahi kujutia ngoma zake.
 
Back
Top Bottom