Bongo hatuna wahandisi+ viongozi hawaoni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo hatuna wahandisi+ viongozi hawaoni?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rugumye, Dec 10, 2010.

 1. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani Wabongo wenzangu, ni aibu mvua ya nusu saa maji kujaa barabarani posta mpya, posta baharini mita 100 tu kutoka baharini. kila mwaka tunashuhudia tatizo hili but no action. hivi hawa watawala wanafanya kazi gani? JIJI linatia aibu kwa kila kitu, foleni barabarani, takataka kila kona, mvua ikinyesha aibu tupu, jamani viongazi acheni uswahili, wahandisi tumiaeni taaluma zenu basi. mnashindwa kuchimba mtalo mkubwaundergraound? kuelekea baharini kuanzia labda somewhere? WALE WACHINA WALIKUJA KUFANYA NINI MIAKA 2-ILIYOPITA? juzi ilikuwa aibu ya mwaka pale akiba, sinza ndiyo usiseme. jamani aibu hii ni kichefuchefu. DR's Magufuli na Mwakyembe watuondolee aibu hii.
   
 2. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 4,935
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Alafu ukiwaita majina yao ya kawaida bila kuanza na Engineer someone wanamind kweli. Hakuna wanachokifanya majengo yao chini ya kiwango, barabara mitaro hata mtoto mdogo wa miaka 3 hazami, umeme mgao kila mwaka.
   
 3. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wahandisi wapo gesti na kimvua hiki wanapiga mikasi huku wakizuga wako saiti.
  Maji yakipungua na wao wanarudi ofisini huku wakijidai, saiti kazi ilikuwa ngumu kwelikweli leo.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Naona mkuu unaelekeza makombora yako kusiko kabsaaaa! Hivi muhandisi unaamka asubuhi unakuta maji yamejaa kule katikati ya jiji, jamboa ambalo limekuwepo miaka nenda rudi basi unaanza uhandisi. Ok nakupa jibu rahisi kabisa , for immediate action ni kupump out hayo maji na kuyamwagia baharini, easy and smooth. Anywayz that is if umeme kama utakuwepo hahaha!!!!!!!! Lakini otherwise for a long term solution kunatakiwa kufanyike upya design ya mitaro, sewarage systems, barabara pia mipango mji so as to cater for the mentioned services for some 100 yrs to come, You betcha ramani ya jiji la Dar kiujumla haileweki na inawezekana haipo. What Dar wil b next yr hakuna anaejua. Nakupa mifano kidogo tu yale majengo around Muhimbili, au ile Umoja heights na hilo linalotaka kujengwa nyumba ya sanaa kuna aliyejua ujio wake 10 yrs ago???? Kwa mtindo huu mtawezaje kuwa na drainage systems zitakazokidhi mahitaji ya miaka ijayo? Pia mkuu kumbuka uhandisi sio kazi ya kanisa au msikiti.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,470
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwanza sio kila mhandisi anajenga mitaro ya barabara..

  Pili, last time I checked hiyo mitaro ya Posta kule mliwapa tenda Wachina kwa sababu mna kihoro cha kuabudu wageni, ninyi na serikali yenu dhaifu ya wasanii.

  Tatu, mhandisi wa mitaro/barbara sio manake wewe unahodhi funds, ujuzi,vifaa na muda..unaeza kuwa na ujuzi lakini huna hivo vingine, na hiyo haikufanyi usiwe mhandisi..na haikufanyi iwe responsible na kila mradi chini ya jua..so hivyo vitu vina taratibu zake..usidandie gari kwa mbele.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Yaani jengo chini ya kiwango inasababishwa na wahandisi? Mgao wa umeme umeletwa na wahandisi? Du!!!!! Hamkawii kusema hata Dowans ililetwa na wahandisi!
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu u nailed it! Naona bado kuna watu wana hangovers za kikomunisti!
   
 8. e

  ejogo JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fikiri kwanza kabla hujaweka post yako hapa. Yaani umehamka asubuhi umeona maji yamejaa basi unawaza hapa lazima tatizo lipo kwa waandisi! Nadhani bwana Nyambala na Abdulhalim hapo juu wameshakueleza vizuri who plays what roles and where.
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 15,864
  Likes Received: 3,137
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Nchi hii maamuzi ya kihandisi yanaamuliwa kisiasa...........
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Dec 10, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  wanafikiri labda kila mhandisi anajenga mitaro
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,711
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  labda nikuulize swali ni nani aliyejenga barabara za posta maana kama kujengwa zimejengwa muda mrefu sana halafu kwani kila mhandisi anajenga mitaro ya barabara?
   
 12. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wahandisi mnajenga, kila siku majengo yanashuka nalo ni ukosefu wa fund? mitalo mnajenga chini ya kiwango kaangalie mbagara road just 2years, mnashindwa kushauri kipi kifanyike, kwani wizarani na tanroad hakuna wahandisi? bahari mita 100 maji yanasumbua karne nzima? hakuna uwezekano wa kuwa na trench kuuubwa underground kuelekea baharini from Kariokoo or somewhere ealse? acheni.
   
 13. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #13
  Dec 10, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na serikali yote inaongozwa na hao penye red
   
 14. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili ni jambo la aibu kweli hasa kwa hawa wanaojiita wahandisi wa wilaya. Posta hapa na baharini hata km 1 haifiki ni jana tu tumesheherekea miaka 49 ya uhuru lakini tumefanya nini hakionekani zaidi ya kuongeza vitambi. Rais na serikali yake yote iko hapa hapa na wao wanapita hapo hapo na wanayaona haya. Jana mti umeanguka pale Sokoine Drive umekaa hapo na leo mchna ndo wameuondoa. Hii inasikitisha hasa pale tunapoona kodi tulipazo ni kubwa na wamegoma kushusha. Sawa tutalipa ila tuone faida zake. Na c tuone ma Land Cruiser V8 kuanzia mawaziri mpaka mkuu wa wilaya. Tutaonana wabaya mwisho wa siku.
   
 15. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #15
  Dec 10, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Suala si kwamba barabara zimejengwa lini maana hata kama zimejengwa kitambo hawa waandisi wamefanya maboresho yapi? Pili ni kweli kwamba si kila mhandisi anajenga mitaro ila wahandisi wako chini ya ERB kazi ya bodi hii ni kuwawajibisha waandisi wanaofanya uzembe na kazi chini ya kiwango. Ni nani aliyewajibishwa kwa hilo.? Ndo maana twasema samaki wote wameoza. Maana kama wazalendo wangefanya jitihada za makusudi kuokoa jahazi.
   
 16. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #16
  Dec 10, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  siasa IMEINGIA KWENYE UTENDAJI WAKUU MBONA KILA MAHALI HOVYOOO!
   
 17. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #17
  Dec 10, 2010
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,968
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ivi mnapolaumu tu mmewapa kazi hawa jamaa wakashindwa au kazi ni kuita contractors kutoka ulaya kuja kufanya kazi zao na katika hali kushangaza huko vijijini kuna wahandisi hewa wengi wengine wanapewa kazi za ujenzi bila hata kuwa na taaluma hiyo yakitokea matattizo mnamlaumu nani tumeweka ten percent mbele kuliko kutimiza wajibu na kufanya kazi kwa ufanisi mtu anaangalia nikimpa kazi mtu fulani ntapata nini badala ya kuangalia ubora wa kazi itayofanywa nasikitika kwa sababu hatutaacha kulalamika mpaka tutakapoamua kubadili fikra zetu mbovu
   
 18. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #18
  Dec 10, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,904
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 180
  Abdulahim , asante sana kwa kumuelimisha huyu jamaa ambaye inelekea uelewa wake juu ya taaluma hii ya uhandisi na city management unamsumbua.
  Vizuri Mkuu rugumye aelewe kuwa uhandisi si kuibua vyoo as a hobby!!
  Jiji kama la Dar es salaam lina uongozi wake ambao umelala, wenyewe wanjiita City Fathers, na mtu wa kuwaamsha ni ninyi wananchi.
  Sita kushangaa mkuu rugumye ukijiuliza kwa nini wahandisi hawajengi barabara ya kwenda Zanzibar!!!
   
Loading...