Bongo Fleva ya zamani tulikuwa tunapewa story.. siku hizi tunapewa nini?

Nakumbuka muziki wa kizazi kipya wa nyumbani hapa Tanzania.. around miaka ya 99 mpk 2000 na kenda... Ilikuwa ukiskia muziki unahit, basi ni kwa sababu una story.. Yaani style ya uandishi na hata kuimba/kurap ilikuwa ni story-telling..

Unakuta msanii anaandika kuhusu mwenendo wa tabia za mtu fulani (fiction).. Ambaye labda alianza kuwa kijana mwema... akaharibikiwa... au mkasa fulani.. simulizi yake sasa ndio daah mpaka raha..

Nakumbuka story ya Barua.. Story ya Aseme.. Story ya Sister sister.. Story ya Jinsi Kijana... Story ya Boss.. Story ya salome... Ya leah.. Story story...

Style hiyo naikosa kwenye miziki ya awamu hii.. wimbo mmoja unakuta una story kibao ndani yake.. unakuta kiitikio tofauti kabisa na verses... ladha inakuwemo lakini haidumu... inachosha..

Shime wanamuziki.. tuushape muziki.. tuchanganye ikibidi... Nilimwona Jay Moe akifanya story telling hivi karibuni kwenye wimbo wake wa Story za watu 3... Ilikuwa poa sana..

Natamani siku zirudi nyuma.. Kama haiwezekani, basi wazee wenzangu humu tukumbushane mistari ya nymbo za zamani ambazo zina stories nzuri..
ule ndo ulikuwa mziki bana...saiv umavi mavi tu! bongo fleva imekuwa sijui km nini maana bora hata ya tarabu na boringo
 
Zama za wazee zimeisha..usijilazimishe kwenda na wakati ndio maana mmewekewa program zenu za zilipendwa..hizi ni zama za kuacha maneno na kuweka muziki...
Ha Ha Ha Ha Ha! Watu walishaga elimishwa Sana, saa hii hawataki tena hadithi... Wanataka burudani tuu kutoa stress, nchi yenyewe hii babu, ohooo flow Kali beat Kali ndo kitu imebaki watu watoe mastress man.
 
Mtoto wa geti Kali 1&2
asali wa moyo 1&2

Ulinikataa -Chief
Zali la mentari- jay
 
Yule afande mwenzangu wakamuuliza,
Umekuja peke yako au umekuja na mukaka wako,
Na wale wafungwa wengine wakawa wanashangilia mwali mwali mwali,
.....................................
Sijui nirudi chijijini,
Mimi sio polisi tena,

(Nimesahau mistari ya yule jamaa)
Imekaa vibaya
hii Bado haijatuliaa
imekaa vibayaaa
 
From
...NAULIZIA HUKO WAPI NINAKOKWENDAAA, SIJUII LINI NITAFIKAAAAAA...........!
to
.WAPO....! MASHOGA WAPO, WASAGAJI WAPO....!
This is pathetic.
 
Athuman-solid ground
jerry -solid ground
Baba jeni-solid ground

Jerry chorus
Kichaaa kimepanda(jerry)
baada ya kuvuta mineli..
wengi walidhani kalogwa na jirani...
kumbe mibange imempanda kichwani...

Baba jeni chorus
Baba jeni alipopata mafao
tabia tabia ikabadilika
na Sasa yamekumkuta
anabaki anajuta..

muziki wa Zamani mtamu sanaaa
 
Athuman-solid ground
jerry -solid ground
Baba jeni-solid ground

Jerry chorus
Kichaaa kimepanda(jerry)
baada ya kuvuta mineli..
wengi walidhani kalogwa na jirani...
kumbe mibange imempanda kichwani...

Baba jeni chorus
Baba jeni alipopata mafao
tabia tabia ikabadilika
na Sasa yamekumkuta
anabaki anajuta..

muziki wa Zamani mtamu sanaaa
Dah, kitu bush party! Aiseeee! Solid Ground Family.
 
MTU na pesa -Afande selle

Chorus
watu nazo pesa
watu nazo pesa
wewe zinakutesa
Mimi zinanitesa pesa
 
Kumbuka braza Kaka
Kati yangu na wewe hakuna aliyekamilika
kama kaoga ni usafi taulo lisinge chafuka..

baadhi ya mistari ya mayowe-Afande selle
 
Nakumbuka muziki wa kizazi kipya wa nyumbani hapa Tanzania.. around miaka ya 99 mpk 2000 na kenda... Ilikuwa ukiskia muziki unahit, basi ni kwa sababu una story.. Yaani style ya uandishi na hata kuimba/kurap ilikuwa ni story-telling..

Unakuta msanii anaandika kuhusu mwenendo wa tabia za mtu fulani (fiction).. Ambaye labda alianza kuwa kijana mwema... akaharibikiwa... au mkasa fulani.. simulizi yake sasa ndio daah mpaka raha..

Nakumbuka story ya Barua.. Story ya Aseme.. Story ya Sister sister.. Story ya Jinsi Kijana... Story ya Boss.. Story ya salome... Ya leah.. Story story...

Style hiyo naikosa kwenye miziki ya awamu hii.. wimbo mmoja unakuta una story kibao ndani yake.. unakuta kiitikio tofauti kabisa na verses... ladha inakuwemo lakini haidumu... inachosha..

Shime wanamuziki.. tuushape muziki.. tuchanganye ikibidi... Nilimwona Jay Moe akifanya story telling hivi karibuni kwenye wimbo wake wa Story za watu 3... Ilikuwa poa sana..

Natamani siku zirudi nyuma.. Kama haiwezekani, basi wazee wenzangu humu tukumbushane mistari ya nymbo za zamani ambazo zina stories nzuri..
Nafikiri ndiyo maana yule msanii ameimba 'naomba unisaidie kushea' ..pengine alimaanisha hivi ili watu waujue mziki wa enzi zile...
bila shaka umemsaidia kushea...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom