Bongo Dar es salaam, inafundisha jamii au inapotosha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo Dar es salaam, inafundisha jamii au inapotosha?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kashaija, May 27, 2009.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya ndugu zangu, kuna huu mchezo unaoitwa Bongo Dar es salaam unaorushwa na TBC ambao main actor anaitwa Dude. Je, mchezo huu unafundisha au Unabomoa? Kwa nini?

  Binafsi naona unabomoa maadili yetu, maana unatoa mbinu mbalimbali ambazo wahalifu wanaweza kuzitumia katika kuhujumu jamii.
   
 2. Blackmamba

  Blackmamba Member

  #2
  May 27, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchezo huo nadhani unawafungua macho wananchi wajhadhari na mbinu zinazotumiwa na wezi ambao wasanii hao wanzianika hadharani ili kuumbua wezi hao. Si mbinu ambazo wasanii wanazibuni, bali ni marudio ya mbinu za wezi ambazo zilikwishatumika eneo moja/fulani ambalo wananchi hawalijui kwa hiyo kazi ya wasanii hao ni kuiambia jamii nzima ielewe kuhusu mbinu hizo kuweza kutumika muda wowote
   
 3. Kiteitei

  Kiteitei JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2009
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 1,257
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  mi nadhani si vibaya pia hizi mbinu zikijulikana ili pia tuwe tayari kukabiliana nazo inapotutokea, licha ya mchezo huu kuna movies na vitabu viingi tu ambavyo vinaonyesha mbinu za kihalifu, nakumbuka miaka ya nyuma nilikuwa mpenzi mno wa chase( James Hardley) kutokana navyo na nilikuwa natamani kuwa jambazi jambazi hivi...
   
 4. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ni kweli lakini tatizo wajitahidi jinsi ya kumalizia mchezo..tapeli kwenye jamii hatakiwi kuonekana shujaa...
   
 5. M

  Msindima JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kwa upande mwingine unafundisha na kwa upande mwingine naona unatoa mbinu za kujifunza utapeli

  Nikianza na kufundisha,unatusababisha tuwe makini na watu ambao wanaonekana kuwa wanataka kutusaidia kupata vibali mbalimbali na kumbe lengo lao si hilo ili ni kutuliza,na pia unatufundisha kuwa makini na mbinu wanazotumia matapeli katika kututapeli iwe pesa,magari na vitu mbalimbali.

  kwa upande huo mwingine kwa kweli naona mmhh no unawapa watu wengine mbinu mbadala za kuingia katika hio ajira,maana mwingine atakapoangalia anaweza kujikuta kutamani kufanya hivyo na anaweza kuamua kuweka hilo katika vitendo,mfano waweza kuta mtu labda amesota mtaani kwa muda mrefu anaweza shawishika na kuona kuwa hiyo ni ajira inayolipa zaidi na hivyo kuamua kuingia katika hiyo ajira.
   
 6. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Duuh ina maana hayo matamanio uliyaacha kwa kusoma nini???
   
 7. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0  Hapa ndipo nasema kwamba mchezo huu unapotosha, maana kwa kipindi hiki ambacho shilingi imeota mataili, ni rahisi watu kuiga mbinu mbalimbali kutokana na mchezo huu na kisha kufanya hayohayo kwenye jamii.
   
 8. K

  Kamuna JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 297
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  That is an eye opener which instill sensitivity to people on being watchful!In my opinion the question should have been-what needs to be rectified for a better impact to the society?
   
 9. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #9
  Sep 14, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Television ya serikali ya TBC imekuwa ikirusha kipindi cha maigizo kiitwacho BONGO DAR ES SALAAM Kipindi hili kimekuwa kiki-u-promote na ku-brand jiji la Dar es salaam kama jiji lililo la matapeli ambalo kila mtu ajaye huko dare s salaam kutoka nje ya Dar es salaam ajitahadhari na atumie ubongo wake maana kuna matapeli kila kona.

  Kipindi hicho huanza na kumalizia kwa wimbo wa kuwaonya watu waingiao dare s salaam wajihadhali .

  Ieleweke kuwa watu toka enzi za mwarabu walihangaika sana kuli-market jiji la Dar es salaam ili lionekane jiji bora sana duniani.Hata jina wakaamua waarabu kuliita DAR ES SALAAM yaani Bandari salama ili ku-pabrand vizuri kisoko duniani.Brand name hiyo waliipigania hadi ikaingia katika ramani ya dunia kama jina rasmi la jiji hilo.

  Bodi ya utalii nayo ikaja na brand name nzuri zaidi nyepesi nay a kueleweka ya kutangaza Jiji hilo kama “HAVEN OF PEACE” na kujitahidi kusambaza hiyo slogan kila kona duniani ieleweke hivyo ili kuvutia watu toka nje ya Dar es salaam waendapo jijini walijue jiji hivyo.

  Sasa wahuni wametokea kuua Brand name iliyojengwa kwa mamia ya miaka kwa makusudi mazima wameingia na kuruhusiwa na wahuni wenzao ndani ya TBC kurusha kipindi kinachoua brand name ya jiji iliyojengwa kwa miaka mingi na kulionyesha jiji la Dar es salaam kuwa brand name yake si HAVEN OF PEACE bali jiji la matapeli kila kona.

  Kinachoniuma ni kuwa kampeni hii ya kuua international brand name ya Jiji la Dar es salaam inaendeshwa na TBC chombo ambacho ni cha serikali ambacho kinatakiwa mojawapo ya kazi zake iwe ni ku-promote brand names nzuri za majiji na miji ya Tanzania kwa wageni’
  Ieleweke kuwa kipindi hiki kinaonekana sehemu nyingi duniani sababu TBC inafika sehemu nyingi kupitia satellite kwa hiyo uchafuzi huo unafika ,mbali.

  Hivi huyo producer wa Hicho kipindi ni nani hasa? Ni mtanzania? Ni Mwarabu? Ni mhindi? Ni chotara?Ni nani hasa? Na ana lengo gani? Je ni mchezo tu au kuna something behind the scene? Na ni nani kamruhusu kuingia TBC? Hivi halmashauri ya JIji la Dar es salaam hawana maafisa masoko au biashara wanaoweza kujua hayo na kuipiga marufuku TBC isiendelee kuchafua brand name ya jiji? Hivi mkuu wa mkoa kazi yake ni nini kama hawezi kulinda brand name ya jiji lake kazi zake hasa ni nini? Ni kwenda kupokea viongozi wa kitaifa Airport na kwenda kula pilau kwenye dhifa za kitaifa ikulu?

  Hivi kuua brand name ya jiji iliyojengwa kwa karne nyingi ni sahihi wewe TIDO MHANDO mkurugenzi wa TBC.Upo hapo dare s salaam kusimamia maslahi ya nani kama huwezi hata kulinda brand name ya jiji linalokuweka mjini na unakubali ku-lounge campaign ya kuua brand name ya jiji? Futa haraka hicho kipindi kwenye programu za TBC

   
 10. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu
  Usishangae mwongozaji wa Bongo Dar es Salaam akishindwa kuelewa hoja yako ya kulinda maslahi ya jina Dar es Salaam. Kama elimu ya mwongozaji wa kipindi hicho haijazidi darasa la saba, utaendelea kuhoji? Hapa simaanishi mkurungenzi (Tido) bali mwongozaji wa kipindi
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  On the one hand, hatutaki TBC ifanye an overly self defeating campaign about Dar.

  On the other hand, we also do not want a government propaganda that all is hunky-dory in Dar.

  Just give us the news and facts.
   
 12. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2009
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Point nzito sana mkuu. Ukijua nani anawapa pesa za kutengeneza hivyo vipindi, utashangaa
   
 13. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  waendelee ni mchezo mzuri sana!! wajaribu kuwa husisha na wasa nii wengine kama wakina sisi-!! wasibuni sana wajaribu kurudia visa vya kweli!!

  Napenda kuwashauri wa ache ubinafsi!! wakumbuke kwamba Itakua ni busara kama waki wasiliana na Profesa J zamani kama Nigger J wautumie wimbo wake ...

  Mimi nina amini wimbo wa J ndio chanzo fulani cha ubunifu wa kipindi hicho!!
   
 14. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo we unapenda ndugu zetu kutoka mikoani waendelee kutapeliwa tu kisa Brand ya Jiji? maana kama mtu ametapeliwa hahao wabongo wanabaki kumcheka kua mshamba wa Galilongwa huyooo....karibu hii ndo Bongo!! so mi naona kipindi kiendelee ili kiwaabarishe ndugu zetu!!
   
 15. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ni kweli suala la elimu ni muhimu katika kazi kama hii. Pamoja na ukweli huo, bado nafikiri muongozaji anajitahidi kufikisha malengo...mimi binafsi na elimu yangu ya digrii pamoja na kuzaliwa na kukulia bongo nimeshawahi kuingizwa mjini mara nyingi tena wakati mwingine kama ningeshtuliwa kidogo kama kinavyofanya kipindi hiki nisingeuvaa mkenge wa kuuziwa kipande cha sabuni badala ya simu.

  Imefika wakati tuwe wa kweli...matapeli dar ni kama wali kwa maharage na siku zote huibuka mashujaa na wanambinu nyingi za kukwepa mkono wa sheria. Kuna wakati hushirikiana hata na maaskari. Kwahiyo ukitaka maoni yangu yasiyo na chembe ya unafiki, JAMAA WANAFANYA KAZI NZURI NA HAKUNA HAJA YA KUJIVUNIA KITU KISICHO CHA KWELI.
   
Loading...