Bondia Mtanzania, Hassan Mwakinyo(23) amchakaza mzungu

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
21,770
39,556
Niko hapa London naangalia TV channel ya Sky action bondia kutoka Bongo anaitwa Hassan Mwakiyo amemchapa vibaya sana bondia Sam Eggington katika round ya pili. Kwa jinsi navyomwona anaweza kufika mbali na akachukua mikanda inayotambulika na yenye heshima duniani.

Ic1wN7yvSWWjrrZ43n1P_brum31.JPG

========

BONDIA Hassan Mwakinyo wa Tanzania jana amefanikiwa kushinda kwa Technical Knockout (TKO) sekunde ya 45 raundi ya pili dhidi ya Muingereza, Sam Eggington Uwanja wa Arena Birmingham, zamani Barclaycard Arena mjini Birmingham, England.

Katika pambano hilo lisilo la ubingwa uzito wa Light Middle, Mwakinyo alimzidi kabisa mpinzani wake tangu mwanzo kabla ya kummaliza katika raundi ya pili kuelekea pambano kuu jana kati ya Muingereza, Amir Khan na Samuel Vargas Colombia anayeishi Canada.

Khan aliyeshinda kwa pointi za majaji wote, alimuangusha Vargas mwanzoni mwa raundi ya pili, naye akaangushwa mwishoni mwa raundi hiyo wote waliinuka haraka kuendelea hadi kumaliza raundi.

Khan aliyemuangusha Vargas na raundi ya tatu pia pamoja na kumjeruhi pua, kwa ushindi huo anaweza kupigana na Manny Pacquiao au Kell Brook.

Na Mwakinyo baaada ya ushindi huo wa jana atapanda tena ulingoni Oktoba 20, kuzipiga na mwenyeji Wanik Awdijan ukumbi wa Alex Sportcentrum mjini Nuremberg, Ujerumani katika pambano la kuwania taji la vijana la IBF uzito wa Middle.

Pambano la jana lilikuwa la tatu Mwakinyo anapoigana nje ya Tanzania akiwashinda kwa mara ya pili baada ya kumshinda pia kwa TKO Anthony Jarmann wa Namibia Agosti 8, mwaka jana ukumbi wa Grand Palm Hotel mjini Gaborone nchini Botswana.
Desemba 2, mwaka jana Mwakinyo alipoteza kwa pointi mbele ya mwenyeji, Lendrush Akopian ukumbi wa Krylia Sovetov mjini Moscow, Urusi.
 
Bora huyo kuna mmoja alidhalilisha juzi kwese sport huko Afrika ya kusini. Alikuwa na mashabiki wengi sana wazauz wanaimba hapa kazi tu lakini alikula makonde ya hatari mpaka akagoma kuendelea
 
Bora huyo kuna mmoja alidhalilisha juzi kwese sport huko Afrika ya kusini. Alikuwa na mashabiki wengi sana wazauz wanaimba hapa kazi tu lakini alikula makonde ya hatari mpaka akagoma kuendelea
Aisee huyu ni namba nyingine. Hata pigano analopigana siyo la uchochoni. Main event ni kati ya Amir Khan vs Samuel Vargas. Na ana miaka 23 tu. Watangazaji nguli wa Sky wamemsifu sana.
 
Aisee huyu ni namba nyingine. Hata pigano analopigana siyo la uchochoni. Main event ni kati ya Amir Khan vs Samuel Vargas. Na ana miaka 23 tu. Watangazaji nguli wa Sky wamemsifu sana.
Nashangaa sana TBC2 inapiga tuu mamiziki siku nzima, nani aliwaambia tunahitaji miziki? walitakiwa wawe wanafuatilia wanamichezo wetu wa michezo mabalimbali wanakokwenda kucheza watuonyeshe. Ona sasa hata hawajawaabarisha watanzania,na yawezekana wewe ndio mtanzania pekee aliyeshuhudia pigano hili
 
akirudi keko malaya lazima wa mmalize. kuna mmoja huku katamba sana miaka 2000 anatoka familia ya ngumi maarufu anafugwa na jimama anagongea hadi fegi akipata meneja huko atatoboa. karama nyirawila alikuwa hata akitembea kichwa kinacheza kama anakwepa ngumi bondia pekee tanzania anashezesha shingo kama nyoka huku akienda mbele kumfata mpinzani huku akikwepa nae chaliii. wanawake keko wanaua vipaji
 
Uliposema mikanda ya Matumla ni ya vichochoroni hapo umeikosea adabu boxing na Matumla mwenyewe, na unaonyesha hujui boxing. Tumpongeza Mwankiyo bila kuwadharau wengine.
Naandika nilicho na uahakika nacho kwa 100% bob! Mashirikisho ya ndoni yenye hadhi duniani ni WBA, IBF, WBO na WBC. Bondia kuchukua mkanda wa uzito wa haya mashirikisho ni ngumu sana. Na ndiyo yanayoongoza. Mengine yaliyobakia ni ya uchochoroni na mabondia wanaojielewa hawahangaiki na mikanda yao. Japokuwa huyu Hassan alipigana kama undercard na hajachukua mkanda wowote lakini pambano lake hakulifanyia uchochoroni kama kina Matumla. Ameweza kuonekana live kwenye channel maarufu kama sky! Sidhani kama kuna bondia wa kulipwa ambaye ameshafikia hatua kama hii.
 
Kweli mkuu ndiyo maana walikuwa wanapigana na vinyozi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom