Bondia Aliyekamatwa na Madawa ya Kulevya Mauritius Arejea Nchini

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
BONDIA Emillian Patrick aliyekamatwa nchini Mauritius Juni, 2008 kwa tuhuma za kuingiza dawa ya kulevya aina ya heroin zenye thamani ya shilingi milioni 600 amerejea nchini kuungana na familia yake.
Taarifa za uhakika ambazo timu ya Nifahamishe.com imezipata bondia huyo alirejea nchini mwishoni mwa wiki na mara alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere alishikiliwa na maofisa Uhamiaji na wale wa kitengo cha kuzuia dawa za kulevya.

Na baadaye, alitoa maelezo yake kwenye kitengo cha kuzuia dawa za kulevya ambako aliachiwa kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na ndugu zake.

Patrick alikamatwa akiwa na bondia mwenzake Petro Mtagwa na kocha wao Nassor Michael hotelini wakati walipokuwa nchini humo kushiriki mashindano maalum ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki iliyofanyika China.

Wakati huo, tayari Patrick ambaye anapigana kwenye uzito wa bantam (kilo 54) alikuwa amefuzu kwa michezo hiyo na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania baada ya kupata medali ya fedha nchini Namibia, lakini kwa vile alikuwa mahabusu hakuweza kwenda China kuiwakilisha Tanzania.

Hata hivyo, hatima ya Nassor na Mtagwa bado haijajulikana na wanaaendelea kushikiliwa na mamlaka za dola za nchini Mauritius.

Alipotafutwa kwa njia ya simu, Patrick aligoma kuzungumza na mwandishi wetu lakini pia akikacha kupokea simu zozote kutoka kwa watu asiowajua.

Wakati wa sakata la kukamatwa kwao, timu hiyo ya Tanzania iliunganishwa na watu wengine watatu ambao hawakuwa mabondia, lakini walionekana kuwemo kwenye orodha ya timu na kujitambulisha kama viongozi waliomo kwenye msafara huo.

Kutokana na kashfa hiyo, timu ya ngumi ya Tanzania ilitimuliwa kushiriki michuano hiyo ya Mauritius.

Baada ya kukamatwa kwa mabondia hao, walisomewa mashtaka yao katika mahakama ya Mahébourg kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya.

Kutokana na kukamatwa kwao, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania, Shaaban Mintanga, alikamatwa jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa mahakamani kusomewa mashtaka ambayo yalikuwa yakilingana na yale waliyosmewa mabondia huko Mauritius. Kesi yake bado inaunguruma.

Lakini pia, Tanzania ilisimamishwa uanachama wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa, ABC, kabla ya kurejeshwa baada ya kamati nzima ya utendaji iliyokuwa chini ya Mwintanga kujiuzulu kupisha uchaguzi mkuu kufanyika na kumwingiza madarakani Joan Minja.
source nifahamishe.com
 
Back
Top Bottom