Bonde la Mto Msimbazi Lafurika-Polisi wahaha Kuokoa Maisha ya Wavuja Jasho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bonde la Mto Msimbazi Lafurika-Polisi wahaha Kuokoa Maisha ya Wavuja Jasho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by spencer, Dec 20, 2011.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreatThinkers,

  Leo Alhamis 22/12/2011 mvua imeanza tena kunyesha, serikali bado inakigugumizi ya nini kifanyike juu ya hawa waathirika.
  Inaamini kuwaambia marufuku kurudi kwenye hayo makazi ni uamuzi mgumu!!!

  Hadi sasa watu 18 wameshakufa, maiti nyingine imeokotwa baharini. Mawasiliano kati ya Kinyerezi na Banana yamekatika tangu jana.
  Segerea na Stakishari daraja lililowekwa na wanajeshi baada ya mvua kubwa ya Elnino nalo limekaa upande. Ukija matumbi sehemu ambayo magodown ya wahindi yameziba bonde jana maji yalivunja kuta na kusukuma makontena kama manne hadi ktk barabara ya Mandela njia ikazibwa ikabaki upande mmoja, Serikali bado ina kigugumizi ktk hili pia!

  Jamani waafrika tumerogwa na nani?
  kwa nini tunashindwa kujisimamia?
  Kuna haja gani ya kuwa taasisi za mipango miji?
  Je wameshindwa hata kuweka nguzo kuonesha End of valley reserve, Kwa nini TANROAD wameweza nchi nzima?

  Au walioko madarakani kazi imewashinda?

  Leo Jumanne, 20/12/2011

  Hali ni tete ktk Bonde la Msimbazi daraja la Segerea maji yanapitia Pomoni tokea Pugu na Kinyerezi,Njoo hadi vingunguti hali ni Mbaya sana. Kigogo Polisi wapo kule wanajaribu kuokoa wananchi?

  2006/7 kulikuwa na Elnino hayo majumba yaliyopo bonde la msimbazi hayakuwepo mengi kama sasa muulize Mzee Makamba ex-Mkuu wa Mkoa wa Dar.
  Tulipata fundisho gani uongozi wa mkoa/taifa ulijifunza, hii mvua iliyokesha inanyesha usiku wa kuamkia leo ni kama tano ktk mia ya Elnino tuliyoshuhudia mwaka ule
  Ndg. wana Dar Es Salaam mnaoaminika kunywa maji ya Bendera mnadhani CCeM inathamini tena mtu mlalahoi?
  Kama wana nia njema nanyi na hawataki kesho baadhi ya miili ikaokotwe baharini kwa nini wanawaruhusu kujenga?
  Je mmewahi kwenda TANESCO kuomba kuunganishiwa huduma mkaambiwa kule ni bondeni hawaweki? Maji Je?
  Je serikali inamchoro wowote uliosambazwa kwa wanamitaa jirani na bonde kuwaarifu waishie wapi kujenga makazi hayo yanayoitwa holela?
  Mfano. Pale Matumbi ukitokea Buguruni kuna matajiri wameziba bonde kwa Kujaza vifusi na kujenga kuta kubwa na kuweka viwanda serikali iko wapi? au ndiyo Umbwe(vacuum) la Uongozi linalosemwa kwa lipo kwa sasa?
  Yangu ni hayo ila maafa yapo.
   
 2. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,825
  Likes Received: 924
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni hili hili mipango miji na linakua na litadumu miaka yote watu watakua wanakufa kwasababu ya uzembe tu wa mamlaka na kusimamia mipango miji na kudhibiti ujenzi holela...tunabadilisha maisha kuwa sadaka hawa watu wangeondolewa kwa mara moja yakaisha...mvua haziishi leo wala kesho tena kuna mabadilko ya tabia nchi manake mvua zitakua zinakuja za kutisha..
   
 3. Imany John

  Imany John Verified User

  #3
  Dec 20, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  pia star tv wapo live mda huu
   
 4. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #4
  Dec 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Maji yanarudi katika sehemu yake masikini!! raia wakawaida alipaswa kupewa elimu ya kujilinda na hili lakini hawakupewa pia wakaachiwa kujenga! sasa leo maji yanarudi katika asili yake ya mwanzo yanaleta madhara kwetu! poleni sana na wala si kazi ya Mungu!! ni makosa yetu!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,414
  Likes Received: 19,726
  Trophy Points: 280
  kuna mzee kasombwa na maji kigogo kwenye bonde hili
   
 6. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Uko wapi mama Tibaijuka professa uliyekimbia taaluma yako ukakimbilia siasa?

  Nimepita jangwani pale Kajima, kama maji yasingevunja ukuta na kuingia kwenye hilo godown maji yangevuka daraja!

  Wacha twende kijijini Christmas 0 tupumzike kidogo hali ya joto la hapa Dar.
   
 7. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Msasani kwa Mwalimu all the way mpaka Shoppers Plaza wameamua kuweka mitumbwi kabisa ...

  Kawe beach almost ipo kwenye dimbwi ...

  Barabara ya Africana ni Mtaro wa maji ...

  Dar es Salaam kuna VITUKO ... Na mvua huwa inaleta VITUKO zaidi... Khaa!!
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Dec 20, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na watu wamepata leo nafasi ya kufungulia vyoo vyao...vinyesi vinasafiri toka hukouswahili hadi baharini.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Dec 20, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh....nisameheni tu. Bongo Nyu Yoki.

  Prezidaa,
  Safarini kuelekea Pyongyang.
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siku nyingine uweke picha za matukio
   
 11. MUREFU

  MUREFU JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,230
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  sasa polisi ndo wamekuwa waokoaji haya kazi kweli kweli sasa huko ni msimbazi na JANGWANI patakuaje jamani mana kha
   
 12. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #12
  Dec 20, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  nchi imekwama hii hamjajua tu mpaka leo? shauri yenu endeleeni kupoteza muda kulalamika
   
 13. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #13
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  N kule mabibo hapaendeki! nimeshuhudia wanafamilia wakizoa maji ndani. Yaani kupata maji ni shida mpaka wakayachote mbali na nyumbani, sasa yameamua kuingia kabisa kwa makazi ya watu!
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Dec 20, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,462
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  Kaongeza foleni huku Tegeta.....anaenda Bagamoyo huku akisindikizwa kwa Helikopta sijui kwa nini hakupand hiyo kitu
   
 15. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #15
  Dec 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Anataka kusalimiana na wananchi wake.
   
 16. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #16
  Dec 20, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Mvua ikinyesha tabu, jua likiwaka tabu!
  Ingewezekana kuhama nchi mtu unahama.Tatizo utahama vp uache ndugu zako wakiteseka?
   
 17. K

  Kikambala Senior Member

  #17
  Dec 20, 2011
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hamia airtel
   
 18. Mrbwire

  Mrbwire Senior Member

  #18
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 197
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kikambala we noma!
   
 19. u

  utantambua JF-Expert Member

  #19
  Dec 20, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimepita sasa hivi hapo jangwani aisee watu wapo barabarani kama vile wanasubiri daladala kumbe wamekimbia nyumba zao zilizofurika. Lakini cha kustaajabisha watarudi tena bahari hii ya maji ikiondoka
   
 20. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #20
  Dec 20, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Watanzania kwa ubishi.....waliambiwa toka enzi za Makamba wahame jangwani wakabisha
   
Loading...