Bonde la kilombero liko hataiani kupoteza kabisa uasilia wake

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,233
KILOMBERO: Kutoka mito 79 hadi 39 ya sasa, kulikoni?

Johnson Mbwambo
Novemba 24, 2010
‘Climate Change’, wafugaji Wasukuma balaa tupu
Aina 20 za samaki zatoweka, wanyamapori wapungua
HAPO kale, Bonde la Mto Kilombero ambalo lipo katika wilaya za Ulanga na Kilombero, mkoani Morogoro, lilikuwa moja ya vivutio vikubwa vya sayari yetu hii. Vivutio vyake vilivuma hadi nje ya nchi kiasi hata cha kusababisha bonde hilo kuingizwa katika orodha ya maeneo ya dunia yanayolindwa na Ramsar; yaani ule mkataba wa kimataifa unaolenga kuhifadhi ardhioevu (wetlands) muhimu duniani.
Sifa zake zilikuwa nyingi: Bonde la Kilombero lilikuwa na mtandao wa mito zaidi ya 79 iliyokuwa ikititirisha maji misimu yote ya mwaka ambapo mito ya Luhuji, Mnyera, Furua, Mpanga, Kihanzi, Luipa, na Ruaha Mkuu huungana na Mto Kilombero na kuwa Mto Rufiji.
Si hivyo tu. Bonde la Mto Kilombero lilikuwa ndiyo makazi ya asilimia 75 ya wanyamapori aina ya Sheshe duniani. Aidha, ndiko pekee duniani vilikopatikana baadhi ya viumbe hai duniani kama vile vyura wa njano wa Kihantsi au Mbega Wekundu wa Udzungwa.
Mbali ya hayo, Bonde la Mto Kilombero lilikuwa ndilo pekee nchini ambako unaweza kupata aina nyingi zaidi za samaki (takriban 40) kuanzia kambale na perege wanaopatikana sehemu nyingi nchini hadi Kapatwa, Ndungu, Ningu nk ambao hupatikana sehemu chache tu.
Hivyo ndivyo Bonde la Kilombero lilivyokuwa angalau miaka 30 iliyopita; lakini katika ziara ya hivi karibuni ya waandishi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), ilibainika kwamba bonde hilo limepoteza baadhi ya vivutio vyake hivyo, na hatua zisipochukuliwa haraka vivutio vilivyosalia navyo vitatoweka kwa kasi.
Kwa mfano, taarifa zilizopatikana kutoka Idara ya Maliasili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mjini Ifakara, zinaonyesha kwamba mito ambayo hutiririsha maji mwaka mzima sasa imebakia 39 tu katika bonde zima kutoka idadi ya mwanzo ya mito 79.
Aina za samaki nazo zimepungua kutoka 40 za mwanzo hadi 20 za sasa. Angalau wenyeji katika vijiji kadhaa vya wilaya ya Kilombero ambavyo ujumbe huo wa JET ulivitembelea, wamethibitisha kwamba samaki aina ya Kapatwa ametoweka kabisa katika bonde hilo. Aina nyingine ya samaki ambao wamepungua sana na wapo katika hatari ya kutoweka kabisa ni Ndungu, Mjongwa, Ningu na Mdelwa (golden fish).
Hata kwa wanyamapori hadithi ni hiyo hiyo. Wenyeji wa vijiji vya wilaya hiyo walieleza kwamba sasa ni taabu mno kumuona mnyama anayeitwa Mbega katika mapori yao wakati ambapo zamani walikuwa wengi mno.
Je nini kimetokea? Ilikuaje Bonde la Kilombero ambalo lilikuwa na mito 79 inayotiririsha maji mwaka mzima libakie na mito ya namna hiyo 39 tu? Ilikuaje mpaka wanyama kama Mbega na samaki kama Kapatwa sasa wawe ni historia katika Bonde la Mto Kilombero?
Kuna mambo mengi yanayoweza kutajwa yaliyosababisha hali hiyo hasi, lakini yote yanaweza kujumuishwa katika jambo moja kubwa; nalo ni uharibifu wa mazingira unaoendelea kwa kasi katika bonde hilo - uharibifu ambao athari zake zimekuwa ni maradufu kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi (climate change) yanayoisumbua dunia nzima.
Japo Bonde la Mto Kilombero liliorodheshwa rasmi kuwa eneo la Ramsar (Ramsar site) tangu Aprili 26, 2002 na kuanzia muda huo Ubelgiji imekuwa ikifadhili mradi wa Ramsar kwenye bonde hilo kupitia Halmashauri za wilaya ya Ulanga na Kilombero, bado kasi ya uharibifu wa mazingira katika bonde hilo inafifisha mafanikio ya mradi huo.
Ni kweli kwamba, kupitia mradi huo wa Ramsar unaofadhiliwa na Ubelgiji katika bonde hilo, wanavijiji wengi wamepatiwa elimu ya mazingira na hata kusaidiwa kuanzisha kamati za mazingira.
Ni kweli pia kwamba chini ya mradi huo vimeanzishwa hata vikundi vya maskauti wa vijiji (VGS – Village Game Scouts) ili kupambana na waharibifu wa mazingira na majangili, lakini mafanikio bado hayaridhishi, na hivyo kazi iliyopo mbele bado ni kubwa.
Lakini pengine kinachokatisha tamaa zaidi ni kwamba wakati mradi wa Ramsar ukijaribu kuliokoa bonde hilo, Serikali imekaribisha ‘tatizo jipya’ katika bonde hilo; tatizo ambalo, kwa sasa, ndilo linalochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika bonde hilo. ‘Tatizo jipya’ linalozungumziwa hapa ni uvamizi wa wafugaji wa Kisukuma katika Bonde la Mto Kilombero.
JET ilijionea katika ziara hiyo namna vyanzo mbalimbali vya maji vilivyoharibiwa na wafugaji hao wa Kisukuma ambao wamevamia bonde hilo na maelfu ya mifugo yao wakitokea Ihefu (Mbarali) ambako walitimuliwa na serikali mwaka 2006 baada ya kuiharibu pia ardhioevu hiyo.
Wafugaji hao wa Kisukuma ambao kwa desturi na tabia zao chafu si rafiki wa mazingira, wamekata miti katika mapori mengi na kuweka maskani yao katika vyanzo vingi vya maji katika Bonde la Kilombero.
Kwa hakika, wamekuwa ndiyo kero kubwa katika vijiji vingi ambavyo JET ilitembelea wakati wa ziara hiyo.
“Hebu wafikishieni salamu wakubwa serikalini huko Dar es Salaam: Wasipochukua hatua ya kuwafukuza wafugaji hawa wa Kisukuma, vyanzo vyote vya maji vitatoweka, na hata Mto Kilombero hautakuwa na maji mengi. Na hata lile pantoni waliloweka kwenye kivuko kile cha Ifakara halitaweza kufanya kazi kwa sababu ya kina cha maji kupungua”, ndivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mofu, Alvinuis Linus Ngwila alivyouambia ujumbe huo wa JET kwa uchungu mkubwa.
Je; wanavijiji wa Mofu, wilayani Kolombero, wanafanya nini kutetea maeneo yao yasiharibiwe na wafugaji hao wa Kisukuma; maana wao ndiyo waathirika wa kwanza wa kuharibka kwa bonde hilo?
Ngwila anacheka kwanza kabla ya kulijibu swali hilo: “Wanavijiji waliwahi kuwakamata wafugaji wa Kisukuma waliowakuta wakikata miti, lakini walipowafikisha kwa mamlaka husika za serikali, wanavijiji wakageuziwa kibao na kushitakiwa wao badala ya wafugaji wale waliowakamata.”
Kwa mujibu wa Ngwila, kuanzia hapo wanavijiji walipoteza morali ya kupambana na wafugaji hao wa Kisukuma. “Na sasa wanaendelea kuharibu vyanzo vya maji na kukata miti katika misitu watakavyo”, anasema mwenyekiti huyo wa kijiji.
Alipoulizwa iwapo mbunge wao wa zamani aliwasaidia lolote katika mapambano hayo dhidi ya wafugaji hao, Ngwila alimaka: “Mbunge?! Mbunge alifika hapa kijijini mara mbili tu – mara ya kwanza kukampeni na mara ya pili kushukuru baada ya kuchaguliwa. Baada ya hapo hatukumuona tena.”
JET ilithibitisha kwamba mahusiano kati ya wanavijiji hao wa Mofu na wafugaji hao wa Kisukuma, ni kama bomu linalosubiri kulipuka. Ni katika kijiji hicho ambako kuna mwanakijiji mmoja ambaye sasa ni kipofu baada ya kuondolewa macho na wafugaji wa Kisukuma aliojaribu kupambana nao alipowakuta wakilisha mifugo kwenye shamba lake.
Katika vijiji vingine vya Njage, Mngeta, Mchombe, Merera na hata mji mdogo wa Mlimba, kidole cha uharibifu wa mazingira kilielekezwa kwa hao hao wafugaji wa Kisukuma waliotimuliwa kutoka Mbarali (Ihefu).
Katika kijiji cha Njagi, mjumbe wa Serikali ya kijiji, Abdallah Iporah, anakiri kwamba mabadiliko ya tabianchi yamechangia mno kuvisambaratisha vivutio vya Bonde la Kilombero. “Zamani hapa tulikuwa tukipata mvua karibu kila mwezi, lakini sasa hatuna tena uhakika wa mvua. Kuanzia Mei hatujapata mvua hata mara moja. Tulipanda mahindi lakini yamekauka.”
Lakini pamoja na mabadiliko ya tabianchi, mzee huyo bado anaelekeza kidole chake kwa wafugaji wa Kisukuma kwamba wanachangia zaidi katika kuyafanya maisha yao wote kuwa magumu zaidi.
“Wamevamia maeneo yetu kwa mamia. Kwanza anakuja mmoja na anawasilisha maombi ya kuishi kijijini kwa serikali ya kijiji. Akishakubaliwa anakaa kama wiki moja tu na kuondoka kwenda kuchukua ng’ombe wake kibao. Baada ya muda anamwita mwenzake na mwenzake naye anamwita mwenzake. Na wote hao kila mmoja ana wake si chini ya wanne na watoto kibao na ng’ombe kibao. Baada ya muda wanavivamia vyanzo vya maji na mifugo yao, na hakuna tena wa kuwaambia “ondokeni”. Wanakuwa wakali na wako tayari kuua”, anasema mzee huyo.
Uharibifu huo wa mazingira na vyanzo vya maji unaofanywa na wafugaji hao wa Kisukuma ukichangiwa na mabadiliko ya tabianchi, vimeyafanya maisha ya wanavijiji wengi katika Bonde la Kilombero yawe magumu zaidi.
Otwin Mafui ni Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Merera. Anasema: “Zamani samaki walikuwa bwerere. Kikombe kikubwa kilichojazwa samaki wadogo wabichi ulikuwa ukikipata kwa Sh. 200 tu, lakini sasa kwa kiasi hicho hicho cha pesa unapata samaki mmoja tu. Mwaka 2003/2004 kambale mmoja alikuwa anauzwa Sh. 1,000, sasa ni kati ya Sh. 5,000 na Sh. 10,000.”
Kwa nini samaki wamepungua katika kijiji chake? Jibu lake ni kwamba maeneo mengi ya ardhioevu ambako walikuwa wakipatikana kwa wingi yamekauka kabisa, na pia samaki wamekimbia katika baadhi ya mito kwa sababu ya kupungua vina vya maji na kuharibiwa kwa maeneo ya mazalio yao.
Mvuvi Alex Ndalala alifikia hatua ya kuutajia haraka haraka ujumbe huo wa JET majina ya mito ya maeneo yao ambayo imekauka. “Mto Mkusi umekauka, Mto Mpakaka umekauka, Mto Nagakuru umekauka, Mto Mkula umekauka... na bwawa la asili la Mhoma nalo ikifika mwezi wa nane tu limekauka. Sasa unadhani hizo samaki zitatoka wapi?”, anauliza.
Ujumbe huo wa JET ulitembelea kata ya Utengule na kujionea wenyewe jinsi bwawa kubwa la enzi na enzi la Ngapemba lilivyoathiriwa na climate change na wafugaji hao wa Kisukuma.
Bwawa hilo lililokuwa na ukubwa wa eka za mraba 1,000 na lililokuwa na hekaheka nyingi za uvuvi, sasa limenyauka na kusinyaa na kubakia eka chache tu za mraba.
Zamani bwawa hilo lilikuwa likichukuliwa kuwa ni takatifu (sacred) kwa imani za makabila ya asili ya maeneo hayo. Ndani ya bwawa hilo kulikuwa na msitu mdogo ambako wanavijiji walikwenda kwa ajili ya kufanya matambiko yao.
Kwa sababu hiyo, ilijengwa imani kwamba mtu yeyote ambaye angetenda chochote dhidi ya ustawi wa bwawa hilo kama vile kuvua samaki wachanga na kuwatupa au kuziba mikondo ya maji yanayoingia katika bwawa hilo, angepotezwa kabisa duniani bila mwili wake kuonekana! Kuna hata simulizi za watu inaoaminika walipotea kwa kufanya vitendo kinyume na ustawi wa bwawa hilo!
Imani hizo za kale, kwa kiasi kikubwa, zilichangia kulitunza bwawa hilo miaka hadi miaka. Lakini hali ilianza kubadilika kwa kasi mwaka 2006 wakati wafugaji hao wa Kisukuma waliofukuzwa kutoka Ihefu walipovamia maeneo jirani na bwawa hilo.
Kwa wafugaji hao wa Kisukuma, ‘vitisho’ vya imani hizo za kale havikuwazuia kuyavamia maeneo ya pembeni ya Bwawa la Ngapemba yaliyokuwa na nyasi mbichi kulisha ng’ombe zao. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kusinyaa na kukauka kwa Bwawa la Ngapemba.
Huhitaji kuwa mtaalamu wa mazingira kutabiri kwamba bwawa hilo ambalo maelfu ya wanavijiji wa Bonde la Kilombero walikuwa wakinufaika nalo sasa lipo “ICU”, na muda si mrefu litatoweka kabisa katika uso wa dunia.
Pengine swali la kujiuliuza ni hili: Je; Serikali inafanya nini kuhusu wavamizi hao wa wafugaji wa Kisukuma katika Bonde la Mto Kilombero?
Maofisa wa serikali ngazi za wilaya waliozungumza na ujumbe huo wa JET walikuwa waangalifu mno kulizungumzia suala hilo, kwa maelezo (au tuseme madai) kuwa ni ‘nyeti’.
Hata hivyo, Rais Kikwete alipata kutangaza mwaka jana kwamba wafugaji hao wangeondolewa wote katika jimbo hilo kwa nguvu za serikali ili kulinusuru. Na kwa hakika, operesheni za kuwaondoa zilishaanza katika baadhi ya vijiji vya bonde hilo; lakini ghafla zilisitishwa kwa maelekezo kutoka “juu”.
JET haikuweza kufahamu mara moja ni kwa nini Serikali iliamua, ghafla, kulisitisha zoezi hilo, lakini habari za uhakika zinasema kwamba hatua hiyo ilikuwa inahusiana na suala nyeti la uchaguzi mkuu uliopita (Oktoba 31).
Kwa maneno mengine, CCM ilihofia kupoteza kura za wafugaji hao wa Kisukuma katika Bonde la Kilombero, na hivyo ikachagua ‘kulisaliti’ bonde kwa ‘malipo ya kura’. Hiyo ndiyo CCM yetu!
Vyovyote vile; lojiki ni kwamba kwa kuwa uchaguzi mkuu umeshapita na hatuna mwingine hadi mwaka 2015, basi, zoezi hilo la kuwaondoa kwa nguvu wafugaji hao wa Kisukuma katika Bonde la Mto Rufiji, litaanzishwa tena na kuhitimishwa haraka iwezekanavyo.
Wapo wadau wa mazingira wanaoamini kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa, lakini wapo wengine wanaoamini kwamba hilo halitatokea; na hao wanadai kwamba wafugaji hao wa Kisukuma wana ka-uwezo ‘fulani’ ka kuwaweka mfukoni watendaji wa Serikali na kuwafanya kuendelea kusitasita kuchukua hatua za kuwatimua.
Wadau hao wanatoa mfano wa Ihefu (Mbarali) ambakoi JET na asasi nyingine kadhaa za mazingira ilipiga kelele kwa Serikali kwa miaka 10 kuwafukuza wafugaji hao wa Kisukuma, lakini hatua ilikuja kuchukuliwa mwaka 2006 (miaka 10 baadaye) wakati hali ilishakuwa mbaya kabisa.
Tatizo, hivyo basi, ni kwamba muda unayoyoma kwa Bonde la Kilombero. Kwa hali ambayo JET ilijionea katika ziara ya bonde hilo, hakutabaki kivutio chochote cha maana katika kipindi cha miaka 10 ijayo kama hatua ya kuwafukuza wafugaji hao itacheleweshwa.
Na isisahaulike pia kwamba Ubelgiji, ambayo msaada wake wa mapesa ulisaidia mno kuendesha programu za kutunza mazingira, itamaliza ufadhili wake kwa mradi wa Ramsar katika bonde hilo miezi mitatu ijayo. Na kama tunavyoijua Serikali yetu, uchacharikaji wake unakua mdogo pasipokuwepo na fedha za mfadhili wa nje! Labda uendeshaji serikali safari hii uwe tofauti.
 
..tufukue kaburi linalohusu uharibifu wa mazingira bonde la mto ruaha, kilombero, na rufiji.
 
KILOMBERO: Kutoka mito 79 hadi 39 ya sasa, kulikoni?

Johnson Mbwambo
Novemba 24, 2010

Climate Change, wafugaji Wasukuma balaa tupu

Aina 20 za samaki zatoweka, wanyamapori wapungua

HAPO kale, Bonde la Mto Kilombero ambalo lipo katika wilaya za Ulanga na Kilombero, mkoani Morogoro, lilikuwa moja ya vivutio vikubwa vya sayari yetu hii. Vivutio vyake vilivuma hadi nje ya nchi kiasi hata cha kusababisha bonde hilo kuingizwa katika orodha ya maeneo ya dunia yanayolindwa na Ramsar; yaani ule mkataba wa kimataifa unaolenga kuhifadhi ardhioevu (wetlands) muhimu duniani.

Sifa zake zilikuwa nyingi: Bonde la Kilombero lilikuwa na mtandao wa mito zaidi ya 79 iliyokuwa ikititirisha maji misimu yote ya mwaka ambapo mito ya Luhuji, Mnyera, Furua, Mpanga, Kihanzi, Luipa, na Ruaha Mkuu huungana na Mto Kilombero na kuwa Mto Rufiji.

Si hivyo tu. Bonde la Mto Kilombero lilikuwa ndiyo makazi ya asilimia 75 ya wanyamapori aina ya Sheshe duniani. Aidha, ndiko pekee duniani vilikopatikana baadhi ya viumbe hai duniani kama vile vyura wa njano wa Kihantsi au Mbega Wekundu wa Udzungwa.

Mbali ya hayo, Bonde la Mto Kilombero lilikuwa ndilo pekee nchini ambako unaweza kupata aina nyingi zaidi za samaki (takriban 40) kuanzia kambale na perege wanaopatikana sehemu nyingi nchini hadi Kapatwa, Ndungu, Ningu nk ambao hupatikana sehemu chache tu.

Hivyo ndivyo Bonde la Kilombero lilivyokuwa angalau miaka 30 iliyopita; lakini katika ziara ya hivi karibuni ya waandishi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), ilibainika kwamba bonde hilo limepoteza baadhi ya vivutio vyake hivyo, na hatua zisipochukuliwa haraka vivutio vilivyosalia navyo vitatoweka kwa kasi.

Kwa mfano, taarifa zilizopatikana kutoka Idara ya Maliasili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mjini Ifakara, zinaonyesha kwamba mito ambayo hutiririsha maji mwaka mzima sasa imebakia 39 tu katika bonde zima kutoka idadi ya mwanzo ya mito 79.

Aina za samaki nazo zimepungua kutoka 40 za mwanzo hadi 20 za sasa. Angalau wenyeji katika vijiji kadhaa vya wilaya ya Kilombero ambavyo ujumbe huo wa JET ulivitembelea, wamethibitisha kwamba samaki aina ya Kapatwa ametoweka kabisa katika bonde hilo. Aina nyingine ya samaki ambao wamepungua sana na wapo katika hatari ya kutoweka kabisa ni Ndungu, Mjongwa, Ningu na Mdelwa (golden fish).

Hata kwa wanyamapori hadithi ni hiyo hiyo. Wenyeji wa vijiji vya wilaya hiyo walieleza kwamba sasa ni taabu mno kumuona mnyama anayeitwa Mbega katika mapori yao wakati ambapo zamani walikuwa wengi mno.
Je nini kimetokea? Ilikuaje Bonde la Kilombero ambalo lilikuwa na mito 79 inayotiririsha maji mwaka mzima libakie na mito ya namna hiyo 39 tu? Ilikuaje mpaka wanyama kama Mbega na samaki kama Kapatwa sasa wawe ni historia katika Bonde la Mto Kilombero?

Kuna mambo mengi yanayoweza kutajwa yaliyosababisha hali hiyo hasi, lakini yote yanaweza kujumuishwa katika jambo moja kubwa; nalo ni uharibifu wa mazingira unaoendelea kwa kasi katika bonde hilo - uharibifu ambao athari zake zimekuwa ni maradufu kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi (climate change) yanayoisumbua dunia nzima.
Japo Bonde la Mto Kilombero liliorodheshwa rasmi kuwa eneo la Ramsar (Ramsar site) tangu Aprili 26, 2002 na kuanzia muda huo Ubelgiji imekuwa ikifadhili mradi wa Ramsar kwenye bonde hilo kupitia Halmashauri za wilaya ya Ulanga na Kilombero, bado kasi ya uharibifu wa mazingira katika bonde hilo inafifisha mafanikio ya mradi huo.
Ni kweli kwamba, kupitia mradi huo wa Ramsar unaofadhiliwa na Ubelgiji katika bonde hilo, wanavijiji wengi wamepatiwa elimu ya mazingira na hata kusaidiwa kuanzisha kamati za mazingira.

Ni kweli pia kwamba chini ya mradi huo vimeanzishwa hata vikundi vya maskauti wa vijiji (VGS Village Game Scouts) ili kupambana na waharibifu wa mazingira na majangili, lakini mafanikio bado hayaridhishi, na hivyo kazi iliyopo mbele bado ni kubwa.

Lakini pengine kinachokatisha tamaa zaidi ni kwamba wakati mradi wa Ramsar ukijaribu kuliokoa bonde hilo, Serikali imekaribisha tatizo jipya katika bonde hilo; tatizo ambalo, kwa sasa, ndilo linalochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika bonde hilo. Tatizo jipya linalozungumziwa hapa ni uvamizi wa wafugaji wa Kisukuma katika Bonde la Mto Kilombero.

JET ilijionea katika ziara hiyo namna vyanzo mbalimbali vya maji vilivyoharibiwa na wafugaji hao wa Kisukuma ambao wamevamia bonde hilo na maelfu ya mifugo yao wakitokea Ihefu (Mbarali) ambako walitimuliwa na serikali mwaka 2006 baada ya kuiharibu pia ardhi oevu hiyo.

Wafugaji hao wa Kisukuma ambao kwa desturi na tabia zao chafu si rafiki wa mazingira, wamekata miti katika mapori mengi na kuweka maskani yao katika vyanzo vingi vya maji katika Bonde la Kilombero.

Kwa hakika, wamekuwa ndiyo kero kubwa katika vijiji vingi ambavyo JET ilitembelea wakati wa ziara hiyo.

Hebu wafikishieni salamu wakubwa serikalini huko Dar es Salaam: Wasipochukua hatua ya kuwafukuza wafugaji hawa wa Kisukuma, vyanzo vyote vya maji vitatoweka, na hata Mto Kilombero hautakuwa na maji mengi. Na hata lile pantoni waliloweka kwenye kivuko kile cha Ifakara halitaweza kufanya kazi kwa sababu ya kina cha maji kupungua, ndivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Mofu, Alvinuis Linus Ngwila alivyouambia ujumbe huo wa JET kwa uchungu mkubwa.

Je; wanavijiji wa Mofu, wilayani Kolombero, wanafanya nini kutetea maeneo yao yasiharibiwe na wafugaji hao wa Kisukuma; maana wao ndiyo waathirika wa kwanza wa kuharibka kwa bonde hilo?

Ngwila anacheka kwanza kabla ya kulijibu swali hilo: Wanavijiji waliwahi kuwakamata wafugaji wa Kisukuma waliowakuta wakikata miti, lakini walipowafikisha kwa mamlaka husika za serikali, wanavijiji wakageuziwa kibao na kushitakiwa wao badala ya wafugaji wale waliowakamata.

Kwa mujibu wa Ngwila, kuanzia hapo wanavijiji walipoteza morali ya kupambana na wafugaji hao wa Kisukuma. Na sasa wanaendelea kuharibu vyanzo vya maji na kukata miti katika misitu watakavyo, anasema mwenyekiti huyo wa kijiji.

Alipoulizwa iwapo mbunge wao wa zamani aliwasaidia lolote katika mapambano hayo dhidi ya wafugaji hao, Ngwila alimaka: Mbunge?! Mbunge alifika hapa kijijini mara mbili tu mara ya kwanza kukampeni na mara ya pili kushukuru baada ya kuchaguliwa. Baada ya hapo hatukumuona tena.

JET ilithibitisha kwamba mahusiano kati ya wanavijiji hao wa Mofu na wafugaji hao wa Kisukuma, ni kama bomu linalosubiri kulipuka. Ni katika kijiji hicho ambako kuna mwanakijiji mmoja ambaye sasa ni kipofu baada ya kuondolewa macho na wafugaji wa Kisukuma aliojaribu kupambana nao alipowakuta wakilisha mifugo kwenye shamba lake.

Katika vijiji vingine vya Njage, Mngeta, Mchombe, Merera na hata mji mdogo wa Mlimba, kidole cha uharibifu wa mazingira kilielekezwa kwa hao hao wafugaji wa Kisukuma waliotimuliwa kutoka Mbarali (Ihefu).
Katika kijiji cha Njagi, mjumbe wa Serikali ya kijiji, Abdallah Iporah, anakiri kwamba mabadiliko ya tabianchi yamechangia mno kuvisambaratisha vivutio vya Bonde la Kilombero. Zamani hapa tulikuwa tukipata mvua karibu kila mwezi, lakini sasa hatuna tena uhakika wa mvua. Kuanzia Mei hatujapata mvua hata mara moja. Tulipanda mahindi lakini yamekauka.

Lakini pamoja na mabadiliko ya tabianchi, mzee huyo bado anaelekeza kidole chake kwa wafugaji wa Kisukuma kwamba wanachangia zaidi katika kuyafanya maisha yao wote kuwa magumu zaidi.
Wamevamia maeneo yetu kwa mamia. Kwanza anakuja mmoja na anawasilisha maombi ya kuishi kijijini kwa serikali ya kijiji. Akishakubaliwa anakaa kama wiki moja tu na kuondoka kwenda kuchukua ngombe wake kibao. Baada ya muda anamwita mwenzake na mwenzake naye anamwita mwenzake. Na wote hao kila mmoja ana wake si chini ya wanne na watoto kibao na ngombe kibao. Baada ya muda wanavivamia vyanzo vya maji na mifugo yao, na hakuna tena wa kuwaambia ondokeni. Wanakuwa wakali na wako tayari kuua, anasema mzee huyo.

Uharibifu huo wa mazingira na vyanzo vya maji unaofanywa na wafugaji hao wa Kisukuma ukichangiwa na mabadiliko ya tabianchi, vimeyafanya maisha ya wanavijiji wengi katika Bonde la Kilombero yawe magumu zaidi.
Otwin Mafui ni Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Merera. Anasema: Zamani samaki walikuwa bwerere. Kikombe kikubwa kilichojazwa samaki wadogo wabichi ulikuwa ukikipata kwa Sh. 200 tu, lakini sasa kwa kiasi hicho hicho cha pesa unapata samaki mmoja tu. Mwaka 2003/2004 kambale mmoja alikuwa anauzwa Sh. 1,000, sasa ni kati ya Sh. 5,000 na Sh. 10,000.

Kwa nini samaki wamepungua katika kijiji chake? Jibu lake ni kwamba maeneo mengi ya ardhioevu ambako walikuwa wakipatikana kwa wingi yamekauka kabisa, na pia samaki wamekimbia katika baadhi ya mito kwa sababu ya kupungua vina vya maji na kuharibiwa kwa maeneo ya mazalio yao.

Mvuvi Alex Ndalala alifikia hatua ya kuutajia haraka haraka ujumbe huo wa JET majina ya mito ya maeneo yao ambayo imekauka. Mto Mkusi umekauka, Mto Mpakaka umekauka, Mto Nagakuru umekauka, Mto Mkula umekauka... na bwawa la asili la Mhoma nalo ikifika mwezi wa nane tu limekauka. Sasa unadhani hizo samaki zitatoka wapi?, anauliza.

Ujumbe huo wa JET ulitembelea kata ya Utengule na kujionea wenyewe jinsi bwawa kubwa la enzi na enzi la Ngapemba lilivyoathiriwa na climate change na wafugaji hao wa Kisukuma.
Bwawa hilo lililokuwa na ukubwa wa eka za mraba 1,000 na lililokuwa na hekaheka nyingi za uvuvi, sasa limenyauka na kusinyaa na kubakia eka chache tu za mraba.

Zamani bwawa hilo lilikuwa likichukuliwa kuwa ni takatifu (sacred) kwa imani za makabila ya asili ya maeneo hayo. Ndani ya bwawa hilo kulikuwa na msitu mdogo ambako wanavijiji walikwenda kwa ajili ya kufanya matambiko yao.
Kwa sababu hiyo, ilijengwa imani kwamba mtu yeyote ambaye angetenda chochote dhidi ya ustawi wa bwawa hilo kama vile kuvua samaki wachanga na kuwatupa au kuziba mikondo ya maji yanayoingia katika bwawa hilo, angepotezwa kabisa duniani bila mwili wake kuonekana! Kuna hata simulizi za watu inaoaminika walipotea kwa kufanya vitendo kinyume na ustawi wa bwawa hilo!

Imani hizo za kale, kwa kiasi kikubwa, zilichangia kulitunza bwawa hilo miaka hadi miaka. Lakini hali ilianza kubadilika kwa kasi mwaka 2006 wakati wafugaji hao wa Kisukuma waliofukuzwa kutoka Ihefu walipovamia maeneo jirani na bwawa hilo.

Kwa wafugaji hao wa Kisukuma, vitisho vya imani hizo za kale havikuwazuia kuyavamia maeneo ya pembeni ya Bwawa la Ngapemba yaliyokuwa na nyasi mbichi kulisha ngombe zao. Na huo ndio ukawa mwanzo wa kusinyaa na kukauka kwa Bwawa la Ngapemba.

Huhitaji kuwa mtaalamu wa mazingira kutabiri kwamba bwawa hilo ambalo maelfu ya wanavijiji wa Bonde la Kilombero walikuwa wakinufaika nalo sasa lipo ICU, na muda si mrefu litatoweka kabisa katika uso wa dunia.
Pengine swali la kujiuliuza ni hili: Je; Serikali inafanya nini kuhusu wavamizi hao wa wafugaji wa Kisukuma katika Bonde la Mto Kilombero?

Maofisa wa serikali ngazi za wilaya waliozungumza na ujumbe huo wa JET walikuwa waangalifu mno kulizungumzia suala hilo, kwa maelezo (au tuseme madai) kuwa ni nyeti.

Hata hivyo, Rais Kikwete alipata kutangaza mwaka jana kwamba wafugaji hao wangeondolewa wote katika jimbo hilo kwa nguvu za serikali ili kulinusuru. Na kwa hakika, operesheni za kuwaondoa zilishaanza katika baadhi ya vijiji vya bonde hilo; lakini ghafla zilisitishwa kwa maelekezo kutoka juu.

JET haikuweza kufahamu mara moja ni kwa nini Serikali iliamua, ghafla, kulisitisha zoezi hilo, lakini habari za uhakika zinasema kwamba hatua hiyo ilikuwa inahusiana na suala nyeti la uchaguzi mkuu uliopita (Oktoba 31).
Kwa maneno mengine, CCM ilihofia kupoteza kura za wafugaji hao wa Kisukuma katika Bonde la Kilombero, na hivyo ikachagua kulisaliti bonde kwa malipo ya kura. Hiyo ndiyo CCM yetu!

Vyovyote vile; lojiki ni kwamba kwa kuwa uchaguzi mkuu umeshapita na hatuna mwingine hadi mwaka 2015, basi, zoezi hilo la kuwaondoa kwa nguvu wafugaji hao wa Kisukuma katika Bonde la Mto Rufiji, litaanzishwa tena na kuhitimishwa haraka iwezekanavyo.

Wapo wadau wa mazingira wanaoamini kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa, lakini wapo wengine wanaoamini kwamba hilo halitatokea; na hao wanadai kwamba wafugaji hao wa Kisukuma wana ka-uwezo fulani ka kuwaweka mfukoni watendaji wa Serikali na kuwafanya kuendelea kusitasita kuchukua hatua za kuwatimua.
Wadau hao wanatoa mfano wa Ihefu (Mbarali) ambakoi JET na asasi nyingine kadhaa za mazingira ilipiga kelele kwa Serikali kwa miaka 10 kuwafukuza wafugaji hao wa Kisukuma, lakini hatua ilikuja kuchukuliwa mwaka 2006 (miaka 10 baadaye) wakati hali ilishakuwa mbaya kabisa.

Tatizo, hivyo basi, ni kwamba muda unayoyoma kwa Bonde la Kilombero. Kwa hali ambayo JET ilijionea katika ziara ya bonde hilo, hakutabaki kivutio chochote cha maana katika kipindi cha miaka 10 ijayo kama hatua ya kuwafukuza wafugaji hao itacheleweshwa.

Na isisahaulike pia kwamba Ubelgiji, ambayo msaada wake wa mapesa ulisaidia mno kuendesha programu za kutunza mazingira, itamaliza ufadhili wake kwa mradi wa Ramsar katika bonde hilo miezi mitatu ijayo. Na kama tunavyoijua Serikali yetu, uchacharikaji wake unakua mdogo pasipokuwepo na fedha za mfadhili wa nje! Labda uendeshaji serikali safari hii uwe tofauti.

WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.
 
Back
Top Bottom