Bomu la arusha na bajeti ya tanzania 2013/2014


kaswalala

kaswalala

Member
Joined
Mar 13, 2013
Messages
42
Likes
0
Points
0
Age
36
kaswalala

kaswalala

Member
Joined Mar 13, 2013
42 0 0
Wapendwa watanzania napenda kutoa tafakari zangu kwa kuhusisha mlipuko wa bomu la arusha na mjadala wa bajeti unaendelea hivi sasa kule bungeni. Wengi wameuhusisha mlipuko ule na nia ya kuvuruga uchaguzi wa zile kata nne za pale Arusha mjini baadaa ya watawala kuona kuwa wanaelekea kushindwa, lakini tujiongeze zaidi awali aliyeharibu uchaguzi wa meya wa jiji alikuwa yule mbunge wa viti maalumu wa ccm kutoka Tanga (simkumbuki jina) pia ikumbukwe kuwa yupo diwani wa TLP ambaye alitumika kuibeba ccm kwenye ule uchaguzi wa meya, kwahiyo kwa mtazamo wangu hata kama chadema watashinda zile kata nne bado nafikiri hawatoweza kuchukua halmashauri kutokana na lile zengwe la awali ( la yule diwani wa TLP na Mbunge wa viti maalumu wa Tanga aliyehusisishwa kwenye uchaguzi wa meya), kwahiyo kwakuwa watawala wanautambua ukweli huu ndio mana najaribu kutafakari kuwa lengo la mlipuko wa lile bomu kama watawala ndio wamahusika basi lengo lao halikuwa kuvuruga uchaguzi kwa ajiri ya utawala wa jiji la Arusha.

Ndugu zangu ikumbukwe kuwa bajeti kuu ya serikali ndio kwanza ilikuwa mbichi tangu isomwe, na jumatatu ilikuwa isomwe bajeti ya kambi ya upinzani, sasa najiongeza kwa kusema huenda watawala kwa kujua nini walichokifanya katika hii bajeti pia kwa kutambua ni kwa jinsi gani watanzania walivyokuwa na hamu ya kusikia michango ya wawakilishi wao ( hasa wa upinzani ) ambao kwa sasa ndio wanaonekana kuwa watetezi wakubwa wa wananchi wakaamua kuamisha makusudi fikra za watanzania kutoka bungeni kwenda Arusha, sasa watanzania wanazungumzia zaidi masuala ya Arusha kuliko kuifuatilia bajeti yao na kujua nini mustakabali wa nchi yao. Huu ni mchezo mchafu sana watanzania tuushtukie na tulaani mipango hii mibovu inayolenga kuumiza watu kwa maslahi ya watawala.

" DAIMA GIZA HALIWEZI KUSHINDA NURU" " TUTAANZA NA MUNGU NA KUMALIZA NA MUNGU"
 

Forum statistics

Threads 1,273,483
Members 490,428
Posts 30,482,924