Bomoabomoa yaitikisa Buza kwa Lulenge wilayani Temeke

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Polisi, wamesimamia ubomoaji wa nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara maeneo ya Buza kwa Lulenge Temeke jijini Dar es Salaam jana.

Imeelezwa kuwa wamiliki wa nyumba hizo walikwisha lipwa fidia na TANROADS lakini wakawa wameshindwa kuondoka huku wengine wakiendeleza ujenzi.

1454253217097.jpg

1454253227496.jpg

1454253235294.jpg

1454253248336.jpg

1454253259397.jpg
 
Tuache unafiki hapa wakati mwingine sio wa kupeana pole,umelipwa na umesaini bado upo hapo hapo?
Dah poleni ki utu tu lakini muwe na utaratibu wa kuishi kwa kufuata sheria
 
Ki ukweli inauma, maana kujenga si mchezo wa kuigiza,ndipo inapotakiwa kuwa makini wakati wa kununua kiwanja. Je hakipo hifadhi ya barabara ???, je hakipo bondeni ???? je hakipo eneo la wazi na je hakipo karibu na kingo za mto/bahari ???
 
Kibinadamu inatia uchungu sana lakini ifike mahali serikali ijifunze. Watu wakilipwa fidia waondoke ndani ya miezi sita.
 
Kibinadamu inatia uchungu sana lakini ifike mahali serikali ijifunze. Watu wakilipwa fidia waondoke ndani ya miezi sita.
isijekuwa alipita politician kama kule rocky city akasema kaeni tu
 
Back
Top Bottom