Bomoa bomoa ya Tabata na masuala ya ndoa

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,462
4,364
Waliovunjiwa makazi Dar sasa wahofia kuvunjika kwa ndoa zao
Furaha Kijingo na Rehema Rajabu

WAKAZI wa Tabata Dampo waliobomolewa nyumba zao na Manispaa ya Ilala, wamesema ndoa zao zipo hatarini kutokana na kutoonana na wenzi wao takribani wiki tatu mfululizo.

Walisema hivi sasa wanalala kwa makundi, huku muda mwingi wakikosa faragha ya kujadili masuala muhimu ya familia.

Sophia Bende alisema, wasiwasi wake huenda ndoa yake ikaathirika au kuvunjika kwa sababu hadi sasa, hajui mume wake alipokwenda tangu kubomolewa kwa nyumba wiki tatu zilizopita.

"Sijui mume wangu aliko mpaka dakika hii, sijui analala kambi ipi, tangu tuoane ndoa yetu ina miaka 23, lakini sasa bomoabomoa inataka kuvunja ndoa yangu," alisema Bende.

Mkazi mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Amani, alionyesha kusikitishwa na kitendo cha kutenganishwa na mkewe, akisema bomoabomoa hiyo inaweza ikasababisha maambukizi ya Ukimwi kwa wahanga hao.

"Sio siri bomoabomoa hii inaweza ikasababisha maambukizi ya Ukimwi, mpaka leo sijakutana na mke wangu," alisema Amani.

Source: Mwananchi 3/26/2008

Posted Date::3/25/2008

Jamani vipi hapo? Kuaminiana kupo?
 
Hao wanaodai au kuhofia kuvunjika kwa ndoa zao hana maadili yandoa na pia hawajui maana ya ndoa.Kwa mujibu wa sheria za TZ,hapa hakuna mazingira ya kuvunjika kwa ndoa ila wanaleta masiala.Mimi nadhani mgogoro wa Tabata tusiunyambulishe sana mwishowe tutapoteza hata ile maana.
 
Back
Top Bottom