Bomoa bomoa ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomoa bomoa ubungo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mimi-soso, Feb 23, 2011.

 1. m

  mimi-soso Senior Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimesoma post yenye tamko la Mhe. Mnyika binafsi kwanza nimeliona liko too soft, sidhani kama hiki ni kipindi cha kuwa kidiplomasia namna hii wakati wananchi wanaendelea kuteseka.

  Kigezo wanachotumia Magufuli na TANROADS si sahihi kwani kuanzia 2006 nyumba zote ambazo zinaathirika na mradi wa mabasi DART zilithaminiwa na wale ambao nyumba zao zilionekana kuathirika na mradi walilipwa fidia na nyumba hizo kubomolewa zikabaki chache ambazo wenyewe hawakuridhika na fidia.

  Kama tayari study ilishafanyika na kuonyesha maeneo yanayoathirika iweje leo kuwe na ongezeko la maeneo yanayohitaji kubomolewa? Na kama kuna watu ambao walishalipwa fidia kwa ajili ya mradi huu kwanini hawa wengine wanyimwe fidia? ni vigezo gani vinatumika kuamua nani analipwa fidia na nani halipwi?

  Na kuna njia nyingi sana za kupunguza msongamano kwanini hizo nazo zisiangaliwe? kwanini wananchi waendelee kukoseshwa usingizi kwa ajili ya mradi mmoja ambao tunausubiri kama vile tunasubiri kuona white elephant?
   
Loading...