Bomoa bomoa, tumpongeze Rais Magufuli kujirekebisha

Chrizant Kibogoyo

Senior Member
Aug 12, 2016
159
81
Tarehe 02 Nov 2017 nilipokea Simu na ujumbe ukinipongeza kwa mahojiano niliyoyafanya na kituo cha runinga cha ITV.

Mahojiano yale niliyafanya na ITV mwaka 2015 nikiwa Mwenyekiti wa Wahanga wa Bomoa bomoa ya Barabara ya Morogoro ikiwa ni moja ya njia za kuwatetea waathirika. Pengine kituo cha ITV waliamua kurejea kurusha mahojiano hayo baada ya suala la bomoa bomoa kuibuliwa na Mhe Rais Magufuli katika hotuba yake ya hivi karubuni jijini Mwanza alipositisha bomoa bomoa iliyokuwa itekelezwe jijini humo na kuzitaka mamlaka husika kuwa na "huruma za kibinadamu" hata wananchi walikosea na kuvunja sheria. Kwa hakika watanzani wengi wameshangazwa na kupigwa butwaa na mabadiliko haya msimamo wa Mhe Rais kiasi cha kuanza kumshutumu kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo ubaguzi, upendeleo n.k

Kiini cha tuhuma hizi dhidi ya Mhe Rais ni ukweli kuwa kauli yake ya kuzitaka mamlaka husika kuwa na huruma na wananchi hata kama wamevunja sheria inakuja miezi michache baada ya maelfu wa wananchi wa eneo la Ubuno hadi Kiruvia kubomolewa makazi yao pasipo huruma yeyote licha ya ukweli kuwa walikuwa wameigaragaza Setikali, Wizara ya Ujenzi na Tanroads mbele ya vyombo vya sheria na mahakama kutamka wazi wazi kuwa wananchi hawa sio wavamizi na wanamiliki Ardhi husika kuhalali kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi. Ikumbukwe kuwa wahanga wengi wa hii bomoa bomoa wameathirika kwa njia mbali mbali ikiwemo kupoteza maisha kwa mishtuko ya kubomolewa makazi yao n.k.

Maandiko ya kidini yanatufunza kushukuru kwa jambo lolote. Wahanga wa bomoa bomoa hii ya kionevu na yenye kila ishara ya uvunjifu wa haki za kikatiba na kusheria za wananchi tulilazimika kumshukuru mungu kwa masahibu yaliyotukuta
.

Kwa dhati ya moyo wangu nichukue fursa hii kumshukuru nwenyezi mungu kwa kumpatia Rais wetu maono ya kuwa na huruma kwa wananchi wake hususan wale waliokosea na kuvunja sheria katika suala hili la bomoa bomoa. Ni imani yangu kuwa kwa uweza wa mwenyezi kumtia mtukufu Rais wetu huruma itanusuru maelfu ya kaya na adha za bomoa bomoa, ikiwemo kaya kukosa makazi, kupoteza vipato n.k.


Ni imani yangu kuwa kupitia maombi yetu mwenyezi mungu atazidi kumwongoza Rais wetu huruma kwa wananchi wake.
 
Alafu wewe unaleta utani kweli
what is Kujirekebisha wakati maelfu ya Raia sasa wamebaki homeless
what is Kujirekebisha wakati makumi ya watu wamekufa kwa sababu ya maamuzi hayo
What is kujirekebisha wakati ni dhahiri kwa maneno yake wale waliobomolewa ni aidha kwa sababu hawakumpigia kura au pengine ni wa wapi
Swala la kujirekebisha sio issue muhimu hapa.Swala ni kuwajibishwa,Kila mtu kwenye nchi hii awajibishwe kutokana na matendo yake
sasa hili la kuwajibishana sio lazima litokee leo.Nchi itaishi milele.Kwa hio zitakuja serikali zijazo.hawa watu watawajibishwa.
 
Tarehe 02 Nov 2017 nilipokea Simu na ujumbe ukinipongeza kwa mahojiano niliyoyafanya na kituo cha runinga cha ITV.
Mahojiano Yale niliyafanya 2015 nikiwa Mwenyekiti wa Wahanga wa Bomoa bomoa ya Barabara ya Morogoro ikiwa ni njia moja ya njia za kuwatetea waathirika. Pengine kituo cha ITV waliamua kurejea kurusha mahojiano hayo baada ya suala la bomoa bomoa kuibuliwa na Mhe Raid Magufuli katika hotuba yake jijini Mwanza alipositisha bomoa bomoa iliyokuwa itekelezwe jijini Mwanza na kuzitaka mamlaka husika kuwa na "huruma za kibinadamu" hats wananchi walikosea.

Kauli hii ya mtukufu Rais inakuja miezi michache baada ya maelfu wa wananchi wa eneo la Ubuno hadi Kiruvia kubomolewa makazi yao pasipo huruma yeyote. Wengi wameathirika kwa njia mbali mbali ikiwemo kupoteza maisha kwa mishtuko n.k.
Mwenyezi
KIRUVIA o_O
 
Niwashukuru nyote mliochangia. Nadhani wengi wenu hamkuupsta msingi wa mafa yangu kuwa ni maandiko ya kudini kuwa "shukuruni kwa kila jambo".

Hivyo nikiwa kiongozi wa wahanga wa hiyo bomoa bomoa ndio niliona njia peke iliyobaki baada ya jitihada zetu zote ikiwemo kuishinda serikali mahakamani kushindwa kunusuru makazi yetu.

Tuna imani kuwa sasa maelfu ya kaya zilizokuwa njiani kubomolewa zitanusurika na madhira hayo. Hivyo ni lazima nimpongeze Mhe Raid kwa hatua hiyo.
 
Niwashukuru nyote mliochangia. Nadhani wengi wenu hamkuupsta msingi wa mafa yangu kuwa ni maandiko ya kudini kuwa "shukuruni kwa kila jambo".

Hivyo nikiwa kiongozi wa wahanga wa hiyo bomoa bomoa ndio niliona njia peke iliyobaki baada ya jitihada zetu zote ikiwemo kuishinda serikali mahakamani kushindwa kunusuru makazi yetu.

Tuna imani kuwa sasa maelfu ya kaya zilizokuwa njiani kubomolewa zitanusurika na madhira hayo. Hivyo ni lazima nimpongeze Mhe Raid kwa hatua hiyo.
Mkuu kwenu wewe ni wangapi katika familia, samahani lakini.
 
Kweli Kibogoyo sasa umepoteza na meno kabisa baada ya kupoteza makazi! Kilichotokea Mwanza kinaibua maswali zaidi kuliko majibu, kuna lipi la kushukuru hapo mbona unaridhika prematurely?! Hivi kwa kauli ya mwanza Mrs Ng'itu kafufuka? Na hao wanaolala nje je?!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom