Chrizant Kibogoyo
Senior Member
- Aug 12, 2016
- 159
- 81
Tarehe 02 Nov 2017 nilipokea Simu na ujumbe ukinipongeza kwa mahojiano niliyoyafanya na kituo cha runinga cha ITV.
Mahojiano yale niliyafanya na ITV mwaka 2015 nikiwa Mwenyekiti wa Wahanga wa Bomoa bomoa ya Barabara ya Morogoro ikiwa ni moja ya njia za kuwatetea waathirika. Pengine kituo cha ITV waliamua kurejea kurusha mahojiano hayo baada ya suala la bomoa bomoa kuibuliwa na Mhe Rais Magufuli katika hotuba yake ya hivi karubuni jijini Mwanza alipositisha bomoa bomoa iliyokuwa itekelezwe jijini humo na kuzitaka mamlaka husika kuwa na "huruma za kibinadamu" hata wananchi walikosea na kuvunja sheria. Kwa hakika watanzani wengi wameshangazwa na kupigwa butwaa na mabadiliko haya msimamo wa Mhe Rais kiasi cha kuanza kumshutumu kwa tuhuma mbali mbali ikiwemo ubaguzi, upendeleo n.k
Kiini cha tuhuma hizi dhidi ya Mhe Rais ni ukweli kuwa kauli yake ya kuzitaka mamlaka husika kuwa na huruma na wananchi hata kama wamevunja sheria inakuja miezi michache baada ya maelfu wa wananchi wa eneo la Ubuno hadi Kiruvia kubomolewa makazi yao pasipo huruma yeyote licha ya ukweli kuwa walikuwa wameigaragaza Setikali, Wizara ya Ujenzi na Tanroads mbele ya vyombo vya sheria na mahakama kutamka wazi wazi kuwa wananchi hawa sio wavamizi na wanamiliki Ardhi husika kuhalali kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi. Ikumbukwe kuwa wahanga wengi wa hii bomoa bomoa wameathirika kwa njia mbali mbali ikiwemo kupoteza maisha kwa mishtuko ya kubomolewa makazi yao n.k.
Maandiko ya kidini yanatufunza kushukuru kwa jambo lolote. Wahanga wa bomoa bomoa hii ya kionevu na yenye kila ishara ya uvunjifu wa haki za kikatiba na kusheria za wananchi tulilazimika kumshukuru mungu kwa masahibu yaliyotukuta
.
Kwa dhati ya moyo wangu nichukue fursa hii kumshukuru nwenyezi mungu kwa kumpatia Rais wetu maono ya kuwa na huruma kwa wananchi wake hususan wale waliokosea na kuvunja sheria katika suala hili la bomoa bomoa. Ni imani yangu kuwa kwa uweza wa mwenyezi kumtia mtukufu Rais wetu huruma itanusuru maelfu ya kaya na adha za bomoa bomoa, ikiwemo kaya kukosa makazi, kupoteza vipato n.k.
Ni imani yangu kuwa kupitia maombi yetu mwenyezi mungu atazidi kumwongoza Rais wetu huruma kwa wananchi wake.