Bomoa Bomoa Mbezi Beach Samaki Wabichi-Goba Rd Yaja?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomoa Bomoa Mbezi Beach Samaki Wabichi-Goba Rd Yaja?.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Mar 22, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Wakazi wa Mbezi Beach eneo la Samaki Wabichi, kuelekea Mbezi Juu kupitia Goba Rd, huenda wakakumbwa na bomoa bomoa ya upanuzi wa barabara ya Goba ambayo ilikuwa ni reginal road yenye upana wa mita 10, na kubadili kuwa main rd kwa upana wa mita 45, hali itakayopelekea nyumba zote pembezoni mwa barabara hiyo, kukumbwa na bomoa bomoa hiyo.

  Isome habari kamili hapa MICHUZI: Tishio la Bomoa Bomoa Mbezi Juu: Wakazi Waishi kwa Wasiwasi!.

  Pia habari hii iko kwenye magazeti ya Daily News, Guardian, Nipashe, Tanzania Daima na Uhuru.

  Swali, kama ni kweli, watu wameishi hapo tangu mwaka 1948 wakapimiwa viwanja, wakamilikishwa kwa hati miliki, hiyo mipango miji ilikuwa wapi kipindi chote hicho, ndio sasa wanaibuka kuja kuwabomolea watu nyumba zao?.
   
 2. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  maendeleo yana gharama zake...! NCHI HII HAIWEZI KUWA DUNIA YA KWANZA UNLESS MANZESE YOTE IS NO MORE.....!!
   
 3. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  'Walikuwepo, ila walibashiri ni miaka 200 ijayo'
  'Aah! Hao viongozi sheria wanazijua!?'
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Upanuzi barabara Mbezi - Goba waanza visa- Source: Tanzania Daima  na Pascally Mayega
  WAKAZI wa Mbezi Juu, barabara ya Goba eneo la Samaki Wabichi jijini Dar es Salaam wameitaka serikali kuwa wazi, kuwashirikisha, kuzingatia sheria, taratibu na kanuni katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo, vinginevyo watajenga chuki kwa wanachi na serikali yao.

  Wito huo ulitolewa jana katika mkutano wa hadhara wa wakazi hao waliokutana kujadili tishio la kukumbwa na bomoa bomoa ya upanuzi wa barabara ya Goba kwa kiwango cha lami kuunganisha na barabara ya Bagamoyo kuanzia Samaki wabichi kisha kuunganishwa na Barabara ya Morogoro, eneo la Mbezi Mwisho.

  Wakiongozwa na Mwenyekiti wa kikao hicho, Dk. Winfred Milinga, wakazi hao wamedai kuishi kwa wasiwasi kutokana na tishio hilo la serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS), kuiarifu serikali ya mtaa bila kuwashirikisha wananchi ambao ndio waathirika.

  Dk. Milinga alisema tishio hilo limeanzia kwenye barua ya Tanroads yenye kumbukumbu namba RM/TRD/DSM/R.90.1/Vol.II/23 ya Februari 25, 2010 kutoka kwa Meneja wa Tanroads mkoa kwenda kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ikielezea mipaka mipya ya barabara hiyo ni mita 22.5 kutoka katikati ya barabara.

  Alisema vipimo hivyo vinatoka kwenye mita tano zilizopo sasa, hali itakayosababisha bomoabomoa kuzikumba nyumba zote zilizo kando ya barabara hiyo.

  Kwa mujibu wa Dk. Milinga, barua hiyo iliyosainiwa na Nyabakari, imeeleza nia ya serikali kuifanyia matengenezo barabara ya Goba kutoka Mbezi Mwisho hadi Samaki Wabichi na kuweka mipaka kuonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara ni mita 22.5 kutoka katikati ya barabara.

  "Lengo ni kutambua hifadhi ya barabara na kuwatahadharisha wananchi kutokujenga ndani ya hifadhi hiyo," ilieleza sehemu ya barua hiyo.

  Mjumbe wa eneo hilo, Mzee Ali Selemani, ameitaka serikali kuwaheshimu wananchi wake kwa kusisitiza kuwa ndio walioichagua iwaongoze na kwamba bila wananchi, hakuna serikali.

  "Nimeishi hapa tangu mwaka 1948, leo watu wa Tanroads wanakuja na kutishia kuivunja nyumba yangu bila maelezo yoyote au ufafanuzi wa fidia?" aliuza mzee huyo na kuongeza kuwa kwa umri wake wa miaka zaidi ya 70 ataanzia wapi?

  Naye Mzee Jackson Msokwa, alisema kama serikali itafuata sheria, taratibu na kanuni, zinazotawala utwaaji wa maeneo ya watu kwa ajili ya shughuli za maendeo, hakutatokea migogoro yoyote na kusisitiza hatua ya kwanza kabisa ni ushirikishwaji wa wananchi ndipo utekelezaji unafuata.

  Alisema kitendo cha serikali kuanza na utekelezaji bila ushirikishwaji ndicho chanzo kikuu cha migogoro.

  Kikao hicho kimeteua kamati ya watu saba ikiongozwa na Dk. Milinga kufuatilia suala hilo serikalini. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Jamhuri Ngelime, Balozi Fanuel Kuzilwa, Jackson Musokwa, Balozi Mkwizu, Rehema Kayuni na Mary Hamisi, ambaye ni katibu wa kamati hiyo.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  D`Salaam residents riled by pending house demolitions-Source, The Guardian.
  BY THE GUARDIAN REPORTER
  22nd March 2011
  Email
  Print
  Comments
  Residents of Mbezi Juu on Goba road, starting from Samaki area in Dar es Salaam, have called on government leaders to abide by laws while implementing its various development plans to avoid antagonism between the people and the leaders.
  The call was made on Sunday at a public meeting that brought together the residents from the area who met to discuss pending house demolitions under a plan aimed at widening the road that connects Samaki area and Bagamoyo road up to Mbezi Mwisho on Morogoro road.
  Chairperson of the meeting Dr Winfred Milinga, said the residents have been living in fear, not knowing exactly what was going on, saying the Tanzania National Roads Agency (TANROADS) simply sent a notice to the local government office about the pending demolitions without first having consulted the residents, who are the victims of the exercise.
  The letter, which was signed by Tanroads regional manager Nyabakari read that the government planned to rehabilitate the Goba road extending from Mbezi Mwisho to Samaki Wabichi area, adding that currently the aim was to establish a road reserve, which is 22.5 meters from the middle of the existing road.
  "The aim is to establish a road reserve area and warn the people not to erect buildings within the reserve area," the letter read in part.
  He said the letter was followed by forceful installation of beacons demarcating the road reserve.
  Milinga said he communicated with the Tanroads manager who agreed to come and explain to the people about what was going on, and that they had agreed that he would meet with the people last Saturday at 10am. However, even though the people had gathered there, the manager did not bother to attend.
  Retired Ambassador Fanuel Kuzilwa, who is also a resident of the area, said such government action which cause people to live in fear may end up causing antagonism between the people and government leaders, something which may pause a threat to peace and tranquility in the country.
  Another resident, retired ambassador Herman Martin Mkwizu, advised the government not to go ahead with the demolitions, especially since the road was not meant to be a highway.
  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona kila kitu kuelekea bagamoyo tu. Vipi kunani huko bagamoyo?
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kila raha na karaha zake.
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Unauliza saluti polisi!.
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mbezi mbona watatoa vilio wengi
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Tukubali maendeleo wakati mwingine hugharimu.....hii ni barabara muhimu sana ya 14 km mpaka Ukonga na itasaidia kupunguza foleni na msongamanao ubungo...muhimu watu walipwe fidia halali....wengi wanaona ndio pakutajirikia hapa ndio maana makelele mengi
   
 11. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio barabar hata umeme bado baadhi ya maeneo ya goba matosa
   
Loading...