Bombardier za ATCL kuanza kupasua anga hadi Kenya

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
atcl-ndege1.jpg

NDEGE mpya za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400 zinatarajia kuanza kutoa huduma za usafiri nchini Kenya kuanzia mwakani.

Hayo yalibainika jana wakati wa Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya Tanzania na Kenya uliofanyika Dar es Salaam kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali.

Akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Aziz Mlima alisema kati ya masuala watakayojadiliana ni kuanzia mwakani ndege hizo za ATCL kuanza kutoa huduma nchini Kenya.

Alisema kwa kuwa ndege za Kenya zinatoa huduma nchini, hivyo watajadiliana kuhakikisha huduma hiyo na nyingine zinafanyika kwa ushirikiano baina ya nchi hizo kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

Ndege hizo za ATCL zilianza safari zake Oktoba 14, mwaka huu na zinatoa huduma katika viwanja vya Mwanza, Zanzibar, Arusha na Kigoma kwa safari za ndani na Moroni, Comoro kwa safari za nje. Lakini mwezi huu wanatarajia kupanua huduma nchini na nchi jirani kwa kuongeza safari za Kilimanjaro, Mtwara, Dodoma na Tabora.

Akizungumzia mkutano huo, Dk Mlima alisema kwa mara ya mwisho mkutano kama huo ulifanyika mwaka 2012, hivyo kikao hicho kitajadili utekelezaji ya maazimio waliyofikia kwa wakati huo na changamoto zake ili kuweza kupata ufumbuzi.

“Kwa kawaida mkutano huu wa mahusiano baina ya nchi kwa nchi unatakiwa kufanyika baada ya miaka miwili, lakini kutokana na masuala mbalimbali ya kitaifa kama Katiba, Uchaguzi Mkuu na mengineyo tulishindwa kufanya hivyo,” alisema.

Alisema mkutano huo utatoa nafasi kwa wajumbe kujadiliana kisekta ili kuangalia maeneo mapya ya ushirikiano na njia zitakazowezesha kuimarisha ushirikiano kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

Naye kiongozi wa timu kutoka Kenya, Balozi Ben Ogutu alisema mkutano huo utatoa fursa ya kujadiliana katika sekta zote kutokana na historia ya ushirikiano baina ya nchi hizo mbili ulioanza tangu wakati wa uhuru.

Alisema wajumbe watangalia masuala mapya ya ushirikiano kwa kuangalia ule wa awali kulingana na mazungumzo ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais John Magufuli walipokutana hivi karibuni.
 
Kila la kheri halafu pia mboreshe viwanja vya ndani ni aibu kwa Kiwanja kama Arusha kusubiria kupambuzuke ndio huduma zianze kisa hakuna mataa kwenye runway ..halafu mkiweka na ka taxway kamoja itakuwa poa
 
Nani atapanda makarai
 
Vipangaboi vinataka kwenda Kenya, jamani mtatuletea aibu, subirini kwanza zije zile nyingine kubwa, haraka ya nini
 
Kila la heri ATCL you will grow big and big like Emirates one day.

Accountability and commitment of Management is vital

Words are words... hata yawe mazuri vipi, ni maneno tu, VITENDO NI VITU TOFAUTI SANA..!!

Hata hivyo vitendo vilianza na Idea ya MTU mmoja hatimaye a big company.

Shirika litakuwa kubwa na Twiga atafanya Global routes all over the six continents.
 
Back
Top Bottom