Ripoti kutoka Nigeria zinaarifu kuwa watu ishirini na wanane wamefariki baada ya bomba la mafuta kulipuka katika mji mkuu wa kibiashara wa Lagos.
Mlipuko huo ulitokea wakati watu wakichota mafuta baada ya bomba hilo kupasuka.
Vipande vya miili ya binadamu vilitapakaa kote kote baada ya mlipuko huo kutokea na waokoaji wamefika kusaidia waathiriwa na kuzima moto.
Mlipuko kama huo ulitokea mjini Lagos wakati kama huu mwaka jana na kuua zaidi ya watu mia mbili.
source:BBC
http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2004/06/000000_leoafrica.shtml