Bomba la mafuta Afrika Mashariki lajadiliwa Uganda

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,224
1,676
Mkutano unaohusu ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Bahari ya Hindi umeanza mjini Kampala nchini Uganda.

Mkutano huu unayashirikisha mataifa waanzilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki - Kenya, Uganda na Tanzania - ambapo baada ya siku tatu maafisa wa Serikali kutoka mataifa hayo wataamua iwapo Bomba hilo linafaa kutoka Uganda na kupitia nchini Tanzania hadi Bandari ya Tanga au kupitia Kenya hadi Bandari ya Lamu au Bandari ya Mombasa.

Bomba la kutoka Tanga hadi Uganda litakuwa na urefu wa kilometa 1,410 na litasafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima eneo la ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Bomba la kutoka Hoima na kwenda Lokichar kisha hadi Lamu linakuwa na urefu wa kilomita 1,476.

Pendekezo la kutoa mafuta Lokichar pamoja kisha kupitia Hoima nchini Uganda na kufika Tanga itakuwa na urefu wa kilomita 2,028.

Ingawa ripoti itakayojadiliwa imetoa njia tatu zinazoweza kutumiwa, ni dhahiri kuwa Kenya na Tanzania watakuwa katika hali ya kuchunguzana sana.

Mazungumzo ya mwezi mmoja uliopita kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Rais Museveni na wakati huo huo kati ya Rais Museveni tena na Rais John Pombe Magufuli juu ya swala la bomba la kupeleka mafuta hadi Bahari ya Hindi yamezusha uhasama baridi kati ya Kenya na Tanzania.

160302053744_john_magufuli_yoweri_museveni_640x360_statehousetanzania.jpg

Tayari vyombo vya habari nchini Tanzania vimesema kuwa Rais Magufuli na Rais Museveni washatia sahihi bomba hilo lipitie Tanzania hadi Bandari ya Tanga.

Mkutano uliofanyika nchini Kenya kati ya Rais Kenyatta na Rais Museveni juu ya bomba hilo, kufuatia mwaliko wa Rais Kenyatta, ulimalizika majuma machache yaliyopita bila suluhu yoyote.

Kila taifa hilo lina hamu ya kuhakikisha bomba la mafuta linapitia kwake kutokana na manufaa ya kiuchumi.

Mafuta ghafi ya Kenya hayako mbali sana na yale ya Uganda lakini ni wazi kwamba kuwa na bomba nchini ni biashara ya kipekee inayoleta faida zaidi.

Source: bbc
 
Mkuu,
Yote yaliyoelezwa katika safi yako ni kweli, Vuta nikuvute kati ya M7 na Uhuru imepelekea kuzua uhasama kati ya Kenya na Tanzania kukiwa na madai kwamba JPM ndie alietengua turufu ya Kenya kupitisha bomba hilo Nchi ni humo.
Ukitathimini swala hili kwa makini utaona pamoja na kwamba nchi waanzilishi wa jumuiya ni wana jumuiya halisi waliobaki wakiwa wasindikizaji tu, kuna mambo mengi yanayojitokeza kuonyesha tabia ya kila nchi kwa upande wa ushirikiano kujamii, kiuchumi hata kiitikadi, kwamba
Kuna nchi shiriki zenye tamaa na itakadi za ukandamizaji nchi nyingine.
Tunashirikiana tukidai jumuia lakini maana ya ukweli kijumuiya haipo ni kuchorana tu.
 
Katika modern societies kila mmoja kuvutia upande wake ni jambo la kawaida.
 
Mkuu,
Yote yaliyoelezwa katika safi yako ni kweli, Vuta nikuvute kati ya M7 na Uhuru imepelekea kuzua uhasama kati ya Kenya na Tanzania kukiwa na madai kwamba JPM ndie alietengua turufu ya Kenya kupitisha bomba hilo Nchi ni humo.
Ukitathimini swala hili kwa makini utaona pamoja na kwamba nchi waanzilishi wa jumuiya ni wana jumuiya halisi waliobaki wakiwa wasindikizaji tu, kuna mambo mengi yanayojitokeza kuonyesha tabia ya kila nchi kwa upande wa ushirikiano kujamii, kiuchumi hata kiitikadi, kwamba
Kuna nchi shiriki zenye tamaa na itakadi za ukandamizaji nchi nyingine.
Tunashirikiana tukidai jumuia lakini maana ya ukweli kijumuiya haipo ni kuchorana tu.
Mgaagaa na upwa,
Asante umenisoma.
Kwa kukumbusha tu na wote mnaosoma nyuzi hii ni kwamba,
Mtakumbuka hapo nyuma kidogo ilitokea tofauti kati ya Mh Kagame na Ndugu yetu Mh JMK.
Rais wetu mstaafu alitoa ushauri mzuri sana kuhusu usalama katika maeneo ya Rwanda na DRC, Kagame akachukizwa na ushauri huo akadiriki kuleta Kashfa na Chuki kwa Rais na wananchi wake.
Nilikuwa Rwanda na mpaka sasa hivi ni mkazi wa Rwanda.
Tulishuhudia wimbi hili kutugusa na kuathiri mambo yetu mengi kama Visa, haki za kijamii n.k. kitu ambacho kwa chi zilizo chini ya mkataba wa kijumuiua hali hii haistahili kutokea.
Kibaya kilichotokea na ninachokizungumzia kwamba ni itikadi ya nchi moja kukandamiza nyingine ni kwamba Uhuru alimwita M7 huyo ambae wameshindwana sasa wakaungana na Kagame kwamba wajenge reli kutoka Mombasa hadi Kigali bila kuwashirikisha Burundi na Tanzania kitendo kilicholeta minong'ong'ono mingi lakini sisi tukijikinga kiungwana tukajitetea kiunyonge kwamba haidhuru ilikuwa sawa kikatiba.
Walimalizia kuazimisha na kurahisisha movement kwa raia
wa Rwanda,Uganda na Kenya kuingiliana kwa National Identities na sio Passport wakiziacha nyumba Burundi na Tanzania katika Azimio hilo hapa ndio utaona ubinafsi uliopo kati ya nchi na nchi. Leo hii Kenya wanalalamika nini? Mkuki kwa nguruwe?
Ukurasa mpya haukuchelewa kufunguka. uhusiano mpya umejitokeza kati ya Rwanda na Tanzania.
Ziara ya kwanza ngosha amefanya nje ni kwa mtutsi wetu Kagame
Lakini ninachohisi sasa kwamba kitazidi kuzorotesha uhusiano wetu na Wakenya ni yule kiboko yao kwasili Tanzania na kuhudhuria misa tena Chato! Kuna minong'ong'ono mingi sana nchini Kenya ambayo nahisi itapelekea Uhuru na JPM kuwa maji na Mafuta na hasa ukitilia maanani kwamba inadaiwa Raila na JPM ni maswahiba wa kweli tangu wakati uuuleee! Wa meli za Dewji. Wapembuzi pembueni.
 
Back
Top Bottom