Bomba la gesi toka mtwara hadi tanga; inanifanya nianze kufikiria sera ya majimbo ya chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomba la gesi toka mtwara hadi tanga; inanifanya nianze kufikiria sera ya majimbo ya chadema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PascalFlx, Jun 28, 2011.

 1. P

  PascalFlx Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "Kwa uchumi na usalama wa nchi serikali ya Tanzania inapaswa kufanya maamuzi mazito na kuwasilisha maombi bungeni ya kutenga kiasi cha Shilingi Bilioni 131 ambacho kinahitajika kama sehemu ya kuchangia asilimia 15 ya mkopo kwa ajili ya mradi wa Bomba la Gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es salaam na baadaye hadi Tanga. "

  Niliposoma hayo maneno yaliyopo juu yamenifanya niandike yafuatayo

  Maamuzi mengi sana ya kisiasa yanayofanyika katika nchi yetu yanaanza kunifanya nianze kufikiria uhalali wa kuwa na Majimbo (States) kama ilivyopendekezwa na Chadema.
  1. Ni kitu gani kinachoilazimisha Serikali kutoa rasilimali toka sehemu moja ya nchi na kuipeleka sehemu nyingine ya nchi kwa gharama ya mabilioni ya shilingi, badala ya kutumia fedha hizo kuanzisha hicho kiwanda pale zilipo hizo rasilimali.
  Tumeshaona songas ilivyosafirishwa toka Kilwa hadi Dar es salaam na gharama zilizoingia, tunashukuru mungu hadi sasa hakuna hujuma zozote zilizofanya katika bomba hilo,
  Je ni vizuri kufanya - assumption kuwa tatizo kama hilo halitatokea?, kwani hatuna uwezo wa kulinda kila sentimeta ya bomba hilo.
  Sasa kuna huu mpango mpya wa kuweka bomba lingine toka Mtwara hadi Tanga.
  Hivi Jamani Kusini kuna nini?, Tayari investment nyingi sana zimeiruka mikoa ya kusini lakini imejitokeza yenyewe kutokana na rasilimali zake bodo tunataka kuhakikisha kuwa hoa watu hawafaidiki chochote na rasilimali zao zaoidi ya kuona bomba linalosafirisha hiyo gesi kupeleka Tanga kuzalishwa umeme hicho kiwanda hakiwezi kuzalishwa huko Mtwara?, Basi afadhali gesi hiyo ingepelekwa Dodoma at least tungesema ni katikati ya nchi ni rahisi kuusambaza huo umeme utakao zalishwa ila kwa nini Tanga?, nimejiuliza sana swali hilo na nimeanza kutazama sera za vyama vya upinzani vinasema nini kuhusu hili.
  Sasa naanza kuingiwa na ushawishi wa kukubali sera ya majimbo kwani sera hiyo haitoa maamuzi ya upendeleo kutoka State moja kwenda nyingine na nina hakika kutakuwa na Maendelea ya haraka kuliko kuweka pesa/rasilimali zote katika chungu kimoja cha Serikali kuu ambacho kila mtu anaweka mkono wake kuchota.
  Tubadilishe mtazamo tuangalie hali halisi tusiruhusu maamuzi ya kisiasa yaharibu kidogo tulichonacho
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ndugu yangu tatizo kwanza wabunge wa kusini hawana umoja katika kutetea rasilimali zao ambazo zinahamishiwa mikoa mingine na pili ni kwamba wabunge wengi wakishachaguliwa wanakimbilia dar es salaamu hawataki kuishi mikoani mwao utawaona huko kipindi cha uchaguzi tu hapo unategemea watatetea kweli rasilimalizao??na tatu ni upumbavu wa wananchi wenyewe wanawachagua watu ambao wanawajua fika kwamba hawana msaada wowote kwa majimbo yao wewe unadanganywa kwa kanga,tshirt na kofia kisha unachagua mtu unategemea kitatokea nini hapo!matokeo yake ndio hayo gesi inatoka kusini inaenda kusaidia watu wa tanga halafu jiulize reli za tanga na mtwara na lindi zilikufa na nini??kwasababu serikali ina dharau kwa watu wa mikoa hiyo!
   
 3. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mikoa ya kusini haina mwenyewe ni shama la bibi. Waache Magamba wapate ujiko kupitia raslimali za kusini.
   
 4. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpumbavu mwenyewe, sisi sio wapumbavu.hao unaowashabikia wamewahi kukuletea ugali.
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni kwamba Tanga kuna mazingira mazuri ya Viwanda. Kuna Bandari, kuna barabara nzuri sana, kuna wafanyakazi ambao wengi wanatoka mikoa mingine na hakuna ugomvi wa viwanja. Chakula na gharama za kuishi Tanga ni ndogo sana. Hivyo mimi ningeshauri hao wabunge wangeanza na barabara za mijini na bandari!. Huwezi kumlazimisha mwekezaji sehemu ya kuwekeza bali unaweka vivutio.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  ..kuna kipindi nchi ilikuwa inategemea kahawa,pamba,na mkonge.

  ..mazao hayo yote hayapatikani kusini mwa Tanzania.

  ..umeshajiuliza wakati mikoa ya kusini ilipokuwa na hali mbaya kiuchumi na hivyo kushindwa kuchangia serikali, nchi hii ilikuwa inaendeshwa kutokana na rasilimali kutoka wapi?

  ..inawezekana hata gharama za utafutaji na hatimaye uchimbaji wa gesi huko kusini zimetokana na mapato yaliyopatikana kutokana na rasilimali za maeneo mengine.

  ..ukiona gesi inasafirishwa toka eneo A kwenda eneo B inamaanisha kwamba eneo B ndiyo lina matumizi ya gesi hiyo.

  ..kwa sasa hivi wacha gesi hiyo ikatumike Tanga,DSM,na kwingineko ambako kuna mahitaji makubwa ya umeme kuliko kusini.

  ..mapato yatakayopatikana yatatumika kuwekeza ktk miundo mbinu itakayovutia uanzishaji wa viwanda na shughuli nyingine zenye mahitaji ya umeme huko kusini.
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  napingana na wewe kitu kimoja ni kwamba kusini kuna bandari na lindi wamekwishawahi kulima mkonge na ndio maana kulijengwa reli huko 3 pale mtwara kuna bandariu yenye kina kirefu kuliko zote east africa kwanini serikali isiwekeze huko kwasababu bandari po jirani hivyo ni rahisi kushusha na kupakia mizigo wangeimarisha ilale barabara ya lami ya tunduru masasi mpaka mbamba bay ili bandari ya mtwara isaidie kuinua uchumi wa kusini na hatimae kupata ajira sasa ukitoa bomba hilo toka mtwara au kusini kwenda tanga unatarajia vijana wanaokosa ajira watakua wanaliangalia tu??mali zao zinaenda kufaidisha watu wa tanga!!!mimi bado naona ni bora kuimalishwe kusini na watanga wafikirie cha kuanzisha kutokana na viwanda walivyo navyo pia naunga mkono hoja ya chadema ya utawala wa majimbo
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  Kilimasera,

  ..nimechungulia data za TRA kuhusu makusanyo ya kodi 2006/07.

  ..mkoa wa Lindi walikusanya 942 mil, Mtwara walikusanya 1.9 billion, Tanga walikusanya 82 billion.

  ..hivi Tanga wakisema makusanyo yao ya kodi yatumike Tanga tu, na yasipelekwe Lindi au Mtwara serikali itaweza vipi kuwekeza huko kusini?

  ..binafsi nadhani wa-Tanzania hatuko tayari na hii sera ya majimbo. nakuhakikishia umajimbo utatuchanganya na nchi haitatawalika.

  ..sikubaliani na hii dhana kwamba kile kinachopatikana ktk sehemu A[Mtwara] in this country kisitumike ktk sehemu B[Tanga] hata kama sehemu B wana matumizi nacho zaidi, na wanaweza kulifaidisha taifa kwa haraka zaidi.

  ..nakubaliana na wewe kwamba serikali inapaswa kuiwezesha zaidi mikoa ya kusini ili iweze ku-contribute ktk pato la taifa kama mikoa mingine, mathalan Tanga na Arusha inavyofanya.

  NB:
   
 9. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Kiifupi na Kihistoria mji wa Mtwara ni mji wa mwambao ambao upo kusini mwa Tanzania yetu ambao kipindi cha ukoloni ulikaliwa na waarabu toka mashariki ya kati, ni mji ambao unajulikana kihistoria zaidi kwa kuwa na ngome kubwa ya Waarabu pale Mikindani(Museums) .

  Hauna tofauti na ule mji wa bagamoyo kihistoria ila tofauti t uni kwamba yale majengo ya mikindani ambayo yalistahili kuwa makumbusho na ni vivutio kwetu si wenyewe na wageni, yamekwisha mno kiasi cha kwamba hayana tena thamani na mengi yameshabomoka kwani hayajawahi kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile kwa kipindi kirefu sana. Mji huu ambao kwa sasa unaitwa Mtwara-Mikindani, hapo mwanzo ulikuwa unaongozwa na kutawaliwa na waarabu ambao baadae walijichanganya na wenyeji na kuzaliana, ni mji ambao wakazi wake wengi ni waislam. Nimeanza hivyo kwakuwa huenda watu walio wengi wanausikia tu huu mji labda kwa umaarufu wake kwa kuwa na zao la korosho, na wengine hawaujui kama huu mkoa upo upande gani wa Tanzania(kusini ukiambatana na mipaka ya msumbiji na Malawi).

  Sasa ni hivi, kwa muda mrefu sana,tangu mimi nimezaliwa huu mji unapiga hatua polepole sana na kwakweli mwendo huu wa kobe sijui kama tutafika kule ambako watanzinia wengi watashawishika hata kuja mara moja kuuangalia. Uongozi na usimamizi mbovu wa viongozi ambao wapo kwenye mji huu kwa kweli unakatisha tamaa sana, na hapa ndipo mada yangu inapoanzia. Sina lengo la kuzungumzia udini katika inshu nzima ya uongozi katika jimbo hili la mtwara mjini la hasha ila itanilazimu niongelee swala hili kwani ndio ukweli uliopo na ndio vitu vinavyofanyika pale.

  Tangu kipindi kile cha miaka ya sabini ambapo kulikuwa na mfumo wa chama kimoja hadi hii leo wabunge waliongoza jimbo hili ni Waislamu, kumbukumbu zangu zinaniambia kwamba kipindi kile nilivyozallliwa kulikuwa na Mbunge toka CCM anaitwa Mzee Mkanyama, huyu bwana hata sielewi sasa hivi yupo wapi,baada ya hapo wabunge waliofuatia ninaowakumbuka ni Mpeme, Sinani na sasa ni Murji aliyepitshwa na CCM. Mchakato mzima wa kuwapata hawa mabwana kiukweli ni udini ulishamiri katika pande hizi. Ikumbukwe kwamba tangu mwaka 1995 pale Rais Mstaafu BENJAMIN WILLIAM MKAPA kutawazwa kuwa raisi, nlidhani ndicho kitakuwa kipindi kizuri kwa watu wa mtwara kuneemeka kupitia mbunge wake Mpeme kuleta maendeleo jimboni.

  Mchakaato wa kumpata huyu bwana ambae kiukweli elimu yake bila shaka ni chini ya darasa la saba, ulijaa udini sana, nasema hivi kwasababu mkapa alimpendekeza mtu mmoja Mr Kambona achaguliwe kupitia CCM,huyu bwana hakupewa hii nafasi na wazee wa kiislamu kwa ile sababu tu eti huyu bwana ni ‘’kafri’’ kwani ameishi sana Italia ambako akiwatumikia wakristu(alikuwa barozi wa Tanzania nchini Italy),kwahiyo hafai kuongoza mtwara eti tu kuna waislamu wengi, vp inaingia akilini kweli? Ndo hivyo wazee wakaamua na kusema kwamba hatuwezi kuongozwa na kafri.

  Taabu ilikuwa kwa wale wagombea wenzake waliopita kwenye kura za maoni!,walitishiwa kuuawa na Mpeme kwa mtu yeyote atakayepata ubunge mbali na yeye. Aliwafanyia vibweka wagombea wenzake mpaka akapata ubunge . cha ajabu miaka yote mitano hakuwahi kuzunguza lolote pale bungeni zaidi ya kulala tu. Mwaka wa 2000 uchaguzi mkuu,wale wazee wa kiislamu wakamchagua tena huyu bwana awe mgombea,akapata ubunge na hakuongea lolote bungeni hadi alipomaliza utukufu wake.

  Mwaka 2005 kwa mshangao wazee wa pale mjini wakamtipisha mtu mwenye uraia wa msumbiji ambae tena elimu yake nadhani kama sio chini la darasa la saba basi ni si zaidi ya form four,huyu ni Mr Sinani agombee kwa tiketi ya CCM kama mbunge, akapata ubunge, hakuongea lolote bungeni hadi miaka mitano ikapita. Funika kombe mwanaharamu apite, huyu bwana akagombea tena na akabwaga vibaya na mgombea mwenzake (mfanyabiashara maarufu wa kihindi na sio mwenye asili ya kihindi,hapana, ni mhindi) . habari ndio hiyo mtwara imesahaulika sana
   
 10. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Napenda my homie , mtwara""!
   
 11. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Hizo bado ni hadithi...
   
 12. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mkuu unauhakika na ulichokiandika? Kama hujui mchango wa mikoa ya kusini na masahibu yaliyowapata kabla na baada ya uhuru "bora utulie au upige marimba, utaskika pia". Au umesahau kuwa mikoa ya kusini ilikuwa chaka la kuficha wapigania uhuru wa nchi takriban zote za kusini mwa bara letu? Kwa hali hiyo kuanzisha miradi mikubwa ingeweza kusababisha hujuma za ulipizaji kisasi kutoka kwa wapinga ukombozi!!? Jambo la kusikitisha ni kuwa baada ya nchi zile kukombolewa juhudi hazikuwekwa kurekebisha hali hiyo.
   
 13. J

  JokaKuu Platinum Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  Mwendabure,

  ..ya nini kuandikia mate wakati wino upo.

  ..nimekuonyesha data hapo toka TRA zikionyesha makusanyo ya kodi Mtwara + Lindi vs Tanga.

  ..mimi sipingi kwamba serikali inapaswa kuwaangalia na kuwawezesha ili muweze kufikia your full potential.

  ..nisichopendezwa nacho ni jinsi hoja ilivyowasilishwa kwa njia ya ukanda-ukanda, umajimbo-majimbo, wakati tunajitahidi kujenga NCHI.
   
 14. P

  PascalFlx Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana kabisa na mwendabure,
  hizo takwimu za TRA, kwanza kabisa zinatokana na Bandari ya Dar es salaam kuvurunda hivyo kutumia ya Mombasa.
  Lakini hiyo haitoi justification ya kuchukua hata hicho kidogo kilichopo na kukipeleka Tanga,.
  Tanga haina tofauti kubwa na Zanzibar na Bagamoyo, nenda Pangani uone uchapakazi wao.
  Hata kama aliyenacho anaongezewa sio kiasi cha kudhulumu/kuondoa kidogo alichonacho mwingine hebu tusubiri hayo makaa ya mawe wataamua nini, maana Southern Province inahusisha Lindi Mtwara na Ruvuma.
   
 15. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Mkuu unauhakika na ulichokiandika? Kama hujui mchango wa mikoa ya kusini na masahibu yaliyowapata kabla na baada ya uhuru "bora utulie au upige marimba, utaskika pia". Au umesahau kuwa mikoa ya kusini ilikuwa chaka la kuficha wapigania uhuru wa nchi takriban zote za kusini mwa bara letu? Kwa hali hiyo kuanzisha miradi mikubwa ingeweza kusababisha hujuma za ulipizaji kisasi kutoka kwa wapinga ukombozi!!? Jambo la kusikitisha ni kuwa baada ya nchi zile kukombolewa juhudi hazikuwekwa kurekebisha hali hiyo.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,775
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  PascalFlx,

  ..soma data za ukusanyaji mapato.

  ..in 2006/07 Mtwara na Lindi kwa pamoja walikusanya about 3 billion, wakati Tanga walikusanya 82 billion.

  ..kwa msingi huo mikoa kama Lindi na Mtwara inaishi kwa kutegemea mikoa yenye makusanyo makubwa kama Tanga, au Arusha.

  ..kinachopaswa kufanyika ni kuhakikisha Mtwara na Lindi nao wanainuka wakati huo huo tukihakikisha Tanga,Arusha, etc nayo inaendelea kushamiri.

  ..gesi inayopatikana Mtwara inaweza kabisa kutumika hapo Mtwara, na kiasi kingine ikasafirishwa na kutumika maeneo mbalimbali ya Tanzania.

  ..
   
 17. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mkuu mbona mimi naona kama sasa hv nchi ndio inashindwa kutawalika vizuri sijui lakini ni mtazamo tu kukubwa naamini kwamba tukiwa na haya majimbo kila watu watakaa na kujipangia mipango yao wenyewe thabiti ya maendeleo kutokana na resource zao walizo nazo naona kama ufisadi,ukabila na unduku umekua kwa kasi sana tanzania sasa hv bila kumjua mtu hupati kazi rushwa imekua kila sehemu makazini watu wamekua wavivu sana na serikali inashindwa kabisa kuzuia yote hayo kutokana na ukubwa wa nchi!mie nadhani devide and rule tukiapply hapa tunaweza kupata mwanga!
   
Loading...