Bomani Naye!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
Kamati Maalum ya kupitia mikataba ya madini bado kukabidhi ripoti
Na Kizitto Noya

KAMATI Maalum ya kupitia upya mikataba ya madini haijakabidhi ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete tangu ilipokamilisha kazi yake Aprili 10, mwaka huu.


Habari zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji Mark Bomani zimesema kuwa mpaka sasa ripoti hiyo haijamfikia Rais Kikwete.


Kwa mujibu wa Jaji Bomani baada ya kumaliza kazi ya kuandaa ripoti hiyo, kamati imeomba miadi ya kukutana na rais Kikwete ili ikamkabidhi ripoti hiyo na sasa inasubiri wito wake kwa ajili ya makabidhiano hayo.


"Ni kweli kazi imekamilika, lakini sijaikabidhi, nimeomba kukutana na Rais ili nimkabidhi. Nasubiri wito wake," alisema Jaji Bomani.


Kazi ya kuangalia upya mikataba ya madini imeichukua kamati hiyo yenye wajumbe kumi moja miezi sita kuikamilisha badala ya miezi mitatu kama alivyoelekeza Rais Novemba 13, mwaka jana alipoiunda kamati hiyo.


Mbali na Bomani, wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera katika Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.


Wengine ni Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.


Rais Kikwete alitaka kamati hiyo pamoja na mambo mengine kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali.


Rais pia aliitaka kamati hiyo kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutoa taarifa yenye mapendekezo ya kuboresha mikataba ya madini.


Kuundwa kwa Kamati hiyo kulifuatia hoja binafsi ya Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa Kamati Teule ya kuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa Mkataba wa Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, nchini Uingereza na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi mwaka jana
 
sasa hii inahusiana vipi na ukumbi wa michezo? Tuwe wastaarabu jamani
 
Back
Top Bottom