Bomani: Dowans sasa imetugharimu • Ataka mitambo ya Dowans ibakishwe nchini


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,611
Likes
634,713
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,611 634,713 280
Bomani: Dowans sasa imetugharimu
• Ataka mitambo ya Dowans ibakishwe nchini

na Irene Mark


amka2.gif
MWANASHERIA Mkuu wa kwanza mzalendo, Jaji Mark Bomani amesema hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC), iliyoipa ushindi kampuni ya Dowans dhidi ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ni matokeo ya namna taifa lilivyolishughulikia isivyo suala hilo. Jaji Bomani, mmoja wa wanasheria wanaoheshimika nchini, alisema hukumu hiyo ni kielelezo cha wazi kwamba, masuala yanayohusu mikataba ya kimataifa kama hayo yanapaswa kushughulikiwa kwa umakini mkubwa ili kuepuka gharama za namna hiyo.
“Sakata la TANESCO na Dowans linasikitisha. Nafikiri liliendeshwa kwa namna ambayo ingewafikisha wahusika pabaya kama ilivyotokea,” alieleza jaji huyo aliyeonyesha dhahiri kutoridhishwa na namna siasa ilivyoingizwa katika suala hilo ambalo kwa maelezo yake alisema lilipaswa kushughulikiwa kwa umakini mkubwa.
Alipotakiwa kueleza ni fundisho gani hasa Tanzania kama taifa linapaswa kujifunza kutokana na hukumu hiyo ya ICC ambayo inaitaka TANESCO/serikali kuilipa Dowans kiasi cha shilingi bilioni 185, Jaji Bomani alisema umakini mkubwa unatakiwa kutumika unaposhughulikia masuala yanayohusu mikataba ya kimataifa.
“Fundisho ni kwamba unaposhughulikia masuala yanayogusa mikataba ya kimataifa kama haya yanayohusu nishati, madini na mengineyo, umakini mkubwa unatakiwa,” alisema Jaji Bomani ambaye alipata kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kupitia Mikataba ya Madini.
Akieleza ni nini basi kama taifa tunapaswa kufanya, Jaji Bomani alisema haoni uwezekano kwa TANESCO au serikali kutolipa kiasi hicho cha fedha kilichoamriwa katika mahakama hiyo ya kimataifa ya usuluhishi labda tu pale pande zinazozozana zitakapokubaliana vinginevyo.
Jaji Bomani aliyekuwa akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jijini Dar es Salaama jana alisema, “Ukiachilia mbali historia ya jambo hili, labda nitoe mawazo yangu juu ya kujikwamua kutoka hapa tulipofika....Kwanza hiyo award ya mabilioni. Hii sijui kama inaweza epukika labda wahusika wakubaliane vinginevyo.”
Novemba 15 mwaka huu, ICC ilitoa hukumu iliyoitaka TANESCO kuilipa Dowans sh bilioni 185 baada ya kuvunja mkataba wa kuzalisha umeme kinyume cha taratibu.
Akiizungumzia mitambo ya Dowans ambayo ingali bado nchini, alisema jambo jingine la msingi ni kujiuliza iwapo bado kuna dhamira ya kweli ya kuiondoa mitambo hiyo nchini halafu taifa lilazimike kuagiza mitambo mingine kwa gharama kubwa zaidi.
“Kwa maoni yangu, TANESCO au serikali wangekubaliana mitambo hii ibaki nchini ili tuiepushe nchi kutokana na balaa la mgawo wa umeme…Nasikia mitambo hiyo ya Dowans ina uwezo wa kufua umeme wa kiasi cha megawati 100 ambalo inaonekana ndilo pengo lililopo kwa sasa hivi.
“...Nasikia pia mitambo hiyo inaweza kuwashwa katika muda mfupi ukilinganisha na miezi mingi ya kusubiri ukiagiza, labda zaidi ya mwaka,” alisisitiza jaji huyo.
Jaji Bomani aliyewahi kuhusika kwenye ufumbuzi wa migogoro ya kimataifa, alisema suala la umeme sasa ni ajenda ya kufa na kupona na kwamba sio jambo la mzaha badala yake viongozi na wataalam wanatakiwa kulivalia njuga ili kulimaliza haraka iwezekanavyo.
Awali, serikali kupitia TANESCO mwaka 2006 iliingia mkataba uliodaiwa kuwa na harufu ya rushwa kwa ajili ya kuzalisha megawati 100 za umeme na kampuni ya Richmond Development LLC ili kuiokoa nchi na giza kwa kukosa umeme kulikotokana na ukame.
Mjadala wa mitambo ya Dowans, uliwahi kuligawa taifa kwa kipindi kirefu mwaka 2008 baada ya Kamati teule ya Bunge chini ya Uenyekiti wa Dk. Harrison Mwakyembe, kutoa taarifa ya kuchunguza uhalali wa kampuni ya Richmond na mtakaba baina yake na serikali.
Kutokana na taarifa iliyowasilishwa bungeni Februari mwaka 2008 aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alijiuzulu ikiwa ni ishara ya kuwajibika kama kiongozi mkuu wa ofisi yake iliyodaiwa kushiriki katika kuiwezesha Richmond kushinda zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.
Wakati wa mjadala huo, aliyekuwa Mkurugenzi wa TANESCO, Dk. Idris Rashid, aliishauri serikali kuinunua mitambo hiyo jambo lililoungwa mkono na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Kabwe Zitto (CHADEMA), huku akipingwa vikali na wa wanzake ndani na nje ya chama chake.
Hata hivyo, Bunge lilikataa kupitisha pendekezo la ununuzi wa mitambo ya Dowans likisema kufanya hivyo ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2004 inayokataza serikali au taasisi zake kununua mitumba.
Uamuzi huo wa ICC ulitolewa na jopo la majaji watatu chini ya uenyekiti Gerald Aksen na wasuluhihi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker.
Jopo hilo liliamuru TANESCO ilipe fidia ya zaidi ya sh bilioni 36 na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 tangu Juni 15 mwaka huu, hadi fidia hiyo itakapolipwa.
Kadhalika, jopo hilo liliamuru malipo ya sh bilioni 60 na riba ya asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.
Katika uamuzi huo, jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi wa ICC na utawala ni sh bilioni moja zinatakiwa kulipwa na pande zote.
 
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
9,876
Likes
1,712
Points
280
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
9,876 1,712 280
Nadhani haya ni manyunyu ya richmond, naota ndoto siku moja kamati ya mwakyembe juu ya richmond ikiwajibishwa kwa kuendesha mambo ya nishati kisiasa.
 
KICHAKA

KICHAKA

Member
Joined
Jun 17, 2009
Messages
58
Likes
4
Points
0
KICHAKA

KICHAKA

Member
Joined Jun 17, 2009
58 4 0
Kuleni chakula bora cha kuujenga mwili na kujenga nyumba bora pa kulala pawe bora! Nani anaweza kuimba nyimbo hizi tena katika Tanzania ya sasa na ni nani naweza kuhamasisha wananchi kula chakula bora ilihali anafahamu hakipo? Tutakula sana haya Madowans ili wanasiasa wanaotafutana katika maslahi yao wakibaki wakicheka
 
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,230
Likes
7,043
Points
280
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,230 7,043 280
Kuleni chakula bora cha kuujenga mwili na kujenga nyumba bora pa kulala pawe bora! Nani anaweza kuimba nyimbo hizi tena katika Tanzania ya sasa na ni nani naweza kuhamasisha wananchi kula chakula bora ilihali anafahamu hakipo? Tutakula sana haya Madowans ili wanasiasa wanaotafutana katika maslahi yao wakibaki wakicheka
TANZANIA+onion_news1703+...jpg
 

Forum statistics

Threads 1,237,207
Members 475,501
Posts 29,281,441